CCM na Pilika za Kumpiga Chura Mateke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na Pilika za Kumpiga Chura Mateke

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albedo, Jan 17, 2011.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  1: Alianza Chagonja na Mkwara wake huku akiongea kwa kukunja Sura kama anakata Gogo kwa kutoa Kauli za Vitisho bila kuushirikisha Ubongo wake

  2: Jeshi la Polisi na Lenyewe likaja na Mkanda kwenye TV( Wenyewe wakaita kipindi Maalumu) ukionesha Jinsi lilivyofanya Mauaji kule Arusha

  3: Likaja Gazeti la Chama Habari Leo na Habari za Kizushi juu ya mazishi ya Mashujaa kule Arusha ( Kilichofuata ni Aibu kwa Mhariri na anaweza kupelekwa Mahakamani kwa Kuposha juu ya Ukweli wa Marehemu Ismail)

  Pilika Pilika hizi zinazofanywa na Propaganda Machine za CCM i.e Jeshi La Polisi, Tambwe Hiza, Makamba, Chatanda na wengine wengi waliodandia Treni kwa Mbele Bila kujua madhara na mbaya zaidi bila kupima Spidi yake zimenifanya Nijiulize Swali Moja

  HIVI UNAPOMPIGA CHURA MATEKE KWA NYUMA MATOKEO YAKE NI NINI?

  Had Makamba and the co. ever asked themselves this Question? Hivi Intelijensia ya Polisi haikuweza kweli kutambua Madhara ya Hatua wanazochukua ni Sawa na Kumpiga Mateke Chura kwa Nyuma?

  Kwamba Kwa kutoka kwao na Matamko yanayojinganya yatawafanya watu waamini kwamba Vifo vya Mashujaa wa Arusha vilitokana na Maandamano na Si RISASI RISASI ZA MOTO ZA POLISI? Kwamba Mtu anaweza kufa kwa Kuandamana kwa Amani?

  Hivi CCM kuna watu wanaofikiri kweli?
   
Loading...