CCM sasa ina 'Lissuphobia'

CCM sasa ina 'Lissuphobia'

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Wakili Msomi Tundu Antipas Mughway Lissu sasa ni 'ugonjwa' kwa CCM yetu. Makada hutetema,hukosa raha na kunyong'onyea linapotajwa jina la Lissu. Ni katika mashauri mbalimbali yanayopelekwa Mahakamani yakiwahusisha makada wa CCM au CCM ikitajwa 'kuanzisha na kubariki' mashauri hayo.Yaweza kuwa ya jinai au madai. CCM yetu sasa ina 'Lissuphobia'.

Kwenye kesi ya ugaidi iliyomhusisha Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Winfred Muganyizi Lwakatare na kusemwa kuwa 'ilianzishwa' na CCM, mara baada ya kujitokeza kwa Tundu Lissu kama Wakili wa Utetezi, makada wa CCM walitimua mbio.Kila mmoja na njia yake. Wakapoteana. Mahakama kuu ikafutilia mbali mashtaka ya ugaidi dhidi ya Lwakatare. Lissuphobia.

Katika kesi kupinga ushindi wake wa uchaguzi wa 2010 katika Mahakama ya Rufani ya Tanzania iliyoketi Dodoma, Lissu alijiwakilisha mwenyewe. Si kama Wakili.Ni kama Mjibu Rufani. Makada wa chama chetu cha CCM walisambaratika na kupotelea kusikojulikana. Wakamuacha Wakili wao solemba.Lissu akashinda. Lissuphobia.

Ni jana tu, ilitolewa taarifa kuwa Wakili Msomi Lissu ataongoza timu ya Mawakili wa Utetezi katika kesi ya 'kutukana' iliyokuwa ikimkabili Mbunge wa Arusha Mjini Ndugu Godbless Lema. Kimsingi,kesi hii imeanzishwa na kada wa CCM na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Ndugu Magesa Mulongo.Kusikia uwepo wa Lissu,makada wote wa CCM wakiongozwa na CCM waliachana njia.Wakaweka mpira kwapani na kukimbia Mahakama na kesi husika. Lema akafutiwa mashtaka yake leo Arusha. Lissuphobia.

Mifano hii, pamoja na kesi ya rufaa ya Ubunge wa Lema iliyosikilizwa Mahakama ya Rufani ya Tanzania iliyoketi Dar es Salaam,itoshe kuonesha jinsi Wakili Msomi Tundu A.M. Lissu anavyoogofya. CHADEMA sasa wana silaha imara.Ni dhidi ya unaoonwa kama ukandamizwaji wa demokrasia nchini na uonevu wa kisiasa kupitia Mahakama. Katabia kanakojengeka na kushamiri.Wana Lissu.CCM tuna nani? Dawa ya Lissuphobia ni nini?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Mkuu Nyie Ma CCM ni kama kenge, hasikii kabisaaa hata upige vp, Mpaka Damu inapoanza kutoka Masikioni ndo Kenge huwaga anastuka kuwa eeh, Kumbe Kifo hiki Hapa!!!!!
 
Halafu Mkuu, Lissu kama Wakili wa Kujitemea,ukiacha kuwa ni Mbunge wa CHADEMA, CCM bado mna Fursa ya Kumtumia kwenye Kesi zenu Kama Murji wa Mtwara alivyomtumia Peter Kibatala, nanyi Mtumieni Lissu basi kama wakili wenu
Hebu jaribuni option hii basi, Mzee, Peleka huu ushauri Lumumba
 
dawa ya "Phobia" yoyote ni UKWELI. CCM wafike mahala wakubali kwamba sasa wamepotea njia. warudi kuwa CHAMA CHA MAPINDUZI ki ukweli. warudi kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi. watetee na kusimamia maslahi ya umma wa watanzania. hapo wala hawatakuwa na haja ya kuogopa mtu. phobia zote wataachana nazo
 
....

.....magamba yote ni "hewa" kuanzaia magogoni mpaka nyumba kumikumi....
 
VUTA-NKUVUTE umesahau kesi ya Sugu kumtukana waziri Mkuu.... Vile vile ile ya Sugu kumpiga ngumi Askari iliyoshindikana kupelekwa mahakamani, Zote ni chini ya Kamanda Lissu.... Hongera Sana Tundu Antipas Mugway Lissu,MUNGU akupe maisha marefu.....
 
Nyie mna
Polisi, Nape , Nkamia, Lusinde, Mwanasheria Mkuu , Kinana , Mnadhimu wa CCM nani huyu wa hapa Iringa anaitwa nani sijui , mna Wassira .Mkuu mnao wengi .

Katika list yako taja pia Mnadhimu wa CCM kakimbia juzi pale Mlimani City .
 
VUTA-NKUVUTE umesahau kesi ya Sugu kumtukana waziri Mkuu.... Vile vile ile ya Sugu kumpiga ngumi Askari iliyoshindikana kupelekwa mahakamani, Zote ni chini ya Kamanda Lissu.... Hongera Sana Tundu Antipas Mugway Lissu,MUNGU akupe maisha marefu.....
Si hayo tu bali pia LUKUVI kukimbia mdahalo kati yake na LISSU
 
mawakili wengi wa ccm hawana uwezo na wala hawahangaiki sana , wanafuata hiyo mihela isiyo na odita , hakuna mwenye uwezo wa kupambana na lissu !
 
Antiphas Mughway Tundu Lissu ni NOUMER..ccm wamewazalisha kina LISSU kadhaa.Nyaronyo KICHEERE,Method Kimomogoro na Peter KIBATALA.
 
Mie nasema,Lissu akifichwa sehemu tulivu kwa miezi mi tatu.
Atatoka na Katiba moja Nzuri ambayo hatujawahi kuwa nayo.
 
dawa ya "Phobia" yoyote ni UKWELI. CCM wafike mahala wakubali kwamba sasa wamepotea njia. warudi kuwa CHAMA CHA MAPINDUZI ki ukweli. warudi kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi. watetee na kusimamia maslahi ya umma wa watanzania. hapo wala hawatakuwa na haja ya kuogopa mtu. phobia zote wataachana nazo

Mkuu umenena dawa ya PHOBIA ni Repeated exposure to the same situation producing phobia labda watazoea
 
This is gud idea for real,tatizo linalowakabiri maCCM ni uvivu wa kusoma vitabu na kujiongeza,mwanaCCM hubaki na alichomezeshwa darasani,mfano ni yule mburula wao MWIGULU,but ni tofauti na mwanaharakati mwingine yeyote kama LISSU,MNYIKA,Rev MSIGWA, KIBATARA PETER au ZITTO,so mtu kama LISSU lazima awasumbue......na bado!
 
VUTA-NKUVUTE, nadhan sasa unatafuta kama yaliyompata the late Kolimba. Hujui kwamba unaposema ukweli unadhoofisha chama
 
Last edited by a moderator:
Magamba wamefanya vyama vya siasa vionekane ni uadui, uhasama, usimba na yanga: isingekuwa chuki za kina mwigulu zidi ya watu wanaoipenda chadema,bsi leo AG angekuwa tundu lissu,maana kikwete anatambua mchango wa lissu na hapo serikali ingenyoka na wananchi wangetii sheria bila shurti.

Ona kenya leo odinga na kenyatta wanashirikiana kujenga nchi yao ila sisi huku upinzani ni uadui tena wakuana kabisa, mpk leo bado nalia na kuhudhunika kwa ile damu iliyomwagika soweto kisa viti vinne vya udiwani?
 
Back
Top Bottom