CCM taabani kifedha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM taabani kifedha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 1, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  CCM taabani kifedha
  Friday, 31 December 2010 20:56

  [​IMG]Katibu wa chama cha mapinduzi,Yusuph Makamba

  Hussein Issa na Habel Chidawali, Dodoma
  MAMBO si shwari ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana taarifa kwamba kiko taabani kifedha, kiasi cha kulazimika kusitisha kutoa ruzuku kwa baadhi ya watendaji wake kwenye ngazi za mkoa, wilaya na kata.

  Usitishwaji wa ruzuku unadaiwa kuzikumba pia taasisi zilizopo chini ya chama hicho vikiwemo vyombo vyake vya habari ambavyo ni Uhuru Publications Ltd, wanaozalisha magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani pamoja na Radio Uhuru.

  Habari zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa hali hiyo inatokana na chama hicho kupunguziwa ruzuku kufuatia kupata idadi ndogo ya wabunge wa kuchaguliwa katika Uchaguzi Mkuu uliomalizika Oktoba 31 mwaka huu ikilinganishwa na idadi ya wabunge hao katika miaka mitano iliyopita.

  Kwa mujibu wa habari hizo, kabla ya Uchaguzi Mkuu CCM ilikuwa inapokea ruzuku ya Sh1.2 bilioni kwa mwezi, lakini baada wabunge wake kupungua kwenye uchaguzi wa Oktoba 31, mwaka jana, sasa chama hicho kinapokea ruzuku ya Sh 800 milioni.

  Mmoja wa makatibu wa CCM wa wilaya mojawapo mkoani Dodoma aliliambia Mwananchi kuwa: "Hali sasa ni mbaya na kimsingi mambo mengi yamekwama kufanyika kwa wakati".

  Habari za uhakika kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa CCM kimekata ruzuku hiyo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kupungua kwa fedha kulikotokana na idadi ndogo ya kura za wabunge kufutia kufanya vibaya katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31 jana.

  Idadi ya wabunge wa CCM katika Bunge la sasa imepungua kwa zaidi ya asilimia kumi ililinganishwa na idadi kiliyokuwa nayo katika Bunge lililipota.

  Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa chama hicho kina wabunge 258 katika Bunge la Kumi sawa na asilimia 75.3 ya wabunge 343 waliopo, wakati katika Bunge lililopita kilikuwa na wabunge 271 ambao ni sawa na asilimia 85.7 ya wabunge 316 wa Bunge hilo la tisa lililomaliza muda wake mwishoni mwa mwaka jana.

  Wakati CCM kikipoteza asilimia zaidi ya kumi ya nafasi za uwakilishi bugeni, vyama vya upinzani vilifanikiwa kuongeza idadi ya wawakilishi wake ambapo hivi sasa vina wabunge 84 sawa na asilimia 24.7 ikilinganishwa na Bunge lililopita ambalo lilikuwa na wabunge wa upinzani 45 sawa na asilimia 14.3.

  Kutokana na hali hiyo ni dhahiri kwamba kiasi cha ruzuku kinachotolewa na Serikali kwa CCM kimepungua kutokana na wabunge wake kupungua huku kiasi kinachokwenda kwa vyama vya upinzani kikiongezeka.

  Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, alisema kuwa kupuguzwa kwa ruzuku hakuwarudishi nyuma kwa sababu chama chao ni kikongwe hivyo hakiwezi kutetereka kama vyama vingine.

  Makamba kuwa chama hicho hakiishi kwa ruzuku hivyo kitaendelea kama kawaida kwani kimeanza tangu mwaka 1954, kinajua nini maana ya kuongoza na hakibahatishi.

  "Wewe kijana nani kakuambia CCM kinaishi kwa kutegemea ruzuku, hiki ni kikongwe yaani chama kianze tangu mwaka 1954 leo hii uniambie suala la ruzuku, wewe vipi bwana?"alisema Makamba huku akicheka

  Aliongeza kuwa kuna watu walifikiri chama kinakufa, lakini wamekosea kufikiri hivyo na kwamba CCM hakiwezi kufa na kitaendelea kukua hata pasipo ruzuku.

  Hata hivyo, uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa viongozi wa ngazi za mikoa, wilaya, kata na matawi wa CCM, walikuwa wakipata fedha hizo kwa ajili ya kukiimarisha chama kwenye ngazi hizo, lakini sasa hawapewi tena.

  CCM ilikuwa ikitoa ruzuku ya Sh 5000 kila mwezi katika ngazi za matawi, Sh10,000 ngazi ya kata na Sh50,000 ngazi ya wilaya.

  Wajumbe wengine katika wilaya ambao walikuwa wakipewa posho hizo ni na Katibu wa Itikadi na Uenezi na Katibu wa Uchumi na Fedha ambao walikuwa wakipewa Sh20,000.

  Kwa nafasi ya mkoa, Mwenyekiti alikuwa akipewa posho ya Sh75,000 na Katibu Mwenezi wa Mkoa na Katibu wa Uchumi na Fedha walikuwa wakilipwa Sh50,000.

  Chanzo hicho cha habari kimeeleza kuwa kutokana na kukatwa ruzuku hiyo, watendaji hao sasa wanatakiwa kuanza kujitegemea.

  “Yaani sisi tunashangaa kwa kuwa mbali na fedha wanazokatwa wabunge wetu katika mishahara yao, lakini bado kuna ruzuku ya zaidi ya Sh800 milioni ambazo tunalipwa kutoka serikalini, lakini, wanabaki nazo wao hii inatuumiza sana,” alisema kiongozi mmoja wa CCM mkoani Dodoma.

  Alisema kuwa wabunge wamekuwa wakikatwa fedha nyingi ambazo badala ya kubaki katika wilaya na majimbo wanakotoka fedha hizo zimekuwa zikipelekwa moja kwa moja makao makuu ya chama jambo ambalo wengi wamekuwa wakihoji.

  Kitu kingine ambacho kiongozi huyo amekilalamikia ni kitendo cha CCM kuwakata katika mishahara yao madiwani wote wa CCM, lakini pia fedha hizo zinapelekwa makao makuu ya chama.

  Katika kipindi cha mchakato wa Uchaguzi Mkuu CCM ilitoa posho kwa viongozi wote wa chama hicho kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa ambapo viongozi wa matawi, Mwenyekiti, Katibu, Katibu wa Uchumi na Katibu Mwenezi walikuwa wakilipwa Sh 5000 kila mmoja.

  Kwa upande wa kata, viongozi wa nafasi hizo walilipwa sh 10,000 kila mmoja na kwa upande wa wilaya kila mmoja alilipwa zaidi ya 100,000 kiwango ambacho kilipanda kwa ngazi ya mkoa pia.

  Haikufahamika mara moja mbunge mmoja wa CCM anakatwa kiasi gani, lakini kwa upande wa madiwani kila mmoja anakiachangia chama hicho Sh 10,000 kila mwezi katika posho yake jambo linalofanya CCM kuvuna fedha nyingi kwa madiwani pekee.

  Katika utaratibu wa Chama hicho hivi sasa viongozi hao watategemea kupata posho kutokana na makusanyo ya ada za wanachama ambazo watakuwa wakilipia kadi zao.

  Kila mwanachama wa CCM analipia kadi yake Sh1200 kwa mwaka ambapo makato yake ni pamoja na asilimia 50 kubaki kwenye tawi, asilimia 30 hupelekwa kwenye kata, asilimia 15 hupelekwa wilayani na zinazobaki hupelekwa makao makuu.

  Awali Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Kapteni George Mkuchika alisema pamoja na kulifahamu suala hilo hawezi kuzungumzia kwa sasa kwa sababu hataki kuhojiwa na waandishi wa Mwananchi.

  "Halo samahani sana nyie si mmesema mnatoka gazeti la Mwananchi, sitaki kabisa kulizungumzia suala hilo pamoja na kulifahamu kwaheri, "alisema Mkuchika na kukata simu.

  Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa alisema kuwa halifahamu suala hilo kabisa na wala hajasikia tetesi kama kuna kitu kama hicho kutoka ndani na nje ya chama.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Tatizo la CCM kila wakati limekuwa n matumizi mabovu ya fedha na uchagzu ujao hata milioni 400 kwa mwezi hawatakuwa nazo na hapo ndipo utakapoona makada wake wakianza kukikimbia chama hicho kwa sababu kinachowaweka pale ni ulaji tu na wala siyo itikadi....................
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Nijuavyo tarumbeta za Uhuru corporation sasa zinaanza kufikia ukingoni kaa ilivyokuwa kwa KANU ambapo gazeti lao ilifikia mahali mwaka jana likafungwa rasmi kwa kushindwa ushindani...............................na wenzetu wa Uhuru wako njia moja kuelekea kaburini...................
   
 4. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Teh he he he he he! DOWANS DEAL ITAWEKA MAMBO SAWA AFTER TANISKO KULIPA HIVYO VIJISENTI VETU JAMANI. DO NOT PANIC GUYS. Ndo maana wenzio wamekomaa na DOWANS usidhani ni bure.
   
 5. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  I would have said that this is the beginning of their end but i put my flag down!!!

  haya jamaa majizi ya kiaina haya. Nina wasiwasi alionao Nyangomboli wa deal za kifisadi kutumika kukiinua chama kifedha.

  Mbona tutuaumia Watanzania? Maana kwa tabia yao na kwa kuwa ndio wameshikilia dola sie wadogo lazima tutakiona cha moto kufidia upungufu wao
   
 6. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Safi sanaaaa! Mwanzo wa mwisho wa CCM unajiri!!! What we need is to reposition our grip on CCM's neck in 2015.... We are going to strangle it for sure!!!
   
 7. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Hapo sasa ni dalili ya kuanza kushikana mchawi.. Mil 800 wanapeleka wapi? Wacha magazeti, viwanja vya mpira na hata majengo wanayokodisha?

  Nadhani sasa ni wakati wa mgaguzi mkuu wa hesabu za serikali kupitia na mahesabu ya vyama vya siasa.. Wanakula hela sana hawa jamaa.
   
 8. N

  Nonda JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Tunaweza kujifurahisha kwa habari kama hii. lakini mimi sioni kama CCM will die soon.
  Kama uchaguzi ndio kwanza umekwisha basi hakuna chama cha siasa chenye mahela mengi hata kimoja kupita CCM. Kama CCM hawana basi na vyengine ni vivyo hivyo.
  Tusisahau Ruzuku 800mil kwa mwezi. Na hizo deals wanazozisuka....
  Bora tuache tu kufurahi,tukiyaamini haya maandishi ujuwe wanatutengenezea surprises nyengine..

  Kila siku tunasema hapa JF kuwa CCM wanawafadhili ambao uhai wao,ufisadi wao unategemea CCM kuendelea kuwa madarakani, halafu tunaamini kirahisi kuwa hawana hela...Wale wanaotegemea Urais baada ya Kikwete ndio wako tayari kuona CCM haina hela ya kujiendesha?
  Tufikirie tena...
   
 9. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Credit crunch?????!
   
 10. Mwalimu Makini

  Mwalimu Makini Member

  #10
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 5, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Msijesahau kuwa CCM wanakusanya hela nyingi sana kutoka kwenye viwanja vya maegesho, viwanja vya michezo na majengo waliyopoka baada ya kukataa kutekeleza hoja ya Marehemu Jaji Francis Nyalali kuhusu mali zote ambazo zilikuwa zinamilikiwa na chama kuwekwa kwenye mamlaka moja serikalini.

  H
   
 11. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #11
  Jan 1, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Yaani pamoja na mtandao wote waliojijengea wa mafisadi wanaoweza kukichangia chama Tsh Bilioni 1 bado waendelee kutegemea ruzuku?
  By the way, CCM kimeanza toka mwaka 1954 kwa reference gani? Yaani katibu mzima wa chama hata hajui historia ya Chama chake?
   
 12. M

  Mnyagundu Senior Member

  #12
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 3, 2008
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asie jua maana haambiwi maana!
   
 13. M

  Mnyagundu Senior Member

  #13
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 3, 2008
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa akili ya haraka huwezi amini mil 800 ni hela ndogo halafu mtu atupotezee mda kuwa ccm wameishiwa! Ndugu zangu humu JF tusiwe kama CHIRIKU likiletwa jambo basi tunadakia na kusema mwisho wao ni 2015 haraka haraka,tusiwe wavivu wa kufikiria jamani! tupime michango mingine! haya chama gani kinapokea zaidi ya mil 800 kama sio ccm! sasa kimeishiwa vipi? nahisi humu ndani kuna mamluki wantaka kutupoteza lengo kabisa! tuanze kujadili hali ya fedha ya ccm hapa? ni ujinga mkubwa!
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Jan 1, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,802
  Likes Received: 5,096
  Trophy Points: 280
  ..tuombe MUNGU hizo mil 800 ziwatoshe.

  ..otherwise these ppl can get very creative and come up with schemes like EPA.
   
 15. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #15
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,082
  Likes Received: 4,031
  Trophy Points: 280
  EPA part II in the making...
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Jan 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,801
  Likes Received: 83,173
  Trophy Points: 280
  Ukiona hivyo ujue kule hazina pia hakuna kitu, vinginevyo wangeshachota nyingi tu za kujikimu kwa muda mrefu.
   
 17. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,617
  Likes Received: 2,998
  Trophy Points: 280
  Hela wanazo na wanapata nyingi sana lakini hata wangekuwa nazo nyingi kiasi gani kwa vile CCM ni kama pakacha linalovuja, daima hawataona hela ya kiwango chochote kuwatosha. Hawa ni watu wa matumizi, hawajui priorities wakatiwote.
   
 18. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  na abdo watafulia sana maana pesa walizotumia kwenye kampeni za uchaguzi wa mwaka jana ilikua kufuru.
   
 19. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  mkuu ndio viongozi tulionao hao.hawana hakika na future yao thats why wananga'nga'nia madaraka.
   
Loading...