Ccm naombeni mnishawishi niwachague tena 2015

Ccm naombeni mnishawishi niwachague tena 2015

Njaa Mbaya

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2012
Posts
666
Reaction score
178
Tarehe 23 August 2015, CCM wanazindua kampeni za kuomba ridhaa ya watanzania kuongaza nchi kwa miaka mitano huku wakiwa wameisha ongoza nchi kwa zaidi ya miaka hamsini. Nikiwa mtanzania ambaye natarajia kuwa miongoni mwa wapiga kura ifikapo october 25.
Nitaipigia kura CCM ikiwa tu:
-Wataniambia kwa nini wameshindwa kumshitaki lowasa huku wakiwa wanajua ni fisadi na ushaidi wanao badala yake wanakuja kulialia kwa wananchi. Hivyo siku ya uzinduzi sitaki kusikia eti EL ni fisadi nataka sababu za kunishawishi kwa nini hajashitakiwa huku wakiwa wao ndiyo wanaongoza dola
-Siku hiyo nataka kusikia kwa nini hadi leo zaidi ya miaka hamsini nakunywa maji machafu hadi naugua kipindupindu
-Nataka kusikia kwa nini natumia masaa sita kwenda kazini hapa dar huku nilihaidiwa foleni itakuwa historia mwaka 2010 nikaichagua CCM nini kimeshindikana hadi bado nateseka na foleni
-Nataka kusikia kwa nini wanafunzi wanakaa chini baada ya miaka hamsini ya uhuru huku wakimaliza darasa la saba wengi wao hawjiua kusoma na kuandika
-Nataka kusikia kwa nini baba yangu kijijini anakopwa mazao yake
-Nataka kusikia kwa nini tembo wetu wanaangamia huku meno yakipitishwa bandarini na viwanja vya ndege vyenye ulinzi madhubuti ambapo mimi nikiwa tu na perfume nazuiliwa ila meno ya tembo yanapita
Nijibu haya na mengine mengi.

Siku hiyo ya uzinduzi nataka kusikia pia kwa nini ile meli kule kwetu kagera haijanunuliwa hadi meli mbovu imetaka tena kufanya msiba mkubwa.
Sitegemei siku hiyo kusikia eti EL ni mgonjwa, ohooo wapinzani wataisoma namba, tutashinda kwa goli la mkono.

Nataka nipate majibu ya mambo ambayo kwa miaka hamsini CCM imeshindwa na nini kilisababisha kushindwa na pia mipango gani mnayokuja nayo kuhakikisha sasa yanatekelezeka. Mkinishawishi nitabadili msimamo wangu wa kupiga kura yangu kwa EL.
 
Zimekuwepo sababu kadhaa ambazo watu kadhaa wamejaribu
kuziweka hapa wakionyesha ndio chanzo cha watu kufurika
kuhudhuria uwepo wa Lowassa mahali fulani baada ya kutangaza
kujiunga na UKAWA/CHADEMA.
Ni kuwa kabla palikuwepo na kukata tamaa kwa kiwango kikubwa
kwa Watanzania kuelekea ndoto yao ya kuiondoa ccm katika
kutawala. Watanzania waliivumilia ccm kuwa inaweza kufanya
mabadiliko yake ya ndani ambayo yangeweza kuleta maisha bora
kwa Watanzania. Kusubiri kwa mabadiliko haya kumekuwa siku
zote hakufanyiki na sana sana kinachofanyika ni kuimarisha
mfumo ambao muda mrefu sana Watanzania waliisha ukinai. Mtu
anazaliwa katika mfumo huo unao mpatia umaskini hadi anazeeka
katika huo mfumo.Watanzania walifika mahali wakajiimanisha
kuwa sio rahisi kuiondoa ccm katika utaratibu huu wa kupiga kura.
Katika utaratibu huu wa amri na kanuni za Demokrasia za ccm
ambazo zimekaa kisanii. Kujua kuwa waliisha kata tamaa
Watanzania wengi wamekuwa hawaoni sababu hata ya kwenda
kupiga kura kwa muda mrefu sasa. Mfano ni mwaka 2010, walio
piga kura ni chini ya nusu ya waliokuwa wamejiandikisha.
Watanzania ni wapenda amani. Amani ya Watanzania ilikuwepo
hata kabla ya Uhuru. Mkoloni aliwakuta Watanganyika wakiwa na
amani kiasi cha kuwatia bakora huku wakiwa kimya. Hivyo
Watanganyika/Watanzania wanahitaji fulsa ili wafanye mabadiliko
ya amani na si rahisi wakalazimisha mabadiliko kwa kutumia
siraha hata uwe umewaonea kwa kiasi gani.
Mwaka 1995 wakati Mrema alipojitokeza Watanzania waliona ni
fulsa ya pekee ya kuiondoa ccm. Kwa namna ccm ilivyofanya
hakuna anayeelewa kilichitokea na kila mmoja alibaki na sababu
zake. Hata mwaka 2010 mambo yalikuwa hivyo hivyo.
Sasa ni kuwa ametokea Lowassa. Watanzania wanaona hii ni fulsa
nyingine ya kutimiza ndoto zao.
Kinacho waaminisha kuwa ndoto yao sasa inaenda kutimia ni:
1. Nyerere alisema atakaye yaleta mabadiliko ambayo Watanzania
watakuwa wanayataka atatoka ccm.
2. Watanzania wanaamini Lowassa atakuwa anajua siri ambazo
ccm huwa wanatumia kuvuka kizingiti cha kukataliwa na wapiga
kura lakini bado ikaonekana wameshinda. Watanzania wana imani
kuwa iko siri ya ushindi tofauti na kura zinazopigwa
3. Watanzania wengine hudhani huwa kuna kuzidiwa kifedha kitu
ambacho Wapinzani huwa hawana sasa wanatumaini hili Lowassa
atalitatua maana nyuma ameonyesha kuweza ktk harambee
kadhaa.
4. Mikakakati mingi ya kushinda aliyo nayo Lowassa.
Sasa ukichanganya na kiwango ambacho Cdm wamefikia, kiwango
ambacho CDM ilihamasisha watu kujiandikisha, Watanzania
wamepata shauku ya kuyaona mabadiliko.
Ndani ya shauku hii Watanzania huwezi kuwambia chochote.
Hakuna propaganda itakayobadili mwelekeo. Sasa mafuriko
hayajaonekana subiri Kampaini zianze.
Natabiri mwaka huu pia kutakuwepo na mafuriko ya wapiga kura
kujitokeza kwenye kupiga kura.
 
Tarehe 23 August 2015, CCM wanazindua kampeni za kuomba ridhaa ya watanzania kuongaza nchi kwa miaka mitano huku wakiwa wameisha ongoza nchi kwa zaidi ya miaka hamsini. Nikiwa mtanzania ambaye natarajia kuwa miongoni mwa wapiga kura ifikapo october 25.
Nitaipigia kura CCM ikiwa tu:
-Wataniambia kwa nini wameshindwa kumshitaki lowasa huku wakiwa wanajua ni fisadi na ushaidi wanao badala yake wanakuja kulialia kwa wananchi. Hivyo siku ya uzinduzi sitaki kusikia eti EL ni fisadi nataka sababu za kunishawishi kwa nini hajashitakiwa huku wakiwa wao ndiyo wanaongoza dola
-Siku hiyo nataka kusikia kwa nini hadi leo zaidi ya miaka hamsini nakunywa maji machafu hadi naugua kipindupindu
-Nataka kusikia kwa nini natumia masaa sita kwenda kazini hapa dar huku nilihaidiwa foleni itakuwa historia mwaka 2010 nikaichagua CCM nini kimeshindikana hadi bado nateseka na foleni
-Nataka kusikia kwa nini wanafunzi wanakaa chini baada ya miaka hamsini ya uhuru huku wakimaliza darasa la saba wengi wao hawjiua kusoma na kuandika
-Nataka kusikia kwa nini baba yangu kijijini anakopwa mazao yake
-Nataka kusikia kwa nini tembo wetu wanaangamia huku meno yakipitishwa bandarini na viwanja vya ndege vyenye ulinzi madhubuti ambapo mimi nikiwa tu na perfume nazuiliwa ila meno ya tembo yanapita
Nijibu haya na mengine mengi.

Siku hiyo ya uzinduzi nataka kusikia pia kwa nini ile meli kule kwetu kagera haijanunuliwa hadi meli mbovu imetaka tena kufanya msiba mkubwa.
Sitegemei siku hiyo kusikia eti EL ni mgonjwa, ohooo wapinzani wataisoma namba, tutashinda kwa goli la mkono.

Nataka nipate majibu ya mambo ambayo kwa miaka hamsini CCM imeshindwa na nini kilisababisha kushindwa na pia mipango gani mnayokuja nayo kuhakikisha sasa yanatekelezeka. Mkinishawishi nitabadili msimamo wangu wa kupiga kura yangu kwa EL.

Hvi kwa kuwaangalia na unavyowafaham hao ccm unatarajia wajibu maswali mazito hvi yanayomgusa mwananchi moja kwa moja? Watakachokuambia sana sana kwa miaka50 tumeunganisha mikoa yote kwa Lami.
 
Mfn. Ata ungekuwa ww mwenyewe ndo kiongoz mkuu wa ccm UNGEJIBUJE? Jumba bovu wamemtupia Mapombe na kumbebesha gunia la Mavi ambalo limechanganywa na Misumali namuonea huruma ndo maana anaishia kuiba ALIMSELEMA ....
 
Back
Top Bottom