CCM pawaka moto Dodoma

MKUTANO wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), umeanza mjini hapa ukiwa umefunikwa na usiri mkubwa kutokana na mambo mazito yanayojadiliwa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.

Tofauti na mikutano iliyopita, safari hii hali inaonekana kuwa tete huku wajumbe wa wakionekana kutopenda kuzungumza lolote kwa wazi kuhusiana na mjadala wa ajenda za mkutano huo.

Katika hali ambayo inadhihirisha kuwa mambo si shwari katika mwenendo mzima wa mkutano huo jana habari kutoka ndani ya kikao na ambazo hata hivyo, hazikuthibitisha mvutano wa Mbunge wa Igunga Rostam Aziz na Spika wa Bunge Samuel Sitta lilitikisa huku baadhi ya wajumbe wakiwataka wafanye suluhu ili kusudi mvutano wao unaokitikisa chama uishe.

Mnamo saa 12:15 hivi jioni Spika Sitta, Mbunge wa Kyela Dk Harrison Mwakyembe na Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela walitoka ndani ya chumba cha mikutano na kukaa kwenye chumba kimoja kwa pamoja wakijadili jambo linaloonekana kuwa ni zito kwa muda wa takribani saa nzima.

Baada ya kuketi pamoja kwa muda huo, baadaye waliamua kuingia ndani ya kikao, haikufahamika kama waliitwa au la, lakini alianza kuingia Dk Mwakyembe akifuatiwa na mama Kilango na baadaye Spika Sitta.

Saa moja usiku umeme ulikatika kwa dakika kama kumi hivi, lakini hakuna hata mjumbe aliyetoka ndani kwenda nje badala yake walibaki chumba cha mkutano na taa zikaingizwa huku walinzi wakiwasukumizia mbali baadhi ya watu waliokuwa na hamu ya kusikiliza nini kilijiri.

Awali, Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete aliingia ukumbini katika jengo la White House saa 8:55 mchana. Punde alipoingia ukumbini alifungua mkutano baada ya kupewa taarifa kuwa idadi ya wajumbe ilikuwa imekamilika.

Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba, alimwambia Rais Kikwete kwamba, idadi kamili ya wajumbe ilikuwa 211, lakini waliohudhuria katika kikao hicho walikuwa wajumbe 205 sawa na asilimia 97 ya wajumbe wote.

"Mheshimiwa mwenyekiti idadi kamili ya wajumbe katika kikao hiki ni 211, lakini waliohudhuria hadi sasa ni wajumbe 205 hivyo mkutano huu ni halali naomba kukukaribisha ili ufungue," alisema Makamba.

Baada ya kusomewa idadi hiyo, tofauti na siku zote Kikwete alitamka neno moja akisema: "Nimefungua" huku akiwa amekaa, kabla ya kuwaomba wajumbe wasimame kwa dakika moja kwa ajili ya kumkumbuka Rashidi Kawawa (Simba wa Vita).

Mkutano huo ulio chini ya Mwenyekiti wa CCM Kikwete na kuhudhuriwa na wenyeviti wote waliomtangulia, Benjamin Mkapa na Ali Hassan Mwinyi unajadili ajenda kuu tatu ambazo ni kupokea na kujadili taarifa ya hali ya kisiasa nchini, taarifa ya Kamati ya Mzee Mwinyi na Uchaguzi wa kuziba nafasi mbili za wajumbe wa Nec.

Mkutano wa Nec ambao ni wa siku mbili (kuanzia jana na leo), ulitanguliwa na kikao cha siku moja cha Kamati Kuu (CC) kilichofanyika juzi, ambacho pia kilitanguliwa na Kamati ya Maadili.

Wadadisi wa mambo ya kisiasa ndani ya CCM, wanaona kuwa Nec ndiyo itatoa taswira na mwelekeo wa chama katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu; hasa baada ya kujadili kwa kina taarifa ya kamati ya mzee Mwinyi.

Miongoni mwa mambo ambayo yanatarajiwa kuibuka katika ripoti ya Mwinyi ni jinsi ya kuwashughulikia wanachama wao waliochafuka kwa tuhuma za ufisadi ambao wamekuwa wakionekana kukichafua chama hicho.

Baadhi ya wadadisi wa mambo wanaona mtu kama Andrew Chenge, ambaye amekuwa akituhumiwa kuhusika katika kashfa ya rada angepaswa kuvuliwa nafasi yake ya uenyekiti wa Kamati ya Maadili ya CCM.

Chenge, amekuwa akipata upinzani kutoka kwa kundi linaloitwa la wapiganaji, ambalo linaona kuwa tuhuma zinazomkabili zinamfanya akose sifa ya kuongoza chombo hicho.

Wengine ambao wako katika mvutano huo ingawa walivuliwa nyadhifa zao ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Nazir Karamagi na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ambao wanatuhumiwa katika kashfa ya mkataba tata kati ya Kampuni ya Richmond Development (LLC) na Tanesco, uliosainiwa Juni 23, 2006.

Kuzimwa ghafla kwa sakata hilo bungeni, kunaangaliwa na wadadisi wa mambo kama hatua ya kuachia chama kiamue hatima ya waliotajwa katika mkataba wa Richmond, ikiwezekana kuwavua nyadhifa au kuwaonya na kuhakikisha chama kinakuwa na umoja.

Hata hivyo, baadhi ya wadadisi wa masuala ya kisiasa wanaangalia upande wa pili wa shilingi na kuamini kwamba, huenda NEC ikakosa nguvu zaidi ya ilivyotarajiwa kutokana na kutanguliwa kwa vikao vyenye nguvu ambavyo vimepunguza makali ya wajumbe.

Kwa kawadia Nec, hupokea ajenda ambazo zinakuwa tayari zimeshapitishwa na CC na kutoa mapendekezo yao pamoja na kuwa na nguvu.

Lakini, habari za uhakika zilizolifikia Mwananchi, zilifafanua kwamba Kamati ya mzee Mwinyi ingetoa taarifa ambayo tayari inadaiwa kuchambuliwa pamoja na misimamo ya baadhi ya wajumbe kulegeza kutokana na maazimio yaliyofikiwa na Bunge katika kulimaliza sakata la Richmond.

Kwa upande wa taarifa ya hali ya kisiasa huenda ikaibuliwa hoja ya kujadili juu ya Chama Cha Jamii (CCJ), pamoja na misimamo ya CCM kuhusu ujio wa chama hicho ambacho hadi sasa kimezusha sintofahamu miongoni mwa wana- CCM na Watanzania kwa ujumla.

Hadi sasa hakuna taarifa rasmi kuhusu nani hasa wahusika wakuu wa CCJ kutokana na kuwepo taarifa tata zinazohusisha watu mbalimbali ndani ya CCM na mfumo unaongoza nchi.

Baadhi ya taarifa zimekuwa zikihusisha CCJ na kambi ya wapambanaji wa ufisadi ambao wanadaiwa kuwa wanajiandaa kujitoa kama watuhumiwa wa ufisadi hawatashughulikiwa ndani ya CCM na kuvuliwa nyadhifa zao.

Lakini, upande wa pili CCJ inadaiwa kuandaliwa na mafisadi kwa lengo la kuwafanya wapambanaji hao kuonekana wamesaliti chama chao (CCM).

Hata hivyo, Spika Sitta amekwisha weka bayana kwamba, hawezi kuzuia watu kusema kuhusu yeye kuhusika na chama hicho na kuhoji kwamba, kuna ubaya gani chama hicho kusajiliwa.

Suala la makubaliano ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani), Amani Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad, kuhusu mustakabali wa kisiasa visiwani humo pia limekuwa likitarajiwa kujadiliwa kwa kina ili lisikinzane na katiba na mwongozo wa CCM.

Hivi sasa Wazanzibar wanatarajia kuundwa kwa Serikali ya Mseto baada ya Seif na Karume kuafikiana kuleta amani visiwani humo na tayari suala hilo limefikishwa kwenye Baraza la Wawakilishi.

Kuhusu uchaguzi, moja ya nafasi zinazozibwa ni pamoja na nafasi ya Sophia Simba ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa chama hicho (UWT), ambapo alikata tiketi ya kuwa mjumbe moja kwa moja.
 
FMEs,
Nakubaliana na wewe kabisaaa. Na sio urafiki tu, bali pia ni msiri wake mkuu wa jinsi JK aliyoweza kuingia madarakani (obvious kwa kutumia milungula). Naamini kabisa kuwa walikuwa wamejipanga kuwa JK akimaliza 10 yake, EL angemrithi.

Mkuu Kubwajinga, si ajabu 2015 bado Lowassa akawa mstari wa mbele kumrithi Kikwete kuliko mwingine yeyote yule ndani ya CCM. Si umeona jinsi Kikwete alivyopigwa vita kwamba hafai kupewa tena awamu ya pili kutokana na utendaji wake mbovu, lakini ndiye huyoo anarudi tena Ikulu 2010.
 
hakuna lolote..........wanajenga tu umoja wao wa kihuni, nakuhakikishia hakuna malumbano.
Ngoja Chiligati atoke ndo utaugundua unafiki wa wa16

amini hivyo lakini huo ndio ukweli hatukulazimishi kuamini,

not every thing you see is as it is! kwa taarifa yako mawimbi ya sauti toka humu ndani yanasafiri had amerika.

umchunguza sole za viatu vyetu tulioko huku ndani.
umechunguza miwani ya baadh ya waheshimiwa? we vipi

kama chiligati akitoka na kauli yake ni yeye, mangapi mmedanganywa na chiligati, hii nayokupa hapa ni laivu toka huku.
 
Tuwekee majina ya wanaochangia basi kama wewe hautudanganyi kama Chiligati
 
inaonekana wajumbe wamechoka maana minon'gono imekuwa mingi zaid, ukiwa huku ndani ndo utajua kuwa kuna ccm mbili. Makundi yanajionyesha.

m/kit amepunguza dk za kuchangia maana mda unaelekea ukingon
 
Mtoa hoja anasema yuko jikoni na anapakua mambo, mimi nilitegemea tungemsikiliza kwanza baada ya kuanza kubishana humu sasa hata mtiririko umepotea na ni vigumu kujua kama jamaa anadaganya au vipi. jamani! "yaani mmeshindwa kukesha nami hata saa moja"
 
mie nchi yangu nimeshamuachia mwenyezi.....,ukosefu wa elimu mkubwa miongoni mwa wapiga kura ni chanzo kikubwa cha upindishwaji wa demokrasia.CCM wanalijua hilo ndio maana wanajitahiti kwa nguvu zote kutengeneza TZ ya ma-bogus,SHULE za kata ni mfano mmojawapo.kama mwaka huu wametengeneza zero+div 4 65,000 in 10 years tutakuwa na hizi sampuli kama nilioni moja hivi.idadi nzuri tu ya wapiga kura kumuweka mh madarakani..,maaa hawa ma-zero milioni moja ukiwaambia nitawapa ajira milioni 2 tu!makofi meengi.ukiwaambia maisha bora kwao in 5 years wanatoa kura upesi sana,bila kuhoji.na kwa nini wahoji jamani?indoctrination waliyofanyiwa kwenye shule za kata ni kuwawezesha waweze kuhesabu fedha na kutofautisha A na B.basi,sio kuchambua chochote.

Naisubiri tanzania Kikwete,Mwinyi,Malecela,Mkapa,Karume,Lowasa na makundi yao ya kifedhuli watakapokuwa MAREHEMU.siwatakii mabaya huko waendako ila natamani waondoke mapema,wakapumzike.naamini watoto wao awatapewa nafasi ya kuwafanya watoto zetu mabwege,kama sio hivyo hata kama wajukuu zetu sawa tu.

KWA sasa hivi nawahurumia watanzania wenzetu tuliozaliwa katika "wrong period of time."kwanza tulikuwa wajamaa,tukapigika na umasikini wa kujitakia,ili fikra za mwenyekiti zidumu,tukaja enzi za ulanguzi,wahindi wakatufanya machangudoa wao,wakatupora kila aina ya kizuri Mwenyekiti alichosaza wakati wa ufalme wake,"wajanja" waswahili wachache wakaliona hilo,the bread is being finished by the few Indians.wakaona isiwe shida,ngoja tugawane/tule nao hawa ma*********,wakauza weee kila wanachokiona,wakaona vingine haviuziki akaamua kuizunguka DUNIA kuvinadi.walivomaliza/kupigwa stop na economic crisis-mungu ashukuriwe kwa hili.wamerudi TZ kupikiana majungu ya kiila aina,wakigombana kuliko wanamipasho kina kopa.

I am kind of tired being optimistic,i have waited for so many decades to see someone do something right,i have waited long enough to realize some countries are doomed,and we sure are.

I am only glad to say our children and grand children will share a better future.one in which no kingunge or some shit has anything to do with it
 
Nakubaliana nawe kabisa. Hawa CCM ni wasanii tu si ajabu Lowassa akawemo katika awamu ya pili ya Kikwete. Hawana lolote bali kutuzuga tu Watanzania.

Bubu MKuu, mimi ninauhakika kabisa kuwa kama Mungu hatupendi na Jakaya akaweza kuwa rais wa miaka mingine mitano; EL atakuwemo kwenye cabinet yake na atampa wizara nyeti ya Tawala za mikoa!!: Tuombe Mungu atupe uhai na JF iwepo tutakujakumbushana.
 
inaonekana wajumbe wamechoka maana minon'gono imekuwa mingi zaid, ukiwa huku ndani ndo utajua kuwa kuna ccm mbili. Makundi yanajionyesha.

m/kit amepunguza dk za kuchangia maana mda unaelekea ukingon

Wewe 16 acha kuseveza watu hapa jamvini kama uko mjengoni mwaga data hapa acha porojo.Tueleze nani kasema nini na response imekuwa vipi.Mara ya mwisho ulitueleza mzee 6 alikuwa anakunywa maji sana na ametoka nje ya mkutano.

Je amerudi na kilichomfanya anywe maji kwa wingi ni nini wakati yeye ni mjumbe tu kama wajumbe wengine au mwelekeo ni kwamba mafisadi wanapata ushindi ndani ya kikao kwa hoja nzito nzito.Toa data kama uko mjengoni.
 
FMEs,
Nakubaliana na wewe kabisaaa. Na sio urafiki tu, bali pia ni msiri wake mkuu wa jinsi JK aliyoweza kuingia madarakani (obvious kwa kutumia milungula). Naamini kabisa kuwa walikuwa wamejipanga kuwa JK akimaliza 10 yake, EL angemrithi.

- Mkuu watu wenye akili nyingi sana duniani wanapokwama hurudi kwenye msingi wa walipotokea, binafsi ninakumbuka Lowassa na Rais wa sasa wakiitwa Boyz To Man, wakakodiwa ndege maalum ya kuwapeleka Dodoma dakika za mwisho wa kikao cha NEC ili wawe alternative ya kugombea urais, wananchi wa taifa hili we never questioned nani amelipia ile ndege, na WHY? Lowassa na Rais wa sasa nani aliwaita dakika za mwisho kwenda Dodoma kwa sababu no question kwamba hawakuitwa na Mwalimu!

- Lowassa alikuwa njiani kugombea urais ninachojua ni kwamba he was a serious candidate kuliko Rais wa sasa, sasa ilikuwaje akaamua kukaa pembeni na kumuachia Muungwana? Kuna dataz moja niliwahi kuzipata then, one time Lowassa alikuwa mahali akizungumza na mtu kwa siri sana, aliulizwa vipi Urais, akamjibu yule mtu tena with confdence sana kwamba "..ninaweza kuwa rais nikitaka maana this is my chance, lakini siwezi kuharibu utamaduni ambao inayokuja ni zamu ya Muisilamu kuwa Rais..." akaendelea "..mimi na Jakaya ni kitu kimoja, tumeongea na nimemfahamisha hilo kwamba ninamuachia kwa sasa.." haya yote niliyasema zamani

- Kwamba Lowassa atapata matatizo ya kisheria under Muungwana's watch haitakuja kutokea, kwamba atakuwa Rais in our watch ninasema haitakuja kutokea unless CCM ivunjike, yanayotukuta sasa ni matatizo tuliyoyataka wenyewe wananchi na hasa hawa waandishi wetu wa habari, we were so happy na political deals za short terms bila kujua nini hasara zake in the long terms na ndio what we are paying for now, Lowassa is fine for now, ingawa matatizo yake kisheria yapo pale pale ndio maana Rostam anayejua better analilia sana majaji kuamua kuhusu Richmond.

- Wananchi tunahitaji kua macho sana, ninaamini sana kwamba huyu Lowassa anajua kwamba yeye alivyo hawezi kugombea urais, isipokuwa kwa sababu he is so determined kua Rais, ataishia siku moja kutupiga changa zito sana la macho, ninaamini and I could be wrong pia, kwamba ata-push to end kugombea urais 2010 akijua sana kwamba hawezi kupata nafasi, in the process ataisukuma na kui-pressure our political system nzima to the wall that kutakua na a political deal ya kumrudisha kwenye power under some capacity, itakapofika 2015 Lowassa atamuweka mtu wake kuchukua urais halafu yule mtu hatamaliza kwa sababu atakazopewa na Lowassa yaani atajiuzulu, hapo ndipo huyu Lowassa ataliliwa na chama kizima achukue Urais ndio the only chance aliyonayo na ninaamini ndiyo njia atakayotumia kushika urais kama ndoto yake inavyomtuma.

Respect.

FMEs!
 
Mkuu Kubwajinga, si ajabu 2015 bado Lowassa akawa mstari wa mbele kumrithi Kikwete kuliko mwingine yeyote yule ndani ya CCM. Si umeona jinsi Kikwete alivyopigwa vita kwamba hafai kupewa tena awamu ya pili kutokana na utendaji wake mbovu, lakini ndiye huyoo anarudi tena Ikulu 2010.

Hilo mbona liko wazi kabisa, Lowassa ndio atakaye achiwa kiti mwaka 2015. Ndio maana unaona amekaa kimya hapigi kelele zozote zile ameshajua kuwa kiti ni cha kwake 2015.

Mungu Ibariki Tanzania, wabariki na watu wake...
 
- Mkuu watu wenye akili nyingi sana duniani wanapokwama hurudi kwenye msingi wa walipotokea, binafsi ninakumbuka Lowassa na Rais wa sasa wakiitwa Boyz To Man, wakakodiwa ndege maalum ya kuwapeleka Dodoma dakika za mwisho wa kikao cha NEC ili wawe alternative ya kugombea urais, wananchi wa taifa hili we never questioned nani amelipia ile ndege, na WHY? Lowassa na Rais wa sasa nani aliwaita dakika za mwisho kwenda Dodoma kwa sababu no question kwamba hawakuitwa na Mwalimu!

- Lowassa alikuwa njiani kugombea urais ninachojua ni kwamba he was a serious candidate kuliko Rais wa sasa, sasa ilikuwaje akaamua kukaa pembeni na kumuachia Muungwana? Kuna dataz moja niliwahi kuzipata then, one time Lowassa alikuwa mahali akizungumza na mtu kwa siri sana, aliulizwa vipi Urais, akamjibu yule mtu tena with confdence sana kwamba "..ninaweza kuwa rais nikitaka maana this is my chance, lakini siwezi kuharibu utamaduni ambao inayokuja ni zamu ya Muisilamu kuwa Rais..." akaendelea "..mimi na Jakaya ni kitu kimoja, tumeongea na nimemfahamisha hilo kwamba ninamuachia kwa sasa.." haya yote niliyasema kule BCS,

- Kwamba Lowassa atapata matatizo ya kisheria under Muungwana's watch haitakuja kutokea, kwamba atakuwa Rais in our watch ninasema haitakuja kutokea unless CCM ivunjike, yanayotukuta sasa ni matatizo tuliyoyataka wenyewe wananchi na hasa hawa waandishi wetu wa habari, we were so happy na political deals za short terms bila kujua nini hasara zake in the long terms na ndio what we are paying for now, Lowassa is fine for now, ingawa matatizo yake kisheria yapo pale pale ndio maana Rostam anayejua better analilia sana majaji kuamua kuhusu Richmond.

- Wananchi tunahitaji kua macho sana, ninaamini sana kwamba huyu Lowassa anajua kwamba yeye alivyo hawezi kugombea urais, isipokuwa kwa sababu he is so determined kua Rais, ataishia siku moja kutupiga changa zito sana la macho, ninaamini and I could be wrong pia, kwamba ata-push to end kugombea urais 2010 akijua sana kwamba hawezi kupata nafasi, in the process ataisukuma na kui-pressure our political system nzima to the wall that kutakua na a political deal ya kumrudisha kwenye power under some capacity, itakapofika 2015 Lowassa atamuweka mtu wake kuchukua urais halafu yule mtu hatamaliza kwa sababu atakazopewa na Lowassa yaani atajiuzulu, hapo ndipo huyu Lowassa ataliliwa na chama kizima achukue Urais ndio the only chance aliyonayo na ninaamini ndiyo njia atakayotumia kushika urais kama ndoto yake inavyomtuma.

Respect.

FMEs!

That's a very scary movie bro!
 
- Waku samahani sana leo nina msiba mzito sana katika familia nimefiwa na shangazi ndio maana toka jana niko buzzy na simu za kuwasiliana na ndugu kuhusu mazish na msiba, lakini otherwise nitakapopata upenyo kidogo nitashika post za dataz huko ndani ya kikao on kinachojiri, as soon as possible,

- Dataz siku zote ni my commitment kwa wana-JF regardless of what. Tuvute subira kidogo!

Pole kwa msiba wa Shangazi.
When it comes to CC na NEC, you an authority of its kind hapa JF, tunakusubiria kwa hamu, wakati tukiendelea kula kila kinachopakuliwa huko ndani, uamuzi wa kumeza au kutema, utategemea kimepikwa na kuiva kiasi gani.
 
- Mkuu watu wenye akili nyingi sana duniani wanapokwama hurudi kwenye msingi wa walipotokea, binafsi ninakumbuka Lowassa na Rais wa sasa wakiitwa Boyz To Man, wakakodiwa ndege maalum ya kuwapeleka Dodoma dakika za mwisho wa kikao cha NEC ili wawe alternative ya kugombea urais, wananchi wa taifa hili we never questioned nani amelipia ile ndege, na WHY? Lowassa na Rais wa sasa nani aliwaita dakika za mwisho kwenda Dodoma kwa sababu no question kwamba hawakuitwa na Mwalimu!

- Lowassa alikuwa njiani kugombea urais ninachojua ni kwamba he was a serious candidate kuliko Rais wa sasa, sasa ilikuwaje akaamua kukaa pembeni na kumuachia Muungwana? Kuna dataz moja niliwahi kuzipata then, one time Lowassa alikuwa mahali akizungumza na mtu kwa siri sana, aliulizwa vipi Urais, akamjibu yule mtu tena with confdence sana kwamba "..ninaweza kuwa rais nikitaka maana this is my chance, lakini siwezi kuharibu utamaduni ambao inayokuja ni zamu ya Muisilamu kuwa Rais..." akaendelea "..mimi na Jakaya ni kitu kimoja, tumeongea na nimemfahamisha hilo kwamba ninamuachia kwa sasa.." haya yote niliyasema zamani

- Kwamba Lowassa atapata matatizo ya kisheria under Muungwana's watch haitakuja kutokea, kwamba atakuwa Rais in our watch ninasema haitakuja kutokea unless CCM ivunjike, yanayotukuta sasa ni matatizo tuliyoyataka wenyewe wananchi na hasa hawa waandishi wetu wa habari, we were so happy na political deals za short terms bila kujua nini hasara zake in the long terms na ndio what we are paying for now, Lowassa is fine for now, ingawa matatizo yake kisheria yapo pale pale ndio maana Rostam anayejua better analilia sana majaji kuamua kuhusu Richmond.

- Wananchi tunahitaji kua macho sana, ninaamini sana kwamba huyu Lowassa anajua kwamba yeye alivyo hawezi kugombea urais, isipokuwa kwa sababu he is so determined kua Rais, ataishia siku moja kutupiga changa zito sana la macho, ninaamini and I could be wrong pia, kwamba ata-push to end kugombea urais 2010 akijua sana kwamba hawezi kupata nafasi, in the process ataisukuma na kui-pressure our political system nzima to the wall that kutakua na a political deal ya kumrudisha kwenye power under some capacity, itakapofika 2015 Lowassa atamuweka mtu wake kuchukua urais halafu yule mtu hatamaliza kwa sababu atakazopewa na Lowassa yaani atajiuzulu, hapo ndipo huyu Lowassa ataliliwa na chama kizima achukue Urais ndio the only chance aliyonayo na ninaamini ndiyo njia atakayotumia kushika urais kama ndoto yake inavyomtuma.

Respect.

FMEs!

Mkuu FMEs nimekuvulia kofia kwa kuwa umeweza kuingia ndani ya bongo ya mafisadi na kuvumbua mipango miovu wanayopanga.Kwa akili ya kawaida kabisa watu wanafikiri itakuwa kiwepese Lowasa kurudi madarakani.La hasha haitakuwa hivyo kwa sababu kunapingamizi kubwa toka kwa wanaojipambanua kuwa ni wapiganaji wa ufisadi.

Njia pekee ya Lowasa kurudi madarakani ni kama alivyoainisha FMEs na hii inasababishwa na political schemes ambazo mafiasadi wamezoea kuzicheza kwa muda mrefu sasa.Kwa kweli Tanzania tunakazi pevu mbele yetu.
 
- Mkuu watu wenye akili nyingi sana duniani wanapokwama hurudi kwenye msingi wa walipotokea, binafsi ninakumbuka Lowassa na Rais wa sasa wakiitwa Boyz To Man, wakakodiwa ndege maalum ya kuwapeleka Dodoma dakika za mwisho wa kikao cha NEC ili wawe alternative ya kugombea urais, wananchi wa taifa hili we never questioned nani amelipia ile ndege, na WHY? Lowassa na Rais wa sasa nani aliwaita dakika za mwisho kwenda Dodoma kwa sababu no question kwamba hawakuitwa na Mwalimu!

- Lowassa alikuwa njiani kugombea urais ninachojua ni kwamba he was a serious candidate kuliko Rais wa sasa, sasa ilikuwaje akaamua kukaa pembeni na kumuachia Muungwana? Kuna dataz moja niliwahi kuzipata then, one time Lowassa alikuwa mahali akizungumza na mtu kwa siri sana, aliulizwa vipi Urais, akamjibu yule mtu tena with confdence sana kwamba "..ninaweza kuwa rais nikitaka maana this is my chance, lakini siwezi kuharibu utamaduni ambao inayokuja ni zamu ya Muisilamu kuwa Rais..." akaendelea "..mimi na Jakaya ni kitu kimoja, tumeongea na nimemfahamisha hilo kwamba ninamuachia kwa sasa.." haya yote niliyasema zamani

- Kwamba Lowassa atapata matatizo ya kisheria under Muungwana's watch haitakuja kutokea, kwamba atakuwa Rais in our watch ninasema haitakuja kutokea unless CCM ivunjike, yanayotukuta sasa ni matatizo tuliyoyataka wenyewe wananchi na hasa hawa waandishi wetu wa habari, we were so happy na political deals za short terms bila kujua nini hasara zake in the long terms na ndio what we are paying for now, Lowassa is fine for now, ingawa matatizo yake kisheria yapo pale pale ndio maana Rostam anayejua better analilia sana majaji kuamua kuhusu Richmond.

- Wananchi tunahitaji kua macho sana, ninaamini sana kwamba huyu Lowassa anajua kwamba yeye alivyo hawezi kugombea urais, isipokuwa kwa sababu he is so determined kua Rais, ataishia siku moja kutupiga changa zito sana la macho, ninaamini and I could be wrong pia, kwamba ata-push to end kugombea urais 2010 akijua sana kwamba hawezi kupata nafasi, in the process ataisukuma na kui-pressure our political system nzima to the wall that kutakua na a political deal ya kumrudisha kwenye power under some capacity, itakapofika 2015 Lowassa atamuweka mtu wake kuchukua urais halafu yule mtu hatamaliza kwa sababu atakazopewa na Lowassa yaani atajiuzulu, hapo ndipo huyu Lowassa ataliliwa na chama kizima achukue Urais ndio the only chance aliyonayo na ninaamini ndiyo njia atakayotumia kushika urais kama ndoto yake inavyomtuma.

Respect.

FMEs!

Heshima kwako FMEs,

Mkuu maneno mazito sana ukweli kuna wakati namuomba Mungu atuepushie huyu jamaa kwasababu anaweza kuipeleka nchi mahali pabaya.Bado naamini wapo wapiganaji wachache ndani ya CCM watakaomzuia/wanaomzuia Lowassa.Ninaamini bila uwepo wa wapiganaji wachache ndani ya CCM hizi kelele za ufisadi zingeshasahaulika siku nyingi.Wapo baadhi ya wanajamvi wanaowabeza wapiganaji lakini kazi walioifanya si haba.

Dayosisi KKKT kanda ya kaskazini[Arusha & Manyara] itazindua jina jipya la dayosisi nadhani 27 / 28 Feb 2010. Mwenyekiti wa kamati ya maadalizi alipoiarifu kamati kwamba Askofu Laiser Kamwalika Lowassa kuwa mgeni rasmi kamati nzima ikakataa kabisa.Jana jumapili Askofu T Laizer kakubali kuondoa jina la Lowassa ,nikasema kumbe inawezekana hata ndani ya CCM wajumbe wakashinikiza atoswe.
 
Lowassa yuko sahihi kabisa na kwasabau hiyo basi hawataweza kumuwajibisha Lowassa kwakuwa chama kizima kina hoja za kujibu.Watatoka vipi katika suala la Kagoda?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom