Hizo takwimu hutumika kujihalalishia wizi wa kura na wala si za kweliccm ccm hawa hawaaminiki hivi toka mwaka 1995 wao wanadai wana wanachama 5milion wana mahesabu watujuze hakuna ongozeko wala kupungua. ina maana hiki chama kimekuwa kama volkano iliyokufa, tunaomba watupe hesabu ya kweli isije ikawa wanahesabu kadi za watu waliokufa. kuna haja watu wa sensa waweke kipengele cha kuhesabu wanachama wa vyama vya siasa kwani tungejua mbivu na mbichi.
Hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, katika Sherehe za Kutimiza Miaka 34 ya Kuzaliwa kwa CCM Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Tarehe 05 Februari, 2011
CCM Oyee!
Kidumu Chama Cha Mapinduzi!
Ni ukweli ulio wazi, tena wa kujivunia, kwamba katika miaka 34 ya uhai wake, Chama chetu kimepata mafanikio makubwa. Kimeendela kukua na kimezidi kuimarika kwa kila hali. Wanachama wameongezeka sana na kufikia takriban milioni 5.7. Wanachama wake ni watu wenye umoja, mshikamano na ushirikiano wa hali ya juu pamoja na kuwepo kwa changamoto za hapa na pale kwa nyakati fulani fulani.
Source: CCM website
Wanachama wa ccm nikama wakaazi wa Vatican. wako 1000, akifa au kuhama mmoja anasajiliwa mwingine!
90% ya watz ni wanavijiji, huko vijijini 80% ni CCM, 20% vyama vya upinzania. Mijini 50% ni CCM na 50% vyama vya upinzani. HIVYO wananchama CCM jumla inafikia milioni 11, laki 3, na elfu 51 tu.