CCM na wanachana wao huwa wanajiandikishia wapi??

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,507
wakati karibu nchi nzima watu wakilalamikia zoezi la uandikishaji huku vyama vya upinzani vikienda huku na kule kuwaimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kuna swali kubwa ambalo linaleta kigugumizi kikubwa kuhusu
ukimya wa ccm, serikali na viongozi wake ktk zoezi hili zima la uandikishaji.

nitaanza na mfano mzuri alioutoa hivi karibuni Prof.Lipumba kwamba kuna eneo kama sikosei Lindi au Mtwara kwy kijiji kimoja chenye wapiga kura 3000 tume iliweza kuandikisha watu mia tatu (300) tu ikaondoka hata baada ya kuombwa kuongeza muda pamoja na matatizo lukuki yaliyojitokeza sasa swali ambalo Mtanzania mwenzangu inabidi ujiulize ktk watu hao 300 ni wangapi wanachama wa ccm?? je kwa kuwa Lipumba alikuwa eneo hilo kuimiza watu pia kuna uwezekano watu hao wote au asilimia kubwa wakawa ukawa lakini ccm haionekani kuwa na wasiwasi wowote ule juu ya watu wachache kuandikishwa!!

ccm na viongozi hakuna anayeimiza suala la kujiandikisha wala kutoa kauli juu ya mateso wanayoyapata watanzania kwy zoezi zima la uandikishaji swali la kujiuliza je wanachama wao hawapo ktk kundi hili la matesoni au linaloshindwa kujiandisha kutokana na urasimu wa tume??? na kama wapo miongoni mwao kwanini ccm wala viongozi wao hawalalamiki??? uzembe na udhaifu mkubwa ulionyeshwa na NEC umekuwa ukikemewa na wapinzani tu ccm imekaa inaangalia pembeni wakati nao uzembe huo unaweza pia kuwaathiri wanachana wao kutojiandikisha. hili suala linaitaji uchunguzi makini bila mzaa.

je zile hisia kuwa ccm kwa kushirikiana na tume ya uchaguzi inaandikisha wanachama wa ccm usiku na mchana kwa kutumia data base ya ccm zinaweza kuwa na ukweli wowote na kuzirudisha kwa wanachama wao kupitia wajumbe wa nyumba kumi kumi?? Binafsi ninaanza kuipa habari ile uzito unaostaili kuwa inaweza kuwa na ukweli ndani yake na kama vyama vya upinzani vina umakini ili suala siyo la mchezo ni mtu mjinga tu anaweza kudharau habari ya ccm kujiweka mbali na zoezi la uandikishaji huku wakijua wazi kuwa ushindi wao ndipo utakapotoka na kitendo cha NEC kutoandikisha au kuandikisha watu wachache kinatishia uhai wao wa kubaki madarakani. nawapeni hii hint muanze kuifanyia kazi nako ni anzeni na jengo la STATISTICS chuo kikuu cha DSM ndiko mchezo huu mzima unaweza kuwa unafanyika na ya pili ni lazima muilazimishe tume kusema ni watu wangapi wamejiandikisha mpaka hivi sasa ili kulinganisha na hesabu zinazotoka vituoni bila hivyo wapinzani jiandaeni kuumizwa october.
 
Kati ya mambo na ushauri wa msingi hasa wakati huu hili ni LA kwanza.
Ni muhim ukawa kufikiri zaidi wakati huu kuliko nyakati zozote.

Uzembe Mdogo tu na upuuzaji wa habari hii maana yake hadi sasahivi ccyemu imepita bila kupingwa.
Amkeni makamanda.

Angalizo jingone ni kwenye mashine zinazoongezwa sasahivi ambazo hazikufanyiwa majaribio kama taratibu zilivyokuwa zinaelekeza juu ya mashine.
Lubuva na ccm kwa maksudi wamechelewesha mashone ili......
 
Ni aibu, viongozi wakuu, kufikiria, mbinu, za namna gani, utaendelea kukaa madarakani, hata kwa kupuuza haki ya mwananchi, kupata kiongozi mzuri, wao, hawana time na mtanzania, hohehahe, wenyewe, ni kuangalia tutapigaje dili, "Hata mzikiri uchi, ccm haita watoa kwenye umaskini"Juma Duni Haji, makamu mwenyekiti, CUF Taifa14 june 2015 Ubungo plaza juma pili.
 
CCM hawawezi kuwa na wasiwasi kwa kuwa hizo ni mbinu zao,wanapofanikiwa kwenye mbinu moja ndiyo wanakuwa busy kuandaa mbinu nyingine.
 
Viongozi wangu waupinzani naona wansubiri October 2015 waanze kulalamika.Hakuna hata siku moja nimemsikia hata mmoja kuwa wameamua kuipeleka TUME ya Mkude Simba mahakamani.Ninamsifu Lema kwa kuingilia kati hilo.
 
wananchi itabidi wadai haki yao(kwa namna yoyote) ya kujiandikisha kabla muda wa kampeni haujaanza...

ukawa mtetee ili
 
CCM hawawezi kuwa na wasiwasi kwa kuwa hizo ni mbinu zao,wanapofanikiwa kwenye mbinu moja ndiyo wanakuwa busy kuandaa mbinu nyingine.

Lakini wanajuaje kwamba kwa kuweka mizengwe hawata athiri na wapenzi wa chama chao?? Maana kwenye foleni na watu wao wanaonekana.
 
Habari hii ni kweli tupu na isipuuzwe na yeyote. Hata mikoa ambayo haijafikiwa na Tume mfano Dar tayari kuna watu huenda wameshaandikishwa. Hiii ni hatari kwa demokrasia ya nchi yetu, ni ukiukwaji mkubwa wa haki.

wakati karibu nchi nzima watu wakilalamikia zoezi la uandikishaji huku vyama vya upinzani vikienda huku na kule kuwaimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kuna swali kubwa ambalo linaleta kigugumizi kikubwa kuhusu
ukimya wa ccm, serikali na viongozi wake ktk zoezi hili zima la uandikishaji.

nitaanza na mfano mzuri alioutoa hivi karibuni Prof.Lipumba kwamba kuna eneo kama sikosei Lindi au Mtwara kwy kijiji kimoja chenye wapiga kura 3000 tume iliweza kuandikisha watu mia tatu (300) tu ikaondoka hata baada ya kuombwa kuongeza muda pamoja na matatizo lukuki yaliyojitokeza sasa swali ambalo Mtanzania mwenzangu inabidi ujiulize ktk watu hao 300 ni wangapi wanachama wa ccm?? je kwa kuwa Lipumba alikuwa eneo hilo kuimiza watu pia kuna uwezekano watu hao wote au asilimia kubwa wakawa ukawa lakini ccm haionekani kuwa na wasiwasi wowote ule juu ya watu wachache kuandikishwa!!

ccm na viongozi hakuna anayeimiza suala la kujiandikisha wala kutoa kauli juu ya mateso wanayoyapata watanzania kwy zoezi zima la uandikishaji swali la kujiuliza je wanachama wao hawapo ktk kundi hili la matesoni au linaloshindwa kujiandisha kutokana na urasimu wa tume??? na kama wapo miongoni mwao kwanini ccm wala viongozi wao hawalalamiki??? uzembe na udhaifu mkubwa ulionyeshwa na NEC umekuwa ukikemewa na wapinzani tu ccm imekaa inaangalia pembeni wakati nao uzembe huo unaweza pia kuwaathiri wanachana wao kutojiandikisha. hili suala linaitaji uchunguzi makini bila mzaa.

je zile hisia kuwa ccm kwa kushirikiana na tume ya uchaguzi inaandikisha wanachama wa ccm usiku na mchana kwa kutumia data base ya ccm zinaweza kuwa na ukweli wowote na kuzirudisha kwa wanachama wao kupitia wajumbe wa nyumba kumi kumi?? Binafsi ninaanza kuipa habari ile uzito unaostaili kuwa inaweza kuwa na ukweli ndani yake na kama vyama vya upinzani vina umakini ili suala siyo la mchezo ni mtu mjinga tu anaweza kudharau habari ya ccm kujiweka mbali na zoezi la uandikishaji huku wakijua wazi kuwa ushindi wao ndipo utakapotoka na kitendo cha NEC kutoandikisha au kuandikisha watu wachache kinatishia uhai wao wa kubaki madarakani. nawapeni hii hint muanze kuifanyia kazi nako ni anzeni na jengo la STATISTICS chuo kikuu cha DSM ndiko mchezo huu mzima unaweza kuwa unafanyika na ya pili ni lazima muilazimishe tume kusema ni watu wangapi wamejiandikisha mpaka hivi sasa ili kulinganisha na hesabu zinazotoka vituoni bila hivyo wapinzani jiandaeni kuumizwa october.
 
Fikra finyu sana...kama mnajua hakuna wana ccm walojiandikisha na niny mlishaapa kuchukua dola iwe usiku au mchana wasiwas wenu nini?? Mi nafikir ndo mfurah mtapita bwelele!! Poor chagadema at work
 
Back
Top Bottom