Crashwise
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 22,227
- 8,739
Na Cecilia Pareso.
Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza wafanyakazi nchini leo wanapoadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani.
Nimemsikia Rais, katika hotuba yake ameahidi kushusha kodi ya Pay As You Earn(PAYE) toka asimilia 11 ya sasa hadi asilimia 9 katika mwaka ujao wa fedha 2016/17.
Jambo hili si la ajabu sana, nashangaa Serikali ya CCM inasikia ushauri huu leo. Katika Bunge la Kumi Kambi ya Upinzani mimi nikiwa Waziri Kivuli katika ushauri niliokuwa natoa kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, mara zote(rejea hotuba zetu zote), tuliitaka serikali ya CCM kupunguza mzigo huo mkubwa wa kodi kwa wafanyakazi nchini ila tulipuuzwa na kudharauliwa.
Ni kweli kuwa Serikali hii inachelewa kuelewa. Hivi leo wana CCM na wafuasi wa CCM watashangilia kwa kuwa Magufuli amesema. Ni wakati wa kuangalia chanzo cha hoja imetoka wapi na si kufunikwa akili zetu kwa uvivu wa kufikiri na kutanzua mambo. Katika hali halisi ni kwamba CHADEMA na washirika wake wa UKAWA wameshinda na si Magufuli na CCM!! Hii ni sawa na kutumia "Copyright au Trademark " ya mtu na kujisifu kuwa wewe ndiye mmiliki wa Kampuni au Biashara fulani.
Maslahi ya Wafanyakazi yasiishie kupunguza tu PAYE bali pia yajikite katika kuboresha mazingira ya Wafanyakazi katika nyanja zote. Sambamba na kuongeza pia ujira wa wafanyakazi. Msingi wa ujenzi wa Nguvukazi yenye tija ni pamoja na kuboresha mazingira yao ya Kazi na kuwa na vitendea kazi visivyo na mashaka katika maeneo yao ya Kazi.
Ifike mahali Viongozi wa CCM wajifunze kutanzua hoja mbadala kutoka vyama vingine vya siasa.
Haiwezekani CCM chama kikongwe chenye mifumo ya muda mrefu wakawa ni watu wa kukandamiza hoja za Upinzani wakati huo huo kwa mlango wa nyuma wanazinyakua na kuzikwapua.
Bado tunaamini CHADEMA ndiyo tunaoongoza nchi kwa kila agenda ya kisiasa yenye mlengo wa Kuinua ustawi wa maisha ya Mtanzania.
Nawatakia wafanyakazi Siku Kuu Njema ya Wafanyakazi Duniani.
CECILIA DANIEL PARESSO (MB)