M-24 Tanzania
Member
- Sep 13, 2013
- 39
- 2
Kwa Lissu,NO COMENT
Wakili Msomi Tundu Antipas Mughway Lissu sasa ni 'ugon] huwo mnazi ulikunywa haukufai
Tuna watoa kucha na macho!! Soon tutamu-ulimboka Lissu!! subiri uone!!Wakili Msomi Tundu Antipas Mughway Lissu sasa ni 'ugonjwa' kwa CCM yetu. Makada hutetema,hukosa raha na kunyong'onyea linapotajwa jina la Lissu. Ni katika mashauri mbalimbali yanayopelekwa Mahakamani yakiwahusisha makada wa CCM au CCM ikitajwa 'kuanzisha na kubariki' mashauri hayo.Yaweza kuwa ya jinai au madai. CCM yetu sasa ina 'Lissuphobia'.
Kwenye kesi ya ugaidi iliyomhusisha Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Winfred Muganyizi Lwakatare na kusemwa kuwa 'ilianzishwa' na CCM, mara baada ya kujitokeza kwa Tundu Lissu kama Wakili wa Utetezi, makada wa CCM walitimua mbio.Kila mmoja na njia yake. Wakapoteana. Mahakama kuu ikafutilia mbali mashtaka ya ugaidi dhidi ya Lwakatare. Lissuphobia.
Katika kesi kupinga ushindi wake wa uchaguzi wa 2010 katika Mahakama ya Rufani ya Tanzania iliyoketi Dodoma, Lissu alijiwakilisha mwenyewe. Si kama Wakili.Ni kama Mjibu Rufani. Makada wa chama chetu cha CCM walisambaratika na kupotelea kusikojulikana. Wakamuacha Wakili wao solemba.Lissu akashinda. Lissuphobia.
Ni jana tu, ilitolewa taarifa kuwa Wakili Msomi Lissu ataongoza timu ya Mawakili wa Utetezi katika kesi ya 'kutukana' iliyokuwa ikimkabili Mbunge wa Arusha Mjini Ndugu Godbless Lema. Kimsingi,kesi hii imeanzishwa na kada wa CCM na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Ndugu Magesa Mulongo.Kusikia uwepo wa Lissu,makada wote wa CCM wakiongozwa na CCM waliachana njia.Wakaweka mpira kwapani na kukimbia Mahakama na kesi husika. Lema akafutiwa mashtaka yake leo Arusha. Lissuphobia.
Mifano hii, pamoja na kesi ya rufaa ya Ubunge wa Lema iliyosikilizwa Mahakama ya Rufani ya Tanzania iliyoketi Dar es Salaam,itoshe kuonesha jinsi Wakili Msomi Tundu A.M. Lissu anavyoogofya. CHADEMA sasa wana silaha imara.Ni dhidi ya unaoonwa kama ukandamizwaji wa demokrasia nchini na uonevu wa kisiasa kupitia Mahakama. Katabia kanakojengeka na kushamiri.Wana Lissu.CCM tuna nani? Dawa ya Lissuphobia ni nini?
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Halafu Mkuu, Lissu kama Wakili wa Kujitemea,ukiacha kuwa ni Mbunge wa CHADEMA, CCM bado mna Fursa ya Kumtumia kwenye Kesi zenu Kama Murji wa Mtwara alivyomtumia Peter Kibatala, nanyi Mtumieni Lissu basi kama wakili wenu
Hebu jaribuni option hii basi, Mzee, Peleka huu ushauri Lumumba
Mie nasema,Lissu akifichwa sehemu tulivu kwa miezi mi tatu.
Atatoka na Katiba moja Nzuri ambayo hatujawahi kuwa nayo.
"ni heri Dr.slaa aingie ikulu kuliko Tundu Lissu kuingia bungeni" - by Jakaya Khalifan Mrisho Kikwete
Mkuu nakubaliana na wewe kabisa, Ila tatizo la Mkuu wa Kaya anawasikiliza sana maccm wakati anajua Lisu ni kifaa kuliko mwanasheria mkuu wa Sereka;li ila amemweka benchi kisa usisiemu.lissu pekee ni, serikali nzima ya jk na jk akiwemo ndani+ wabunge wa sisiemu.
Hakuna anayeweza kusimama na lissu mbele ya mahakama toka sisiemu.
Mchambuzi swali sio CCM ni ya nani, Ila CCM ina nani wakupambana na LISSU MAHAKAMANI, BUNGENI, MDAHALO nk.Ina maana upo ndani lakini Haujui kwamba ccm ina wenyewe?
Dawa yake ni utawala wa haki na sheria;
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums