CCM ni mali ya Makamba na Msekwa.

Tonge

JF-Expert Member
May 7, 2010
695
12
NAWAHABARISHA WAKEREKETWA WA CCM KUWA CCM SI MALI YOA ILA NI MALI YA MAKAMBA NA MSEKWA.HAWA WAHESHIMIWA WAMETOA KAULI ZINAZODHIHIRISHA HAYA.

MFANO MSEKWA ALITOA RUHUSA KWA "WANACCM WALIOSHINDWA KWENYE KURA ZA MAONI PAMOJA NA WANAOWAPENDA WANAWEZA KUHAMA CHAMA KAMA WAKIPENDA" NA HII YA URAIA WA BASHE MAKAMBA ANASEMA "NIMEPOKEA VIDHIBITISHO VYA URAIA TOKA UHAMIAJI KUWA BASHE NI RAIA LAKINI MI NASEMA BASHE SI RAIA LICHA YA KWAMBA CHAMA TUNAKIPENDA"

Kauli hizi na nyingine vyingi zinathibitisha kuwa CCM ni chama cha watu hawa wawili,KWANI WAO HUWEZA KUSEMA MANENO YA NYODO AU DHARAU NA KUAMUA MAMBO MENGI WENYEWE BILA VIKAO MUHIMU VYA CHAMA,

Je wanachama mliopo mnangoja nini? kwani hawa wanao uwezo wa kuwalinda wale wawatakao kama ilivyotokea kwa Iringa nk.Hameni muwang'oe madarakani kama kundi la wanachama wa KANU waliohama wakiing'oa KANU madarakani.Karibuni CHADEMA tuungane kuking'oa Chama Cha Majungu (CCM).
 
Huo ni ulevi wa madaraka, lakini watakuja jutia kauli zao hizo za kishamba, hebu wamuulize JK anavyopata tabu ya kukanusha nyodo yake kwa wafanyakazi. Ila kwa upande mwingine naona tambo za hivi vijeba ni blessing in disguise, kwani wanakibomoa wenyewe chama chao kwa manufaa ya upinzani.
 
Nadhani na uzee nao unachangia kwa hawa wazee kuwa na kauli hizi..Ila inaonekana dhairi kuwa bashe hakubaliki ndani ya wazee hawa...
Sioni watu jasiri kwenye CCM wakuweza kufanya mapinduzi kama yaliyofanyika KENYA..sie watz tunaweza kuongea weee pasipo vitendo....Km watz tungekuwa na ujasiri kama wa watu wa tarime ambao ni kama wakenya tu..tungeweza kuibadilisha na kuipa nidhamu CCM
 
Mwenye masikio asikie, mwenye macho aone na mwenye miguu.................
 
Nadhani na uzee nao unachangia kwa hawa wazee kuwa na kauli hizi..Ila inaonekana dhairi kuwa bashe hakubaliki ndani ya wazee hawa...
Sioni watu jasiri kwenye CCM wakuweza kufanya mapinduzi kama yaliyofanyika KENYA..sie watz tunaweza kuongea weee pasipo vitendo....Km watz tungekuwa na ujasiri kama wa watu wa tarime ambao ni kama wakenya tu..tungeweza kuibadilisha na kuipa nidhamu CCM

Naskia hili zengwe limeanzishwa na mtoto wa mzee wa kaya.. Kama ilitokea kwa masuni atakuwa Bashe? Yanayotokea ndani ya Chama cha Majungu ni kama mtu aliyekula akavimbiwa akaamu kijitapisha sasa njaa imemkaba ameamua kuyala yale yale matapishi ili kusitiri njaa...
 
Huu ndio uzuri wa kuwa mwanaJF, kweli hapa ndipo watu wanye akili timamu na wanye uchungu wa nchi yao hukutana, Hivi huyu dogo anakiendesha chama cha majungu kama naniiiiiiiiiii?, halafu juzi juzi tu ndio kamaliza chuo na kuanza kazi hapo BRELA atawezaji kumiliki jengo la gorofa kadhaa moro, kama si kutaka kuendelea au kutaka kulindwa na serikali.Jamani eeeeeh tuungane tuwamng'oe dingi yake madarakani kisha tuwachunguze uhahali wa mali zao kisha tuwafilisi kwa manufaa ya uma sio kama Liyumba walivyomlinda.

Slaa mwendo ule ule Baba tumechoka kunyanyaswa na kufisadiwa na serikali ya CCM.
 
Upinzani wakiungana na kusimamisha mgombea mmoja, Mkuu wa Kaya CHALI kama ya mende.
 
Upinzani wakiungana na kusimamisha mgombea mmoja, Mkuu wa Kaya CHALI kama ya mende.

Wakisha ungana wamsimamishe nani? Slaa au Lipumba au mgombea mwingine yeyote?
Ninavyojua mimi Cuf hawatakubali asiposimamishwa Lipumba kwani hawana mgombea mwingine wanayemwamini kwa ngazi ya uraisi zaidi ya Lipumba.
 
Nafikiri iko haja ya wataalamu wa sheria kufafanua suala la uraia wa Bashe kama anastahili au la manake tukiongea kiushabiki yawezekana likatushuka..nahisi kiko kitu wanajiamini nacho ndo mana wamemtosa...Tafsiri ya kisheria inahitajika kuliko chochote...tupate picha kamili ya mazingira ya utata wake na tafsiri ya kisheria ni nini hatma ya sakata hili.( yani hatua kwa hatua toka anazaliwa hadi anaukana uraia wa somali 2008 na je aliomba wa TZ na mambo yatayosaidia kutoa mwanga)
 
Lakini je vyama vya upinzani vipo tayari kuungana na kusimamisha mgombe wake kwenye uchaguzi wa raisi?
 
Naskia hili zengwe limeanzishwa na mtoto wa mzee wa kaya.. Kama ilitokea kwa masuni atakuwa Bashe? Yanayotokea ndani ya Chama cha Majungu ni kama mtu aliyekula akavimbiwa akaamu kijitapisha sasa njaa imemkaba ameamua kuyala yale yale matapishi ili kusitiri njaa...

Onother umbeya jf. Sidhani kama anajeuri hiyo. Aitoe wapi. I said again this is onother umbeya.
 
Onother umbeya jf. Sidhani kama anajeuri hiyo. Aitoe wapi. I said again this is onother umbeya.

Hiyo waliyokuambia kuwa zatokea kwa mtoto wa mzeee ndio kweli twajua sie anapolenga na anawaandaa watu kwa ajili ya 2015 kaaa ujue hilo mkuu soma alama za nyakati we wazania kila kitu ni umbea humu ngoja omba MUNGU akupe pumzi ya uhai wako iliufike hiyo 2015.

Jiulize kwanini alikwenda piga kambi Nyamagana kumwokoa Masha?
Jiulizi huyo aliyeshinda Maswa na kumbwaga Shibuda anauwezo gani?

NAWAHABARISHA WAKEREKETWA WA CCM KUWA CCM SI MALI YAO ILA NI MALI YA MAKAMBA NA MSEKWA.

Una hakika ? Huyo aliyewateua Makamba na Msekwa unamweka wapi ? Kwa nini usiseme CCM ni yake mwenyewe Mkulu - hawa ni marugaruga tu.

HAWA WAHESHIMIWA WAMETOA KAULI ZINAZODHIHIRISHA HAYA.

Je, una hakika hizo kauli zao hazina baraka zake ? Kama ni hivyo kwa nini hawatimui ? Kwani kauli zake Mkwere zinadhihirisha nini ?
Kauli hizi na nyingine vyingi zinathibitisha kuwa CCM ni chama cha watu hawa wawili,KWANI WAO HUWEZA KUSEMA MANENO YA NYODO AU DHARAU NA KUAMUA MAMBO MENGI WENYEWE BILA VIKAO MUHIMU VYA CHAMA,
Hivi maneno yao ya nyodo na dharau yanapishana na ya Mwenyekiti wao ? Unajuaje hawatumi kusema wanayoyasema ? Mbona unataka kuwaonea Msekwa na Makamba ? Aliyesema hataki kura za wafanya kazi mbona unamsetiri ?
Je wanachama mliopo mnangoja nini? kwani hawa wanao uwezo wa kuwalinda wale wawatakao kama ilivyotokea kwa Iringa nk.Hameni muwang'oe madarakani kama kundi la wanachama wa KANU waliohama wakiing'oa KANU madarakani.Karibuni CHADEMA tuungane kuking'oa Chama Cha Majungu (CCM).
Kuwang'oa Makamba na Msekwa pekee kutasaidia nini kama mlinzi mkuu wa mafisadi yuko pale pale kajaa tele. Je, Makamba anaweza kukohoa mbele ya Rostamu au Msekwa atasema nini mbele ya Chenge. Mkuu Tonge kwenye hii vita tusimwonee yeyote haya, Makamba na Msekwa ni kama matawi tu, mizizi ndio yahitaji kung'olewa. Humwui nyoka kwa kumkata mkia, unamponda kichwa !
 
Back
Top Bottom