CCM na Rushwa: Uchaguzi CCM Mkoa Pwani wavunjwa kwa Rushwa.....

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Ajabu PCCB hawaoni haya mambo

Rushwa yavunja uchaguzi CCM Pwani Send to a friend
Wednesday, 17 October 2012 21:40

Na Julieth Ngarabali, Kibaha
TUHUMA za kushamiri kwa vitendo vya rushwa katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa CCM mkoani Pwani, jana vilimlazimisha mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo, Mwinshehe Mlao kuvunja mkutano huo.

Uchaguzi huo uliokuwa ufanyike kwenye Jengo la Mkuu wa Mkoa wa Pwani, uliahirishwa saa chache, kabla ya upigaji kura kuanza kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba baadhi ya wajumbe walikuwa wakitoa na kupokea rushwa ili kushawishi ushindi wa baadhi ya wagombea.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza aliwaeleza wajumbe hao kuwa amepata taarifa kutoka vyombo vya usalama kuwa uchaguzi huo umegubikwa na vitendo vinavyoashiria kuwapo na rushwa.

Akiahirisha mkutano huo jana, Mlao alisema amelazimika kusitisha uchaguzi huo hadi utakapotangazwa tena, kutokana na baadhi ya wajumbe kukidhalilisha chama kwa kujihusisha na rushwa.

“Kwa haya yaliyotokea lazima tuwasiliane na wenzetu makao makuu. Baada ya kusema haya natangaza kuahirisha kikao hadi tarehe ya uchaguzi itakapotangazwa tena,” alisema Mlao.

Akizungumza katika mkutano huo, Mahiza alilaani kitendo hicho akisema kuwa kimeidhalilisha CCM na ofisi yake.

Awali Mahiza alisema kuwa alipata taarifa kutoka kwa maofisa wa Takukuru kuhusu kuwapo kwa mazingira ya rushwa yanayofanywa na wajumbe wa mkutano huo na baadaye alifika katika ukumbi wa mkutano.

“Baada ya kupata taarifa kuhusu mazingira ya rushwa, nilitoka nje na kweli ukumbini sikukuta watu. Niliposhuka chini niliwakuta wajumbe wengi wakiwa wamesimama makundi. Sikujua na wala sikushuhudia nani aliyekuwa anatoa rushwa ila maofisa wangu wameliona hilo," alisema Mahiza.

Mkuu huyo wa mkoa aliendelea kusema, "Najua nitabeba lawama kubwa sana, nitatukanwa sana na baadhi yao, lakini hili sitalivumilia.”

Nafasi iliyodaiwa kuwa ndiyo iliyokuwa ina wagombea waliokuwa wakichuana vikali zaidi ni katibu wa uchumi ambayo wagombea wake ni, Imani Madega na Haji Abuu Jumaa.

Baada ya kuahirishwa kikao hicho, Mahiza alifanya kikao cha ndani na wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa (NEC) wa mkoa huo, Ridhiwan Kikwete na Rugemalila Lutatina.

Alipotakiwa kuzungumzia hali hiyo jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema, " Waseme wenyewe wa Pwani. Kama imetokea leo siwezi kupata taarifa leo."

Aliendelea kusema," Kama imetokea wataleta taarifa, zikifika tutakuwa na cha kuzungumza, lakini leo waache waseme wao kwanza."

HIVI KWELI TAKUKURU HAWAWAONI WATOAJI RUSHWA NA KUWAKAMATA???????
 
Nimekuja kugundua kuwa tuna maana tofati ya rushwa. Hiko wanachofanya CCM siyi definition sahihi ya rushwa mbele ya TAKUKURU, maana ni jana tu wamekanusha kuwa hakuna vitendo vyovyote vya rushwa kwenye hizi chaguzi za CCM zinazoendelea. Nafikiri kunahaja ya hiki chombo (TAKUKURU) kuundwa upya kama tuna nia njema na nchi hii.
 
umeisoma habari hii kabla ya
kuipost? maana takukuru ndio waliomtonya RC kuhusu uwepo wa rushwa

HIVI KWELI TAKUKURU HAWAWAONI WATOAJI RUSHWA NA
KUWAKAMATA???????
 
Ukitaka
kuiua ccm kirahisi itenganishe na rushwa.

mfumo wao ndo unachohea mambo hayo. takukuru tutawalaumu lakini hata
wakiwakamata watapeleka ushahidi gani mahakamani wakati mtoaji na
mpokeaji wote wameridhika?
 
sasa mkuu wa mkoa na mikutano ya CCM? katiba yetu nayo inahitaji mabadiliko mengi sana
 
nafasi ya uenezi mkoa inashindaniwa na madega(yule wa yanga)na mdogo wake ramadhani dau(yule wa nssf)madega alikuwa likely kushinda na pamoja na rushwa iliyomwagwa na dau mdogo lakini madega bado alikuwa juu hivyo mkutano ukavunjwa kibabe,..kama suala la rushwa hakuna uchaguzi wa ccm usiohusisha rushwa..ukumbi wa mkoa wametumia na kulipa hawalipagi,hii ni kawaida yao,sometimes hadi chakula wanapewa kwa fedha za serikali..i hate this country
 
Ajabu PCCB hawaoni haya mambo

Rushwa yavunja uchaguzi CCM Pwani Send to a friend
Wednesday, 17 October 2012 21:40

Na Julieth Ngarabali, Kibaha
TUHUMA za kushamiri kwa vitendo vya rushwa katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa CCM mkoani Pwani, jana vilimlazimisha mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo, Mwinshehe Mlao kuvunja mkutano huo.

Uchaguzi huo uliokuwa ufanyike kwenye Jengo la Mkuu wa Mkoa wa Pwani, uliahirishwa saa chache, kabla ya upigaji kura kuanza kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba baadhi ya wajumbe walikuwa wakitoa na kupokea rushwa ili kushawishi ushindi wa baadhi ya wagombea.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza aliwaeleza wajumbe hao kuwa amepata taarifa kutoka vyombo vya usalama kuwa uchaguzi huo umegubikwa na vitendo vinavyoashiria kuwapo na rushwa.

Akiahirisha mkutano huo jana, Mlao alisema amelazimika kusitisha uchaguzi huo hadi utakapotangazwa tena, kutokana na baadhi ya wajumbe kukidhalilisha chama kwa kujihusisha na rushwa.

"Kwa haya yaliyotokea lazima tuwasiliane na wenzetu makao makuu. Baada ya kusema haya natangaza kuahirisha kikao hadi tarehe ya uchaguzi itakapotangazwa tena," alisema Mlao.

Akizungumza katika mkutano huo, Mahiza alilaani kitendo hicho akisema kuwa kimeidhalilisha CCM na ofisi yake.

Awali Mahiza alisema kuwa alipata taarifa kutoka kwa maofisa wa Takukuru kuhusu kuwapo kwa mazingira ya rushwa yanayofanywa na wajumbe wa mkutano huo na baadaye alifika katika ukumbi wa mkutano.

"Baada ya kupata taarifa kuhusu mazingira ya rushwa, nilitoka nje na kweli ukumbini sikukuta watu. Niliposhuka chini niliwakuta wajumbe wengi wakiwa wamesimama makundi. Sikujua na wala sikushuhudia nani aliyekuwa anatoa rushwa ila maofisa wangu wameliona hilo," alisema Mahiza.

Mkuu huyo wa mkoa aliendelea kusema, "Najua nitabeba lawama kubwa sana, nitatukanwa sana na baadhi yao, lakini hili sitalivumilia."

Nafasi iliyodaiwa kuwa ndiyo iliyokuwa ina wagombea waliokuwa wakichuana vikali zaidi ni katibu wa uchumi ambayo wagombea wake ni, Imani Madega na Haji Abuu Jumaa.

Baada ya kuahirishwa kikao hicho, Mahiza alifanya kikao cha ndani na wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa (NEC) wa mkoa huo, Ridhiwan Kikwete na Rugemalila Lutatina.

Alipotakiwa kuzungumzia hali hiyo jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema, " Waseme wenyewe wa Pwani. Kama imetokea leo siwezi kupata taarifa leo."

Aliendelea kusema," Kama imetokea wataleta taarifa, zikifika tutakuwa na cha kuzungumza, lakini leo waache waseme wao kwanza."

HIVI KWELI TAKUKURU HAWAWAONI WATOAJI RUSHWA NA KUWAKAMATA???????

Kwenye alama nyekundu hao ndio walisababisha kikao kuvunjika kwa kuwa ilionekana mtu wao hawezi kupita wakaleta kisingizio cha rushwa, mbona sehemu nyingine rushwa ilikuwepo waziwazi na uchaguzi ukafanyika. Mkuu wa Mkoa alikutana nao kupewa maelekezo ya kufanya,maana kila mkutano una msimamizi ambaye ndiye mwenye mamlaka kwenye mkutano huo, sasa kupata ushauri wa wajumbe wawili ina maana gani? Au kwa kuwa kuna mtoto wa RAISI?
 
Back
Top Bottom