Ccm ni ufalme uliofitinika ni lazime ufe.

Sengeon

JF-Expert Member
Dec 29, 2011
529
112
Chama cha Mapinduzi kwa sasa wamekaa kama ufalme uliofitinika.

Ikimbukwe mpaka sasa kuna Makundi Matatu hasimu ambao hawaelewani wala hawapikiki chungi kimoja na wote kwa pamoja wako kwenye kauli inayoitwa bora tukose wote.

1- Kundi la kwanza ni lile la Mb wa Monduli ndg Lowasa. Hili kundi mpaka sasa ndilo linaloonekana kuwa na nguvu kubwa. Ni kundi ambalo linacheza rafu sana kwa mtu yeyote anayeonyesha kuhatarisha mbio za mgombea wao.

2- Kundi la Membe. Hili kundi linaonyesha kuwa na ushawishi kupitia kwa Viongozi waandamizi na linaonekana kuwa mshindani mkuu katika mbio za kusaka kwenda ikulu. Hili kundi ndilo linalojitahidi kuhakikisha Lowasa anakatwa ktk Kamati kuu.

3- Kundi la Sitta. Hili ni kundi ambalo limekuwa na ugomvi wa mda mrefu sana na kundi la El na haliko tayari kabisa kumuunga mkono endapo atapata nafasi ya kupeperusha Bendera ya Ccm. Pia kundi hili limeendelea kupoteza Mvuto siku hadi siku.

Hawa wote ni kama Watoto wa Mfalme ambao wote wanataka kuridhi Ufalme wa Baba yao. Na kati yao hakuna ambaye yuko tayari kumuunga Mkono mwenzie endapo atachaguliwa.

Namalizia kwa kusema - Ccm ni ufalme uliofitinika na ni lazima utasambaratika.
 
Back
Top Bottom