Wasalaam, ccm chama dola chama tawala tokea uhuru kimefika hatamu kimechoka kinaongoza kwa nguvu za vyombo vya dola na kutumia nguvu kubwa dhidi ya RAIA wa Tanzania.
Kwanini nasema haya,;
1.ccm ndicho chama kilichotuingiza watanzania kwenye mikataba ya makaburi hasa ktk umeme na gesi. Pale kuna mikataba ya miaka hadi99 huku serikali ikipata 3% ktk 100%. Hii ni mikataba ya hovyo hata babu zetu wakati wakitawaliwa na mkoloni hawajawahi ingia na kusaini.
2.ccm ambao ni mabigwa wa ulaghai, walishirikiana wao na wezi kuchota pesa hazina ambazo ni kodi za wavuja katika ufisadi wa kutisha wa Richmond, epa, tegeta escrow, arv feki, barabara kujengwa chini ya viwango na kuharibika ndani ya muda mfupi.
3.ccm wameongoza kwa kuvunja katba walioipotisha wenyewe, kufanya siasa za kibaguzi kwa kuzuia vyama vingine vya siasa kufanya siasa, kuibuka mauji ya viongozi wa kisiasa wa upinzani, utekaji na kupotezwa kwa kila anaowakosoa na kuwapinga.
4.kuingilia vyombo vya habari, uhuru wa kuongea kwa mujibu wa ibara ya 18 ya katiba, kuzuia bunge live, mahakama kutokuwa huru, kuibuka kwa kundi LA wauaji na watesi dhidi ya RAIA ambao ccm wamewabatiza jina WATU WASIOJULIKANA ili hali tuna vyombo vya dola km tiss, jeshi imara, police, magereza na uhamiaji. Kweli km taifa tumeshindwa kuwajua watu wasiojulikana? Kwa kweli inasikitisha tumepoteza utaifa, kwani siku zote kubomoa ni rahisi kuliko kujenga. Nanukuu maneno ya marehemu HORACE KOLIMBA katibu wa ccm aliwahi kusema, nanukuu," CCM IMEPOTEZA DIRA. je alikurupuka au maneno yake yanaishi?