CCM Nguvu zako na jeuri yako imepimwa na sasa Utawala wako Utaondolewa kwako. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Nguvu zako na jeuri yako imepimwa na sasa Utawala wako Utaondolewa kwako.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by majata, Mar 13, 2011.

 1. majata

  majata JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Hivi ni Mtanzania gani asiye penda haya?

  1. Makazi bora.
  2. Afya bora
  3. Elimu bora

  Nnaimani kila mtanzania hicho ndicho akipendacho, CCM ilipewa muda wa miaka50 itimize hayo, lakini ukweli walio fikia angalau nusu ya hapo ni chini ya asilimia 20, Raia wengi bado wanaishi kwa umasikini mkubwa wengine wanakufa kwa kukosa huduma bora za afya Malaria ugonjwa unaozuilika ndio umekuwa kama mpunguza watu wa kitaifa.

  Swali:
  Je! ninani anaweza kuiongoza serikali yetu kwa ufanisi?


  Kama CCM waliokaa wikiongoza serikali iliyobarikiwa kwa utajiri wa ardhi nzuri yenye rutuba, madini yakila aina, nchi yenye kuvutia watalii wa kila aina, nchi yenye mito mingi mikubwa, nchi yenye pwani yenye samaki wengi kutoka Tanga mpaka Mtwara na pwani nzuri kwa usafirishaji, nchi ambayo uoto wake wa asili haujaharibiwa bado nchi ambayo wakoloni waliigombania kulingana na uwepo wake kijiografia, Nchi yenye maziwa mengi nadhani kuliko zote afrika hata ukiangalia ramani ya afrika hata kama mipaka ya nchi haijaonyeshwa unaweza kuiona kwa kuangalia maziwa yake mengi yakiwa mipakani, nchi yenye mlima mrefu kupita yote afrika, nchi yenye rasili mali watu ya kutosha, Kwa miaka 50 sasa bado wanaendelea kutaka kututawala wakati bado maisha yetu ni magumu sana, ccm wamefanyia mambo maovu mengi nchi yetu na kuiacha nchi yetu ikijenga matabaka makubwa sana kati ya matajiri na masikini, viongozi wameacha sera za mwalimu nyerere za kuhakikisha haki sawa katika kugawana rasilimali za taifa.

  Je unajua utajiri wa viongozi hawa?

  1. JK
  2. RA
  3. BwM
  4. EL
  5. Mama A mkapa.
  Hao ni wachache tu nimatajiri sana, wamepata wapi mali zote walizonazo?. kwanini ni viongozi tu?


  Watanzania wenzangu popote mlipo hapa nchini au popote Duniani Tuamini kwamba CCM nguvu zake zimishapimwa kwa miaka 50 na sasa utawala wake uondoshwe kutoka mikononi mwake kwani kazi ya ccm haikuwa kuwanufaisha vigogo pekee ambao wengi wamepata maisha bora kwa kuwadhulumu raia wa tanzania, kazi ambayo sio wananchi walioituma ifanye, Tuiombee CCM iondoke na tuikatae sisi wote kwani ndio mchawi wa maendeleo yetu, lasivyo ifumuliwe yote upya kabisa ili iaminiwe tena.
   
Loading...