CCM si BABA wa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM si BABA wa CHADEMA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kigarama, May 11, 2009.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2009
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Jana katibu Mwenezi wa CCM ambaye pia ni waziri wa Habari na utamaduni George Mkuchika alitoa malalamiko yake juu ya "upotoshaji" habari ulionesha kwamba viongozi waandamizi wa CCM walizomewa kwenye kampeni zinazoendelea huko kwenye Jimbo la Busanda.

  Maudhui ya hoja za mkuchika niliyaelewa kwamba "bila CCM ,nchi itayumba" lakini kuna hili moja la kudai CCM ni baba wa CHADEMA nalikataa kwa nguvu zooote!

  CHADEMA haina baba anayetuhumiwa kwa Ufisadi huku akichekelea, baba anayetuhumiwa kwa kutumia vyombo vya dola kujijengea uhalali wa kutawala.

  CHADEMA haikuzaliwa na baba ambaye maslahi makubwa ni Chama na wala si nchi. Baba ambaye chaguzi zake za ndani ya chama na zile chaguzi zinazohusisha vyama vingine anategemea kugawa fulana,khanga au kkofia ili ashinde.

  Baba ambaye hana dira wala sera zinazoeleweka kwa wananchi wake. baba ambaye pamoja na kuwa na wabunge wengi kwenye bunge la Muungano na Baraza la wawakilishi hawezi kufanya maamuzi yanayofaidisha sehemu kubwa ya Watanzania.

  Kiuhalisia uhuwezi kusema kwamba CHADEMA na CCM ni "like son like Father"

  Huo ndiyo ukweli!!!!
   
 2. M

  Mwakaleli Member

  #2
  May 11, 2009
  Joined: Sep 23, 2008
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuchika ni naibu katibu mkuu wa chama. John Chiligati ndiye katibu mwenezi wa chama, naomba nikusahihishe katika hilo. baada ya hapo tuendelee na mjadala
   
 3. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2009
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Niliteleza,nakubaliana nawe!
  maudhui yanabaki kama yalivyo!!
   
Loading...