Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
Ili kuepuka mitandao na makundi maslahi ndani ya CCM kuvuruga ustawi wa chama na ili kutorudia makosa ya 2015 yaliyokipasua chama, ninashauri CCM imuue nyani bila kumuangalia usoni, ninamaanisha wote Nape na Polepole ni "madegenyanga" wachukuliwe hatua sawia ili ku-harmonize hali hii inayotishia mpasuko katika kipindi cha majaribu ya chama na kutoa funzo kwa wengine wenye tabia na nia kama zao. Ikumbukwe kwa CCM maandalizi ya uchaguzi mkuu mwingine yanaanza pale ambapo uchaguzi mkuu uliopita ulikoishia. Bila kujali Nape ana mizizi mirefu ya kihistoria kwenye chama kumzidi Polepole ambaye ni mtoto wa mkulima wa mihogo Tanga, vikao vifanye kazi ya msumemo ya kukata mbele na nyuma kwasababu wote wawili wana mtaji wa wanachama/wafuasi. Mwenye masikio na asikie, mwenye macho na aone, asomaye na afahamu.
Taswira zote kwa hisani ya google.
Taswira zote kwa hisani ya google.