CCM, siasa za visasi hazifai kamwe

CCM, siasa za visasi hazifai kamwe

tzkwanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
1,567
Reaction score
3,611
Kuna watu wamekatwa majina kwa sababu tu ni marafiki wa Membe. Sasa hivi CCM hata uhuru wa kuongea na mtu asiyepatana na mwenyekiti haupo. Taifa linakwenda wapi?

Kuna watu walitoa rushwa hadharani kama Kingwangala, Waitara na Gambo ila majina yamepitishwa. Kuna wengine wamekatwa kwa kisingizio cha rushwa. RPC wa Arusha pamoja na mkuu wa TAKUKURU walitolewa kisa rushwa za Gambo ila mtoa rushwa karudi wao wamekwenda na maji. Na siku zote Gambo waliambia nimetumwa na mwenyekiti nimtoe Lema ndio maana wakamuacha, leo ukweli upo hadharani.

Kuna watu walitumbuliwa kisa urafiki na Lowasa leo wamerudishwa na chama kimechonga maadui wengine feki, eti marafiki wa Membe.

Polepole na Bashiru mlimshauri mwenyekiti anunue wabunge wa CHADEMA na CUF leo hii mnalazimisha kuwanadi. Hao watu upinzani hawatakiwi na CCM hawatakiwi. Mwambe, Gekul, Katambi na Silinde walipigwa chini na wajumbe ila nyie mnalazimisha kuwapa ubunge.

Patachimbika; hizo ni dharau kubwa sana. Polisi hawawezi kushindana na nguvu ya umma. Mliona kilichotokea Tunduma? au mmepanga kumwaga damu za watu ilimradi tu Silinde ashinde?
 
Dah! mtu yoyote mwenye akili timamu hawezi kukubali huu ujinga. Magufuli ameleta madhara makubwa sana kwenye uhuru wa watu hapa nchini. CCM wanaugumia/wanaugulia maumivu kuliko hata wapinzani.
 
Dah! mtu yoyote mwenye akili timamu hawezi kukubali huu ujinga. Magufuli ameleta madhara makubwa sana kwenye uhuru wa watu hapa nchini. CCM wanaugumia/wanaugulia maumivu kuliko hata wapinzani.
Kwa alivyomdhalilisha mzee Kinana Mie ndo nikichoka. Mtu aliyeishi kwa kuheshimiwa vizuri na Chama pamoja na maraisi 4( Marehemu Nyerere na Mkapa pamoja na Mwinyi na kikwete) alikuja kudhalilishwa vibaya sana Eti na magufuli mpaka mzee Eti akarekodiwa anaomba msamaha????😢

Hapana Aisee! Pombe Must Go. It’s now or Never

Lissu chukua nchi!!!
 
Aisee! Mkuu kwa kweli ni kama wajumbe walipoteza muda wao tu katika kura za maoni. Basi CC wangefanya wao tu kieleweke tu tangia mwanzo
Mjumbe hapo chini hilo vazi lake ni bora akaligeuze kua Pazia tu maana maoni yake wakuu wamegoma kuyaheshimu mkuu.
Screenshot_2020-07-26-08-09-00-1.jpg
 
Asante ndugu kwa hoja yako. Agenda yetu Watanzania sasa iwe ni utawala bora. Miundo mbinu tumepata, n.k. lakini kilichikosekana ni utawala wa sheria na kwa sababu tumempata mgombea mwanasheria wacha tumtwishe zigo ya kutengeneza katiba bora isiyochezewa chezewa.
 
Katiba mpya itapunguza madaraka ya uteuzi maana kila kukicha ni uteuzi usiokwisha,
 
Back
Top Bottom