CCM na watumishi wa umma

 
du, kwa heri...naona nabishana na msukule wa Lumumba.
Huo uzi haukuzungumzia Lugumi unataka kubadili thread content kibiafra fulan! Msukule? Ha haa acha hasira kiongozi
 
Unawaita watumishi malofa? Wewe ni mse... nge maana hukuwaajiri wewe
 
Kwahali hii itafika kipindi tutaambiwa ukitaka kuajiliwa ni lazima uwe na kadi ya ccm.
Not only kuajiriwa hata kuishi TZ inabidi uwe na kadi ya CCM hapo ndipo siasa inapohatarisha usalama wa nchi kwa sababu kama kigezo kimojawapo kitakuwa ni kadi ya uanachama basi hata wasomali, wanyarwanda, wakenya watakuwa na kadi za CCM na wataingia kichama kwenye kazi za serikali.
 
Kwahali hii itafika kipindi tutaambiwa ukitaka kuajiliwa ni lazima uwe na kadi ya ccm.
Not only kuajiriwa hata kuishi TZ inabidi uwe na kadi ya CCM hapo ndipo siasa inapohatarisha usalama wa nchi kwa sababu kama kigezo kimojawapo kitakuwa ni kadi ya uanachama basi hata wasomali, wanyarwanda, wakenya watakuwa na kadi za CCM na wataingia kichama kwenye kazi za serikali.
 
Tumia vikao kukosoa au andika write up wasilisha katika menejimenti ya taasisi ya umma uliyipo.
Upo kwenye gari, watu wanalalamikia huduma mbovu za taasisi za serikali, na wewe unajua kuwa haki ni mbaya. Utateteaje wakati huo kama sio unafiki?
Au hukumwelewa mleta mada?
utaratibu wa kukosoana kiofisi upo, na wakati mwingine huwa haufuatiliwi. Mifano hata wewe unayo.
 
Naona taratibu tunaanza kurudi kwenye zama za chama kushika hatamu! Ni ujinga wa hali ya juu kudhani mtumishi wa umma ni mtumishi wa CCM; ni kushindwa kutofautisha kati ya chama na dola!
 
Mimi ni mtumishi wa umma na siyo mtumishi wa CCM, sikuajiriwa na CCM na wala silipwi na CCM, siwajibiki kwa CCM. Anayedhani ninapaswa kuwa mtumishi wa CCM ajitafakari upya
 
Watu wanakosoa serikali kwenye vikao halali vya serikali wanabatizwa jina la "mpinzani" kinachofata hapo ni kukupiga nje ama kukuhamisha kituo!!!!
 
Hata nikiwa mtumishi wa umma cwez kuitetea ccm,ukiwa mtumishi wa umma cjaona katika mkataba haipo ccm,nitafuata wajibu wangu wa kaz wala cjawah kuona ama kusoma ilani ya ccm.Nina wasiwas kama rais anauelewa utumishi wa umma vzr.
 


Na hata mshahara ukichelewa we tetea serikali tu....
 
Thread inaanza kwakutukana
Dah mods mods mpige ban
Akitukana watu watachangiaje
Aibu si kitu kikubwa tuchutame Tu
 

Watumishi wa umma huwa wanafanya kazi kwa circulars-hatusomi ilani ya chama chochote kiofisi na hata tunapoajiriwa hatupewi ilani ya chama hivyo wengi hawaijui ukiacha labda wanachama wa chama hicho na wale wanao chaguliwa kazi zenye ukada (ambao tuliona vitendea kazi vyao ni pamoja na ilani ya chama tawala). Yaliyomo kwenye ilani kuna wanaopewa majukumu kuyaingiza kwenye sera na program za serikali ambazo hutekelezwa na wafanyi kazi wa umma. Na kawaida hakuna sera ambayo ni 100% kamili-hivyo kawaida kuna kutafsiri sera inataka nini na hapo tena kuna weza kuwa na mawazo gongana.
Ukianza kufikiria kama unatekeleza sera ya CCM ndio unaweza kuishia kufanya yale usiotegemewa kuyafanya. Wafanya kazi wa umma hutekeleza sera za serikali na ndio wanachotakiwa kuona wanafanya full stop. Kesho ikiingia serikali chini ya chama kingine mtizamo unakuwa hivyo hivyo. Wale ambao hubadilisha ilani kuwa sera ya serikali na kuhahakikisha hilo linafanyika kukija serikali inayo ongozwa na chama kingine wao huachia ngazi au kutolewa ili wengine wahakikishe uingizaji wa sera za chama kipya.
 
Umesema vyema ila nikukumbushe kuwa Tanganyika ilikombolewa chini ya TANU. Ni chama hicho ndicho kilichounda Serikali.

Chama chochote kabla ya kusajiliwa lazima kiwe na Katiba yake katiba ambayo itasaidia kuunda chombo (Serikali) cha utekelezaji wa ilani yake.

Sasa sidhani kama Serikali itakayoundwa kwa maslahi ya chama tawala itaajiri watumishi wanaokinzana kimtizamo/kisera completelly ila inaweza ajiri watumishi neutral.

Kama kitaajiri watumishi wenye fikira za chama kingine lazima serikali hiyo itakuja kuanguka tu kama isipoanguka basi itayumba mno kiutendaji.

Circular zote ni tool ndani ya Serikali ya chama tawala ili kuwalazimisha watumishi wasitoke nje ya misingi ya utumishi.

Ndo maana kama utakumbuka miaka ya kuelekea uchaguzi lazima kuwepo na circular principally za kuwabana watumishi wasije kuigeuka Serikali na kuiangusha. Mf. Uchaguzi uliopita watumishi waliwekewa waraka wa kuwabana wasijihusishe na siasa baada ya kuona idadi fulan ya watumishi walikuwa washabiki wa vyama pinzani. Can you think a bit- kuwa unadhani waiotunga huo waraka ni akina nani (Ndio mipango mizima ya chama tawala) kama hujui.

Hata kama hupewi ilani ya CHAMA kwenye kazi zako za utumishi wa UMMA kiongozi yaani msimamizi wako wa kazi anayo. Mwisho wa mwaka wa fedha wowote lazima taasisi za UMMA zitoe taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Kati ya vyama vya upinzani kipo kimoja kinaamini katika utawala wa MAJIMBO kwa hiyo pindi kikishika dola lazima Katiba ya JMT itabadiishwa ili kukidhi matakwa ya chama hicho hii iko wazi haihitaji Phd. Ndo maana CCM wakati wamchakato wa mabadiliko ya Katiba walitetea kulingana na wao wanachotaka (kwa kuwa wao ni wengi- Watanzania ndio reflection).

Niseme tu kuwa kwa sasa vyama vya upinzani vimeanza kukua huenda baadae WAAJIRIWA wa serikali watachunguzwa hata ushabiki wao kisiasa. Tumeona kwenye ngazi za juu karibu wateule wengi ni waumini wa sera za ruling party.

Bado nawaza kingine....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…