CCM, Operation TUJISAHIHISHE irudiwe tena!

Kwakuwa imeishiwa ushawishi na inaona aibu kukubali, na sana sana hofu yao kubwa watakapotoka madarakani wengi wao wataishia jela kutokana na wizi na unyama waliofanyia wananchi.
Umenikumbusha siku ya Mkutano Mkuu maalum wa CCM, Mzee Wasira alipopewa nafasi ya kumsifia Kinana, akaeleza Chama Chao kilivyokuwa na Hali ngumu mwaka 2012 Hadi uchaguzi wa 2015. Nikakumbuka mwaka huo huo huyu Mzee alivyotabiri kifo cha CHADEMA kabla ya 2015 nikamuuliza, makanisani na misikitini huwa wanakwenda kufanya nini kama ni Wanafiki kiasi hicho?

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Kwa machalii na dogo wengi, hawawezi kuijua hii Operation Tujisahihishe , ambao ulikuwa msimamo wa chama TANU, Mwaka 1976/77.

Mwalimu, a thinker, strategist na visionary, aliliona tatizo katika misimamo ya chama, misimamo ambayo ilileta utata na matatizo makubwa katika jamii.

Mojawapo ya matatizo ni msimamo wa chama cha TANU Operation Musoma, ambapo wanafunzi wote waliomaliza Form VI walitakiwa kwenda JKT kwa mwaka mmoja na kujajiriwa kwa mwaka ndipo waende Chuo Kikuu chochote.

Athari zake zilikuwa kubwa na mbaya sana, hasa kwa wanawake, waliopoteza nafasi za kusoma na kuishia kuolewa.

Operation TUJISAHIHISHE, ya 1976, ilikuja ondoa kabisa kadhia hii, kwa kujisahihisha wenyewe, na sasa CCM kusonga mbele.

CCM ya sasa na vikao vyake vya Kamati zKuu na Halmashauri Kuu hadi Mkutano Mkuu, havijaweza mpaka sasa kuwa na ujasiri wa kutamka wazi wazi madudu ya kutisha, ya kisiasa ya Awamu ya Tano.
Awamu ya Tano ni zao la CCM.

Hatuwezi kuwaachia wapinzani, kina Zito wa ACT, ndio watuonyeshe njia sahihi wakati nasi tulikuwepo na tuliona madudu na tunajua namna ya kuyasahihisha.

Naamini Komredi Kinana, na hata Kikwete miaka ya Operation Tujisahihishe walikuwa vijana wa TANU.
Hili ni somo ambalo chama, kwanza kikubali makosa makubwa yalitendeka , pili chama kitamke namna ya kuyasahihisha ili yasirudiwe tena.

Huo ndio utakuwa ukomavu wa kisiasa kwa chama CCM.
CCM ya Sabaya, Magufuli, ALLY HAPPY, usalama, polisi, utekaji, uuaji, ubambikiaji kesi haina cha kujisahihisha. Isubiri kuchomwa moto na MUNGU.
 
Hayo ni pamoja na madudu ya wizi .ambayo hayatokani na msimamo wa chama.

Ni msimamo usio rasmi wa chama. Fursa za wizi, ubadhirifu na ufisadi ndicho kivutio cha wengi katika hicho chama dola. Ndio kete kuu inayotumika “kununua” wapinzani wanaotishia uhai wa CCM.
 
Mkuu CCM, kwa muda mrefu tu ujao, kitakuwa ni chama kinachoonyesha dira ya mustakabali na muelekeo wa wananachi wa Tanzania.Na CCM ni chama kikubwa kuliko mtu yeyote.
CCM lazima iendeshwe na mawazo chanya, hakiwezi kujifungia na kutekwa katika pressure groups za ukabila, ubaguzi hata ukanda.

Kujisahihisha ni muhimu kwani chama kutakuwa kime preempt matatizo yake yenye athari mbaya katika jamii.

Vilevile kujisahihisha ndio guarantee kwamba makosa yaliyofanyika hayatarudiwa tena.

The only solution ni pale mtakapokubali kumuondolea Rais wa JMT “absolute power”, kumuweka chini ya utawala wa sheria, na kurejesha uhuru wa Bunge, mahakama na tume ya uchaguzi: Katiba mpya ya JMT.
 
Ccm haijawahi kushinda..ni wizi wa kura na mabavu...kupitia tume na vyombo vya dola.

#MaendeleoHayanaChama
Exactly. Ingawa naamini 2005 walishinda uRais kwa kura halali ingawa, kama kawaida yao, lazima waliiba za ziada kwa kutojiamini.
 
The only solution ni pale mtakapokubali kumuondolea Rais wa JMT “absolute power”, kumuweka chini ya utawala wa sheria, na kurejesha uhuru wa Bunge, mahakama na tume ya uchaguzi: Katiba mpya ya JMT.
Naafiki absolutely!
 
Kwanini CCM ilipora uchaguzi mkuu?
Chama kikiwa na unpopular policies, watendaji wake wanataka status quo, iliwabaki madarakani.

Niliwahi shangazwa na kauli za aliyekuwa Katibu Mkuu CCM, Bashiru Ali Kakurwa, kuwa malengo makuu ya chama chochote ni kubaki madarakani, hata kwa kutumia dola!

Hapo nikajua, kama waingereza wasenavyo, The Party has gone to the dogs!
 
Ni ngumu kwa Sasa kuanzisha operation aina hiyo kwa sababu itakuwa kwa sehemu kubwa kuzungumzia madudu ya awamu ya tano. Tatizo ni kwamba masalia ya Magufulist bado wapo wengi na wanaweza kukiletea chama chao mtikisiko mkubwa sana.
Tayari Kuna tetesi ya kuanzishwa chama Cha masalia hao ingawa kwa ubabe wa CCM hakiwezi kusajiliwa aslan.
Hayo mambo walishindwa kina Mzee Samuel Sitta na CCJ yao wakaishia kumtowa kafara Fred Mpendazoe wao na kina Nape wakabaki ccm.
 
Hayo ni pamoja na madudu ya wizi .ambayo hayatokani na msimamo wa chama.
Makosa mengine ni ya viongozi binafsi, na hayaendani kamwe na misimamo na sera za chama.
CCM haijawahi kuvumilia uonezi, ukabila, ubabe wa kiongozi, wizi na maovu kama hayo.
 
..Ccm haina culture ya kujadiliana hoja kwa hoja mpaka hoja iliyobora ishinde.

..mara nyingi hoja na mitizamo ya mwenyekiti ndiyo hupitishwa harakaharaka.

..wanaoonekana kutofautiana na mwenyekiti huitwa majina mabaya na kumalizwa kisiasa.

..utamaduni huo umekuwepo tangu enzi za Mwalimu Nyerere ambapo wengi waliotofautiana naye waliitwa majina mabaya kama wasaliti, vibaraka, etc etc.

..kwa mfano, wakati hali yetu ya uchumi ni mbaya miaka ya 1980 kuna baadhi ya viongozi walianza kudai marekebisho ya sera zetu za uchumi. viongozi hao walipewa majina mabaya na wenzao ikiwemo kuitwa wasaliti na baadhi yao walianguka ktk chaguzi mbalimbali za Ccm.

..Udini, ukabila, ukanda, uzushi, ukatili, ni baadhi ya mbinu zinazotumiwa ndani ya Ccm kuwakabili wale wanaotofautiana na mwenyekiti, au walioko nje lakini wanakitishia chama chao.
 
Mleta mada ni mtu mjinga na asie na ufahamu wowote kuhusu nchi na ccm,tujisahihishe ni kitabu kilichoandikwa na mwl nyerere mwaka 1992,baada ya utepetevu na rushwa iliyokuwa imetamalaki ndani ya chama na serikali yake,lkn kubwa zaidi ni zanzibar kujiunga na oic, na wabunge 55 wa ccm wakiongozwa na njeru kasaka,Philip marmo,tuntemeke SANGA,na crizant maji ya tanga mzindakaya,nafkiri hata huyu mlevi na mvuta bangi jenerali ulimwengu alikuwepo,nyerere alichukia sana,John Marcella aliliwa kuchwa,
 
Hayo ni pamoja na madudu ya wizi .ambayo hayatokani na msimamo wa chama.
Lakini chama chako CCM kimebariki wizi huo, serikali imeundwa kutokana na wabunge waliotokana na wizi wa kura, na bunge la CCM linaendelea kutunga sheria na kuishauri serikali. Huwezi kusema madudu hayo hayatokani na chama chako.

Ukiamua kujisahihisha, kubali mapungufu yote yaliyosababishwa na CCM, vinginevyo acha maisha yaendelee.
 
Ni ngumu kwa Sasa kuanzisha operation aina hiyo kwa sababu itakuwa kwa sehemu kubwa kuzungumzia madudu ya awamu ya tano. Tatizo ni kwamba masalia ya Magufulist bado wapo wengi na wanaweza kukiletea chama chao mtikisiko mkubwa sana.
Tayari Kuna tetesi ya kuanzishwa chama Cha masalia hao ingawa kwa ubabe wa CCM hakiwezi kusajiliwa aslan.
Kianzishwe tu, watu wagawane mbao. Tuanze upya.
 
Kwa machalii na dogo wengi, hawawezi kuijua hii Operation Tujisahihishe , ambao ulikuwa msimamo wa chama TANU, Mwaka 1976/77.

Mwalimu, a thinker, strategist na visionary, aliliona tatizo katika misimamo ya chama, misimamo ambayo ilileta utata na matatizo makubwa katika jamii.

Mojawapo ya matatizo ni msimamo wa chama cha TANU Operation Musoma, ambapo wanafunzi wote waliomaliza Form VI walitakiwa kwenda JKT kwa mwaka mmoja na kujajiriwa kwa mwaka ndipo waende Chuo Kikuu chochote.

Athari zake zilikuwa kubwa na mbaya sana, hasa kwa wanawake, waliopoteza nafasi za kusoma na kuishia kuolewa.

Operation TUJISAHIHISHE, ya 1976, ilikuja ondoa kabisa kadhia hii, kwa kujisahihisha wenyewe, na sasa CCM kusonga mbele.

CCM ya sasa na vikao vyake vya Kamati zKuu na Halmashauri Kuu hadi Mkutano Mkuu, havijaweza mpaka sasa kuwa na ujasiri wa kutamka wazi wazi madudu ya kutisha, ya kisiasa ya Awamu ya Tano.
Awamu ya Tano ni zao la CCM.

Hatuwezi kuwaachia wapinzani, kina Zito wa ACT, ndio watuonyeshe njia sahihi wakati nasi tulikuwepo na tuliona madudu na tunajua namna ya kuyasahihisha.

Naamini Komredi Kinana, na hata Kikwete miaka ya Operation Tujisahihishe walikuwa vijana wa TANU.
Hili ni somo ambalo chama, kwanza kikubali makosa makubwa yalitendeka , pili chama kitamke namna ya kuyasahihisha ili yasirudiwe tena.

Huo ndio utakuwa ukomavu wa kisiasa kwa chama CCM.
Mkuu Mudawote ukuje umsome kada mwenzako huku.
 
Nadhani tunachotofautiana ni namna ya kuyajadili haya mambo ya awamu ya 5 ambayo kimsingi hata Mama Samia naye ni sehemu ya hii ripoti ya kupikwa. Mazuri yote yaliyofanyika chini ya Dkt Magufuli yanajulikana na wengi wanakubali, inakuwaje mnakomaa na vitu petty vya kupika???
 
Kawaida kenge hasikii hata pale ubongo utakavyo ning'inia nje ya fuvu lake🐒
 
Nadhani tunachotofautiana ni namna ya kuyajadili haya mambo ya awamu ya 5 ambayo kimsingi hata Mama Samia naye ni sehemu ya hii ripoti ya kupikwa. Mazuri yote yaliyofanyika chini ya Dkt Magufuli yanajulikana na wengi wanakubali, inakuwaje mnakomaa na vitu petty vya kupika???
Vyakupika wakati yote ya awamu Yako pendwa mambo hadharani 🤸🤸
 
Back
Top Bottom