Hossam
JF-Expert Member
- Feb 10, 2011
- 3,538
- 2,155
Napenda kukipongeza CCM namna kinavyojitahidi kila siku kuja na mbinu mpya ya wizi wa kura na wizi wa maliasili za watanzania, zaidi sana na pesa zetu katika benki kuu yetu na mawizarani. Nafarijika sana kuwaona watoto wa wakubwa wakiishi maisha ya anasa, ubabe na kwa viburi vya baba zao huku wakiwa juu ya sheria kwa sababu sheria za Tanzania zilitungwa kwa ajili ya makabwela na sio wenye nazo.
Binafsi nafurahi sana kuona mafisadi wakubwa wa nchi hii wanatokea CCM na hakuna wa kuwafanya kitu kwa kuwa hakuna sheria wala chombo chochote cha dola chenye uwezo wa kuwakabili. Taasisi ya Urais ya JK nayo ikilegalega napata faraja mno, na zaidi sana napenda kila mara kuona mheshimiwa rais akirandaranda nchi za nje kutafuta chakula kwa watanzania.
Inaleta matumaini sana kuona CCM ikifanya kila hila kulithisha uongozi wa watoto na ndugu zao ili kulinda maslahi yao na kuendeleza unyonyaji kwa Watanzania mambumbumbu wasio na uwezo wa kuhoji, na zaidi sana naoenda kuona nafasi zooote nyeti serikalini zikiendelea kuteuliwa na rais kwa manufaa yake.
Inanipa raha sana kuona mafaili ya wala rushwa na wezi wa pesa za umma yanapotea hovyo kwenye ofisi nyeti serikalini na hakuna wa kuhoji kwa sababu sisi ni mambumbumbu kabisa, na naona raha kabisa mtu mmoja wa CCM akiwapiga mkwara Watanzania milioni 55 bila hata mmoja kuhoji. Hii inanipa raha sana kwa kuwa sasa CCM itatumia watu wachache kuwatisha wananchi kwa kuwa hao wachache ndio walioichafua CCM, yaani win win situation, naona raha kabisa.
Binafsi na familia yangu tunafarijika sana kuwaona Watanzania milioni 55 wakikenua meno wamuonapo rais wao huku kwa hakika hakuna wanachoambulia zaidi ya kuungua na jua na kupanda mafuso ili kujaza watu.
Napenda na naomba mafisadi wazidi kushika makampuni muhimu nchini na tenda hata za ikulu zitolewe kwa upendeleo ili CCM izidi kupendwa na mafisadi. Zaidi sana nasikia raha sana kuona fujo zile za Kivukoni na jinsi watanzania wanavyopoteza muda kusubiria MV Kigamboni na Magogoni, hata daraja lile linalojengwa Kurasini linanipa raha sana kwa kuwa watu sasa hawataweza kwenda huko maana ni ujinga kabisa, hii ina maana serikali ya CCM itajisifu kujenga daraja hilo na lakini itasema hatutaondoa vivuko hivyo anayetaka daraja achome mafuta kurasini ama aendelee kulipia vivuko, sasa kwa sababu njia ya mkato ni vivuko basi daraja litumiwage kwa fujo na daladala za mbagala tu. Hii inanipa raha sana.
Nafarijika mno kuona mheshimiwa rais anatembea na first class ambulance wakati wakazi wa Kibondo na Tabora wanaendelea kufa bila kuwa na vitua vya afya halafu wakimuona kiongozi wa CCM wanakenua tu meno, hii inanipa raha sana.
Mwisho nafarijika kuona maisha yanakuwa magumu na ajira hakuna nchini. Nasikia raha mno kuona sukari inauzwa sasa hadi na polisi kwa kuwa inafaida kwa wenzetu na sio bongo, naona raha pale PM anaposema sasa JWTZ italinda sukari badala ya mipaka maana polisi kazi yao kumbe ni vibaka wadogo wadogo wa kariakoo, hii inanipa faraja sana ikizingatiwa kwamba mkuu wao yaani IGP anafurahia kusifiwa kwamba yeye anaweza sana kula sahani moja na vibaka wa kariakoo na sio wahujumu uchumi halafu akipewa na lile V8 basi anakenua meno tu, nasikia raha sana aiseee.
CCM ikiiba kura, ikiendesha siasa za mwenyenacho mpishe, ubabe, uimla, vitisho na ubaguzi kwangu ni raha sana aisee. Mwigule eehh hivi hakuna mchongo mwingine wa wizi BOT? Nataka na mie kuleta scania langu lina tani 40 nadhani litasaidia ubebaji. CCM raha sana, mungu awatie nguvu aisee muendelee hivyohivyo hadi akili zitusogee!!! Kesho nitaleta ya Chadema, stay tuned.