CCM sasa wameishiwa sera

GINHU

Member
Feb 7, 2011
68
14
Nimeshangazwa na kusikitishwa na kitendo cha Wassira na wafuasi wa CCM kuwapiga na kuwakamata vijana alio nyosha mikono na kuonyesha ishara ya CDM katika mkutano wa CCM.

Jamani naomba mnisaidie;
1. Hii mikutano ya kampeni inayofanywa inatakiwa ihudhuriwe na wafuasi wa vyama tu?
2. Km sivyo kunaubaya gani wa mtu kuwa mkweli kuwa ni mfuasi wa chama fulani na yuko pale kusikiliza sera zenu, na km mtamshawishi anaweza kubadilika?
3. Je kwenye mikutano hiyo kuna umhimu gani wa kuanza kuulizana nani wafuasi wa chama hiki na siyo?
4. km ni haki ya kila raia kupata habari km walivyofanya vijana wale, kwanini wafuasi wa CCM wawapige na kuwtoa mzobe mzobe na kuwapakia kwenye gari km waharifu?

hii jamani siyo haki, na kwa hili CCM wameishiwa sera. walichopaswa TYSON na wafuasi wengine wa CCM ni kuwapongeza wafuasi hao wa Chadema kwa kufika kusikiliza sera zao, hivyo walipaswa kuwashawishi kwa sera na si kuwa treat km walivyowafanya.

Nawasilisha wadau.
 
Ccm yenye iliisha mwaka 2000,Ccm ya sasa imebaki na ahadi,vitisho,wizi na umalaya.kama Mwigulu,angalia sera wanazotoa Igunga,"tukishindwa Igunga nakunywa sumu"ndio ahad zao hizo.
 
Ccm muda umewatupa mkono vile wao hawaamini kuwa hawatakiwi Tena
kuongoza nchi hii. Ccm ni Kama mzee ambae
amezeeka sana lakini anatamani kuwa kijana
Ccm wote wanaishi kwa matumaini
ndio maana hawana mtu maalum wa kuwasemea
kila mtu anaamka kivyake vyake. Wanaboa sana .
 
Hawajaishiwa sera, sera wanazo nyingine sana ila asilimia kubwa ni sera uchwara. Zimeandikwa tu kwenye vitabu lakini kwa vitendo hawezi kutekeleza.
 
Hawajui maana ya vyama vingi always magamba uwezo wao wa kufikiri umezeeka kama Tyson mwenye.
 
Hao chadema nao washari, kwanini walifata ccm kwenye kampeni zao?. Je ccm ikiingia kwenye mikutano ya chadema na sare za ccm itakuwa vipi?
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Kwa hili chanzo ni hao vijana wa cdm.
 
Lakini hawakutakiwa kuwateka na kuwapeleka kusikojulikana. Halafu halikuwa kosa kunyoosha alama ya vidole viwili kama wao ni washabiki wa CDM kama hawakufanya vurugu zozote.
 
Hao chadema nao washari, kwanini walifata ccm kwenye kampeni zao?. Je ccm ikiingia kwenye mikutano ya chadema na sare za ccm itakuwa vipi?
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Kwa hili chanzo ni hao vijana wa cdm.

waTZ tunahitaji viongozi wenye busara siyo hawa wanaotumia masaburi kwa kawaida hatuzuiani kwenye mikutano ya kampeini isipnkuwa kwenye usangoma au mitambiko, kama walikuwa wanatoa kafara au kutambika au kuwanga mchana waseme?Akili na Sura ya hilo zee vinafanana
 
Nafikiri hapo ndipo angemwaga sera za chama chake kuwashawishi hao Vijana, wamekata tama hao gamba
 
Adhabu ni moja tu kukinyima kura tar 2 oct, badala ya kuwashawishi wanawapiga! bila kujua ndio wanawapa sababu ya kutowaunga mkono. Shame on them
 
sababu ya vyama kuwa na ratiba tofauti za mikutano ya kampeni ni kuwapa fursa wananchi wa eneo husika kusikiliza sera za wagombea na au vyama tofauti tofauti bila kujali itikadi zao, ule haukuwa mkutano wa CCM, bali mkutano wa kampeni wa CCM, ambao kimsingi unawapa watu wote wa eneo husika kulinganisha sera za vyama tofauti na kisha kufanya maamuzi, walichokifanya hao magamba ni kuonesha umasikini wa fikra na si jingine, lakini pia kumbuka jamaa si ndo huwa anaitwa Tyson, yule bondia aliyeingia uwanjani bila gum protector ili amng'ate mwenzie
 
Hao chadema nao washari, kwanini walifata ccm kwenye kampeni zao?. Je ccm ikiingia kwenye mikutano ya chadema na sare za ccm itakuwa vipi?
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Kwa hili chanzo ni hao vijana wa cdm.

Hawakuwa na sare za chadema. Lakini kosa moja halihalalishi kosa la pili, CCM kama waliona hao vijana wameleata vurugu, tena ikiwa chama dola walipaswa wawakabidhi kwa wenye jukumu la kuhukumu (mahakama)
 
Back
Top Bottom