CCM ndio wanaobebana kifamilia. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM ndio wanaobebana kifamilia.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanza Madaso, Sep 18, 2009.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mbowe: CCM ndio wanaobebana kifamilia

  [​IMG]
  Mwandishi Wetu​
  Septemba 16, 2009[​IMG]
  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema tuhuma za ukabila na ubadhirifu wa ruzuku zinazoelekezwa kwake na kwa chama zinatangazwa kwa makusudi na chama tawala, Chama cha Mapinduzi (CCM).
  Amesema CCM hakina uhalali wa kuyatangaza mambo kama hayo kwa vile chenyewe kina viongozi wengi waandamizi wa kutoka familia moja, kinapokea ruzuku ya zaidi ya Sh. bilioni moja kila mwezi, fedha ambazo wanachama wake hawajui zinatumikaje.
  Kwa muda mrefu, shutuma hizo zinazoelekezwa CHADEMA zimekuwa zikiibuliwa na kushabikiwa na baadhi ya wanasiasa wakiwamo wa CCM kama ilivyojitokeza wakati wa chaguzi ndogo za ubunge katika Majimbo ya Busanda, Biharamulo na Tarime.
  Lakini akizungumza katika mahojiano maalumu na Raia Mwema wiki iliyopita, yaliyochapishwa katika kurasa za kati za toleo hili, Mbowe alisema:
  “Niseme tu kwamba, ruzuku ni asilimia 50 tu ya fedha za kuendesha chama. Zilizobaki tunachangia sisi viongozi. Watanzania waelewe viongozi wa CHADEMA tunajitolea, hatulipwi mshahara. Tunajitolea rasilimali zetu na muda wetu.
  [​IMG]

  MWENYEKITI wa CHADEMA, Freeman Mbowe
  “Chama kinapata ruzuku ya milioni 65, lakini CCM wanaozusha hayo, wanapata ruzuku ya Sh bilioni mbili. Hawazungumzii hizi. Jambo jingine, mimi kama mwenyekiti wa chama ningestahili kupata malipo, mshahara, nyumba, mafuta ya gari, simu, walinzi, lakini hizo zote chama hakinilipii na ukienda CHADEMA hutakuta vocha yoyote kuhusu Mwenyekiti kuchukua pesa.’’
  Alisema Kamati Kuu ya chama hicho iliagiza sekretariati taifa itoe malipo ya sh milioni tano kila mwezi kwa ajili ya mwenyekiti lakini amekuwa hachukui fedha hizo ili kutoa fursa zitumike kuendesha shughuli nyingine.
  Alisema Mbowe: “Shutuma za kula ruzuku naamini ni uwendawazimu. Kwenye vikao vyetu vya chama bajeti inapelekwa kwenye Kamati Kuu ya watu 34 makini. Wapo Bob Makani, Balozi Ngaiza, Edwin Mtei, Profesa Mwesiga Baregu, wapo mawakili, wenyeviti wa mikoa, wabunge kama akina mzee Arfi na Ndesamburo, wote hawa watakuwa wanaangalia tu hela za chama zinaliwa? Mwenyekiti hahusiki na masuala ya fedha, anayesimamia ni Katibu Mkuu,” alisema.
  Akizungumzia shutuma kuwa CHADEMA ni chama chenye kukumbatia ukabila (hasa kabila la Wachaga) kutokana na nafasi za uongozi kushikwa na watu wenye nasaba moja, na hasa yeye akitazamwa uhusiano wake na muasisi Edwin Mtei ambaye ni mkwewe, na viongozi wengine kama Mbunge wa Moshi Mjini Philemon Ndesamburo ambaye binti yake Lucy Owenya ni mbunge wa Viti Maalumu, Mbowe alisema uhusiano kati ya mtu na mtu haumpotezei mtu sifa ya kuchagua au kuchaguliwa na wenzake kama ana uwezo husika.
  “ Kila Mtanzania ana haki zake binafsi za kikatiba. Kila mtu ana haki ya kuwa mgombea lakini watu hawa wanapozungumza hivi ni watu wa CCM hawazungumzi ndani ya chama chao kuna nini.
  “Malecela (John Malecela, Mbunge wa Mtera na makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM) na mkewe (Anne Kilango Malecela, Mbunge wa Same Mashariki) ni wabunge kwa hiyo tuite CCM ni chama cha Malecela? Sitta (Spika Samuel Sitta) na mkewe (Margaret Sitta) ni wabunge, mmoja ni Spika, mwingine ni Waziri.
  “Msekwa (Pius Msekwa, spika msitaafu sasa Makamu Mwenyekiti wa CCM) alikuwa Spika na mkewe (Anna Abdallah) Waziri. Dk. Abdalah Kigoda ni Mbunge na dada yake (Dk. Aisha Kigoda – Khatib, Naibu Waziri wa Afya na mke wa Muhammed Seif Khatib, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais) ni mbunge.
  “Shelukindo (William) na mkewe (Beatrice) ni wabunge. Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, mwanawe Makongoro Nyerere ni Mwenyekiti wa Mkoa anakotoka Nyerere.
  “Vita Kawawa (mtoto wa Rashidi Kawawa, mkongwe wa siasa nchini aliyepata kushika vyeo vingi serikalini na chama tawala) yuko bungeni. Ridhiwani (mtoto wa Rais Kikwete), Mama Salma Kikwete na Rais Jakaya Kikwete mwenyewe wapo CCM.
  “Sasa huwezi kuwanyima watu hawa uhuru wao wa kisiasa kwa sababu eti ni wanafamilia au wanandoa. Kila mmoja ana haki ya kugombea, hata wana-CCM mimi siwalalamikii”.
  Alisema kwenye Kamati Kuu iliyopita kulikuwa na Wachaga wanne kati ya wajumbe 34 ambao ni yeye, mkwewe mzee Mtei anayeingia kama mwanzilishi na mwenyekiti mstaafu, Ndesamburo aliyeingia na kofia yake kama Mwenyekiti wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa upande wa chama, Grace Kiwelu akiwakilisha wabunge kwa sababu wabunge wa CHADEMA wanawakilishwa kwenye Kamati Kuu.


  Source: Raiamwema

  Maoni yangu: Hapo pekundu pamekata mzizi wa fitina.Walisema
  sana hapo Mbowe amenena
  [​IMG]
   
 2. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Nadhani si vema Mbowe kujiingiza kwenye siasa hizi, yeye aendeleze siasa zilizokomaa. Amefanya vizuri kujibu shutma mbalimbali ila hili la kubebana kwa CCM aachane nalo awaachie wakurugenzi wa chama.
   
 3. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hapa nitakupinga kidogo, kafanya vizuri kujibu kwani shutuma zote alikuwa anatupiwa yeye.
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  nadhani kama ni ukabila, rushwa, wizi vimejaa CCM
   
Loading...