CCM ni chama pekee Afrika chenye wanachama wengi

chamilo nicolous

JF-Expert Member
Mar 10, 2016
1,991
1,364
FACT KUELEKEA UCHAGUZI:- MTAJI WA WAGOMBEA.

Na Thadei Ole Mushi.

Ccm inakwenda kwenye uchaguzi ikiwa na Jumla ya Kura Milioni 11,111,500 (Milioni Kumi na moja,Laki Moja,kumi na Moja elfu na miatano).

Ipo hivi Jumla ya matawi ya CCM nchi nzima na yaliyoshiriki Kura za maoni Ni 2,22,230 kila tawi moja lina wanachama 50 hivyo kufanya kuwa na jumla ya wanachama 11,111,500 nchi nzima. Kwa hiyo hizi ndio kura za wanaCCM za kuanzia 2020.

Ndio chama pekee barani Africa chenye wanachama wengi kuliko vyama vingine. Ndio chama pekee ambacho kina mfumo imara kuanzia kwenye kundi la kaya kumi kwa maana ya mabalozi wa nyumba kumi kumi.

Waliojiandikisha kupiga Kura mwaka 2020 kwa mujibu wa website ya tume ya Taifa ya uchaguzi ni 29,188,347 ukitoa Kura za wanachama wa CCM kwa mujibu wa matawi yao zinabaki Kura 18,076,847.

Hizi kura 18,076,847 tuondoe hapo wanachama wa Chadema Milioni tano kwa mujibu data zilizopo kwenye makarabrasha yao kupitia Kampeni ya sera mbadala. Ukitoa Hawa wanachadema wanabakia Wapiga Kura 13,076,847.

Hawa waliobakia 13,076,847 ndio wanaoshawishiwa kwenye Kampeni na Rais Magufuli na Lisu. Kwenye hizi Kura zilizobakia CCM wanahitaji Kura Milioni 4 tu watafikisha Kura Milioni 15 plus. Kura hizi haziwezi kufikiwa na chama chochote kile.

Hali Halisi.

Sio Siri mgombea wetu wa CCM anaelezea Mambo mengi aliyoyafanya na Ni yapi atayafanya kipindi kijacho. Kwenye kuelezea hili amelenga nadharia ya Win win situation, kuwa nipeni kura Jimbo A na mm niwatatulie shida zenu kwa kuwapa priority.

Pamoja na kwamba Upinzani wanapinga nadharia hii ya win win situation Ila Ni mwiba mchungu Sana kwenye Kampeni hizi. Hakuna namna unayoweza kumwambia mtu mwenye shida ya maji kuwa msiichague CCM ili muwe na Uhuru wa kuongea. Hakuna namna...... Narudia Hakuna namna mtu ambaye Hana Barabara au umeme anaweza akaingia Mkataba na Mtu ambaye hajui Kama atashinda.

Kwa maana hiyo hizi Kura Milioni nne ambazo JPM anazitafuta huko Site zilishatosha labda Kama anataka kushinda kwa kishindo. Hifadhini hii post tutakuja kutafuta asilimia za Ushindi baadaye.

Hima hima wanaccm tengenezeni network ya Kutoka kwa pamoja kwenda kupiga Kura tarehe 28. Mwana CCM usiache kupiga kura, nenda kapige kura.

Ole Mushi
0712702602
 
Back
Top Bottom