Mwanantogakulya
Senior Member
- Mar 18, 2025
- 130
- 118
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara,Stephen Wassira alifanya ziara katika mkoa wa Simiyu kuanzia Machi 28-30 mwaka huu kwa kutembelea wilaya zote za mkoa huo ambazo ni Maswa, Meatu, Itilima,Bariadi na Busega.
Akiwa wilayani Maswa ambapo akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)katika wilaya hiyo alionya juu ya matumizi ya fedha kwa wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani.
Pia alionya kuwepo kwa makundi ndani ya chama hicho huku akisisitiza mkoa huo ndiyo kinara wa jambo hilo jambo ambalo linaweza kutumiwa na wapinzani kushinda katika uchaguzi mkuu ujao.
Ametumia muda huo kuwaonya viongozi wa CCM mkoa wa Simiyu ambao wanawatishia wanachama kuwa watawakata majina yao ili wasiweze kugombea nafasi za ubunge na udiwani.