CCM ni chaka la wezi, majangili na mafisadi

Kazimzubwee

Member
Nov 7, 2016
51
57
Amani iwe nanyi, kweli CCM ni sikio la kufa, ujangili CCM, Lugumi CCM, Escrow, Meremeta Kagoda, vitambulisho feki vya taifa, Faru John, huu wizi wote unafanyika chini ya baraka za vigogo wa CCM na wanajuana na kulindana. Mkuu wa kaya amekuwa hodari wa kutumbua vipele majipu anayaogopa eti hataki kufukua makaburi atashindwa kuyafukia; kauli hii inathibitisha CCM wote ni wezi na mafisadi.

Ningependa jipu la Lugumu na sakata la fedha za Tegeta Escrow limulikwe, mkuu anapata kigugumizi gani? Anaogopa atakivua nguo chama chake? Mbona serikali hii chini ya CCM inafanya kazi kwa magengeza, ina maana kweli Tanzania ni shamba la bibi halina mwenyewe? Inasikitisha kuona hata serikali hii nayi inalinda wezi kisa ni vigogo wa CCM.
 
>>>>Chadema wamekuwa kama popo, hawajulikani ni ndege ama ni mnyama...

Chadema kitaaminika baada ya kuachana na kubadili gia angani....



Hivi Ben Saanane mmeshamtoa mlikomficha??
 
Kama mtu kupendekeza tu kuongeza bei ya umeme anatumbuliwa, inashindikana vipi kuwatumbua wahusika wa Lugumi, Escrow, Kagoda, Meremeta, n.k? au haya ndo makaburi anayoyagwaya malaika wa Tanzania?
 
Back
Top Bottom