Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 17,563
- 28,524
Kwa machalii na dogo wengi, hawawezi kuijua hii Operation Tujisahihishe , ambao ulikuwa msimamo wa chama TANU, Mwaka 1976/77.
Mwalimu, a thinker, strategist na visionary, aliliona tatizo katika misimamo ya chama, misimamo ambayo ilileta utata na matatizo makubwa katika jamii.
Mojawapo ya matatizo ni msimamo wa chama cha TANU Operation Musoma, ambapo wanafunzi wote waliomaliza Form VI walitakiwa kwenda JKT kwa mwaka mmoja na kujajiriwa kwa mwaka ndipo waende Chuo Kikuu chochote.
Athari zake zilikuwa kubwa na mbaya sana, hasa kwa wanawake, waliopoteza nafasi za kusoma na kuishia kuolewa.
Operation TUJISAHIHISHE, ya 1976, ilikuja ondoa kabisa kadhia hii, kwa kujisahihisha wenyewe, na sasa CCM kusonga mbele.
CCM ya sasa na vikao vyake vya Kamati zKuu na Halmashauri Kuu hadi Mkutano Mkuu, havijaweza mpaka sasa kuwa na ujasiri wa kutamka wazi wazi madudu ya kutisha, ya kisiasa ya Awamu ya Tano.
Awamu ya Tano ni zao la CCM.
Hatuwezi kuwaachia wapinzani, kina Zito wa ACT, ndio watuonyeshe njia sahihi wakati nasi tulikuwepo na tuliona madudu na tunajua namna ya kuyasahihisha.
Naamini Komredi Kinana, na hata Kikwete miaka ya Operation Tujisahihishe walikuwa vijana wa TANU.
Hili ni somo ambalo chama, kwanza kikubali makosa makubwa yalitendeka , pili chama kitamke namna ya kuyasahihisha ili yasirudiwe tena.
Huo ndio utakuwa ukomavu wa kisiasa kwa chama CCM.