CCM sasa chasimika mabalozi bila kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM sasa chasimika mabalozi bila kura

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Apr 8, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Christopher Maregesi, Bunda
  MWENENDO wa uchaguzi wa viongozi ngazi za shina unaoendelea ndani ya CCM wilayani hapa, unadaiwa kuingia dosari baada ya baadhi ya wanachama wa chama hicho kususia kugombea kwa madai kuwa, chama hicho hivi sasa hakina mvuto kwa umma.Kufuatia hali hiyo, taarifa zinasema uongozi wa CCM ngazi za kata na wilaya, umekuwa ukihaha kubembeleza kisha kuwasimika wanachama wake wakongwe, ili kunusuru aibu ya kukoswa uwakilishi ngazi ya shina.

  Chanzo cha habari kilieleza kuwa, baadhi ya wanachama wanaojiita wenye msimamo mkali, hawaoni sababu ya kukitumikia kwa wadhifa wowote ule kwani, kimekosa mvuto kwa jamii wanaona bora kubaki wanachama wa kawaida.
  “Chama chetu kwa sasa hakina mvuto wala mshiko kwa jamii. Sasa hilo wengi hasa wenye msimamo mkali hawataki kabisa kuongoza, badala yake wanaona heri wabakie walalahoi ndani ya chama,” kilieleza chanzo hicho.
  Kwa mujibu wa chanzo hicho ambacho ni miongoni mwa watu waliosimikwa kwa nguvu kuwa mabalozi, baadhi ya sababu zinazowakera wanachama hao ni ukimya kilionao kuhusu tuhuma mbalimbali zinazotolewa dhidi ya mafisadi.
  Chanzo hicho kilisema hali ya chama kukaa kimya bila kuwachukulia hatua wanaotuhumiwa kwa ufisadi, vinawatia kinyaa baadhi ya wanachama.

  Kwa upande wake, Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Bunda, Daudi Iramba, licha ya kudai kutojua kwa undani kuhusu mwenendo wa uchaguzi, alikana kuwapo kwa wanachama wanaogoma kugombea nafasi za ubalozi.
  “Sina taarifa rasmi maana sihusiki na uchaguzi, mhusika ni katibu maana ndiye mkurugenzi wa uchaguzi. Lakini kwa ujumla hatuna taarifa za watu kususia nafasi hizo,” alisema Iramba na kuongeza:
  “Hili la chama, bado kiko imara kikiwa na mvuto tele kwa jamii kinaowatumikia kwa uadilifu mkubwa."


  chanzo:-GAZETI MWANANCHI
   
Loading...