CCM na watumishi wa umma

CCM na watumishi wa umma

SHIKAMOOO MAGUFULI.

Nchi imeanza kurudi kwenye misingi yake.

Watumishi wa UMMA wote si vyema hata kidogo kutofautiana na ilan ya CCM ama kutokukubaliana na mtizamo wa RAIS.

kama wapo baadhi ni wale Malofa na mbumbumbu wasiotaka kukubali ukweli unaowazunguka.

Si busara kukaa kijiweni unakosoa utendaji kazi wa serikali wakati wewe ni mtumishi wa UMMA ambaye ni sehemu ya Serikali.

Kama kuna matatizo ama changamoto zinazokukwaza katika utekelezaji wa majukumu yako tumia vikao, weka mikakati ya utekelezaji na tumia vizuri hekima uliyopewa ili kuishauri serikali. Kuwa m-bunifu. Acha kukaa kijiweni ili uonekane mzunguzaji kwa kukosoa serikali.

Endapo kijiweni kwako imetokea watu wanakosoa serikali, ni wajibu wako kuitetea serikali kwa nguvu zote maana mtumishi wa UMMA ni sehemu ya Serikali ya CCM.

Kinachonikera ni pale ninapowasikia watumishi wa UMMA wamekazania kuikosoa serikali wakati wananchi wanapokuwa wanailalamikia serikali kwa kutowapatia huduma fulani. Mara nyingine huenda inatokea kati ya huduma inayolalamikiwa mtumishi wa UMMA huyo anakuwa ni sehemu ya watumishi wanaotakiwa kuelezea au kutetea utoaji huduma. Badala yake anajitoa ufahamu ( hapa ndo unajitwika ulofa au umbumbumbu) anaanza kuikandia serikali ya CCM.

Si bure mara nyingi watumishi ya jinsi hii ni wabadhilifu sana kwa mali za UMMA. hupenda kutumia kivuli cha kuilaumu serikali ya CCM ili kuwapofusha wananchi wasitambue wizi wao.

Ubovu wa Serikali ya Ccm unachangiwa na mtumishi mmoja mmoja siyo "lumpsum" wa ngazi zote kuanzia kitongoji hadi Ikulu ama kuanzia Ikulu hadi kitongoji. Kwa hiyo unapopindisha utaratibu wa utoaji huduma fulani unakuwa wewe ni msingi wa kulaumiwa kwa Serikali ya CCM.

Na watumishi wa UMMA wachache wanaofanya kazi katika misingi ya utaratibu wanakuwa wao ni sehemu kubwa ya mafanikio ya serikali ya CCM.

kuitete serikali ya ccm unaitaji uwe na akili za maiti haka kama ni mtumishi wa umma
 
Umesema vyema ila nikukumbushe kuwa Tanganyika ilikombolewa chini ya TANU. Ni chama hicho ndicho kilichounda Serikali.

Chama chochote kabla ya kusajiliwa lazima kiwe na Katiba yake katiba ambayo itasaidia kuunda chombo (Serikali) cha utekelezaji wa ilani yake.

Sasa sidhani kama Serikali itakayoundwa kwa maslahi ya chama tawala itaajiri watumishi wanaokinzana kimtizamo/kisera completelly ila inaweza ajiri watumishi neutral.

Kama kitaajiri watumishi wenye fikira za chama kingine lazima serikali hiyo itakuja kuanguka tu kama isipoanguka basi itayumba mno kiutendaji.

Circular zote ni tool ndani ya Serikali ya chama tawala ili kuwalazimisha watumishi wasitoke nje ya misingi ya utumishi.

Ndo maana kama utakumbuka miaka ya kuelekea uchaguzi lazima kuwepo na circular principally za kuwabana watumishi wasije kuigeuka Serikali na kuiangusha. Mf. Uchaguzi uliopita watumishi waliwekewa waraka wa kuwabana wasijihusishe na siasa baada ya kuona idadi fulan ya watumishi walikuwa washabiki wa vyama pinzani. Can you think a bit- kuwa unadhani waiotunga huo waraka ni akina nani (Ndio mipango mizima ya chama tawala) kama hujui.

Hata kama hupewi ilani ya CHAMA kwenye kazi zako za utumishi wa UMMA kiongozi yaani msimamizi wako wa kazi anayo. Mwisho wa mwaka wa fedha wowote lazima taasisi za UMMA zitoe taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Kati ya vyama vya upinzani kipo kimoja kinaamini katika utawala wa MAJIMBO kwa hiyo pindi kikishika dola lazima Katiba ya JMT itabadiishwa ili kukidhi matakwa ya chama hicho hii iko wazi haihitaji Phd. Ndo maana CCM wakati wamchakato wa mabadiliko ya Katiba walitetea kulingana na wao wanachotaka (kwa kuwa wao ni wengi- Watanzania ndio reflection).

Niseme tu kuwa kwa sasa vyama vya upinzani vimeanza kukua huenda baadae WAAJIRIWA wa serikali watachunguzwa hata ushabiki wao kisiasa. Tumeona kwenye ngazi za juu karibu wateule wengi ni waumini wa sera za ruling party.

Bado nawaza kingine....
Nafikiri tukubaliane kutokubaliana kwa hili. Unacho-ongea kingekuwa na kilikuwa sawa enzi zile za chama kimeshika hatamu. Tulikuwa na matawi ya vyama ofisini hadi vyuo vikuu. Sidani kama mambo hayo yanatakiwa yawepo sasa. Kama CCM inayafanya jinsi ulivyo-eleza basi ni upofu wao. Ahsante.
 
Nafikiri tukubaliane kutokubaliana kwa hili. Unacho-ongea kingekuwa na kilikuwa sawa enzi zile za chama kimeshika hatamu. Tulikuwa na matawi ya vyama ofisini hadi vyuo vikuu. Sidani kama mambo hayo yanatakiwa yawepo sasa. Kama CCM inayafanya jinsi ulivyo-eleza basi ni upofu wao. Ahsante.
Dola ina raha yake hawapendi wanyang'anywe.
 
Aliyewadanganya kuwa ukiwa mwanachama wa chadema ndio kujitambua ni nani??

Tangu lini Chadema imekuwa kipimo cha mtu kujitambua??

Kweli chama ambacho kinabadilisha gia angani na kuuzwa hovyo , hakina hata ofisi kwa miaka 20 ,ndio kiwe kipimo cha MTU kujielewa??

Bavicha kuna haja ya kupima bongo zenu, huenda mnamtindio wa ubongo.
Kwa hiyo ccm ndio kipimo cha kujitambua
 
Mtu mwenye sifa kama hizi hakustahili kupewa hata ujumbe wa nyumba kumi kumi achilia mbali Urais, lakini fisadi Kikwete na fisadi Mkapa wakaweka mbele maslahi yao badala ya nchi kwa kutaka mtu ambaye ataendelea kulinda maovu yao waliyoyatenda walipokuwa madarakani.

Habari hii ilichapishwa kwenye gazeti la RAI miaka michache iliyopita ikisomeka...

Huyu Ndiye Pombe Magufuli:

- Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
- Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani

ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

“Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.


Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

“Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.


Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.


Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.


“Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

SALVA RWEYEMAMU
RAI
 
Aliyewadanganya kuwa ukiwa mwanachama wa chadema ndio kujitambua ni nani??

Tangu lini Chadema imekuwa kipimo cha mtu kujitambua??

Kweli chama ambacho kinabadilisha gia angani na kuuzwa hovyo , hakina hata ofisi kwa miaka 20 ,ndio kiwe kipimo cha MTU kujielewa??

Bavicha kuna haja ya kupima bongo zenu, huenda mnamtindio wa ubongo.
Unavojiona unadhani we mzima hapo ulipo..??
Kama bado hujawehuka mda si mrefu unaelekea huko.
 
Back
Top Bottom