CCM ni chama cha ukoo wa watu fulani, kama si mwanaukoo usijichanganye

wazagamba nkoko

JF-Expert Member
Nov 23, 2021
392
998
Ile dhana ya ccm ni chama cha wakulima na wafanyakazi ,na ya kwamba ni taasisi ruksa kwa mtanzania yoyote kujiunga na kugombea nafasi ya uongozi imetoweka na Nyerere.

Ili taka kurudi kwa hayati Magufuli kwa sasa imeshindikana. Lazima ufahamike na huo ukoo ,kadhalika nguvu zako kiuchumi ndio zitakazokuwezesha Kupata nafasi ya uongozi chamani na serikalini.

Shime,kama si mwanaukoo wewe ndani ya chama hicho ni msindikizaji na mpiga vigelegele.

Karibuni chama kipya makini mbadala wa ccm na vyama pinzani mamluki .

Tumedhamiria kuwakomboa watanzania dhidi ya huu ubwanyeynye unaoendelea nchini
 
How ? Au mpaka kwanza mpewe Kula muwezeshe kushiba na mkisaza ndio mwananchi apate makombo
 
Mkuu hata kama ni njaa basi ya kwako imezidi, ndo maana uzi wako unaogopwa kuchangiwa hata na wachumia tumbo wenzako. Ebu kuwa fair na uweke mawazo yako huru ili uje na mada yenye ukweli.

Hizi mada za kungoja kuandikiwa na kina Mnyika afu kukupa ww uje uandike humu zinawadhalilisheni wengi maana zinakunyima uhuru wa kuchangia lolote kutoka ktk kichwa chako zaidi ya kuandika yale tu yanayotoka ktk kichwa cha kina Mnyika nk. Fikiria vizuri muundo wa chadema afu uangalie na uchafu ulioandika kuhusu CCM.

Najua unalipwa kwa ujinga huu lkn usikubali malipo yakakufunga akili kiasi hiki. CCM kila baada ya miaka 5 au 10 wanabadilisha uongozi wa kitaifa kuanzia mwenyekiti taifa, makamu mwenyekiti taifa, katibu mkuu nk. Chadema kilianza na baba mkwe wa mwenyekiti wa sasa, na sasa kipo kwenye mikono ya mkwe wa muasisi wa chama kwa zaidi ya miaka 18, safu ya viongozi wa kitaifa ni ile ile wanabadilishana tu position.. katibu mkuu anakuwa makamu mara makamu anakuwa katibu mkuu nk.

Hakuna sura mpya ktk uongozi. Ila sikulaumu kwa vile najua na ww unapigania tumbo lako na familia yako. Kama kila uzi mnalipwa buku tano tano na data za buku kwanini na ww usiandike chochote ili ulipwe kama wenzako!!

images (25).jpeg
 
Ile dhana ya ccm ni chama cha wakulima na wafanyakazi ,na ya kwamba ni taasisi ruksa kwa mtanzania yoyote kujiunga na kugombea nafasi ya uongozi imetoweka na Nyerere...
Orodhesha majina ya familia za vigogo walioshika madaraka utaeleweka zaidi, otherwise itakuwa kama ni majungu.
 
Back
Top Bottom