CCM na Mwigulu mnajua kinachoendelea Marekani?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,412
38,704
Wakati Mwigulu na wana CCM wenzake wanafanya kila jitihada kuwadanganya watanzania kwamba Marekani na ulaya uchaguzi ukimalizika walioshindwa husubiri uchaguzi ujao bila ya kufanya kazi za siasa, hali halisi inaonesha kwamba huo ni uongo.

Ben sanders.jpg

Huu ni mkutano uliofanywa Jumamosi usiku na Benn sanders aliyeingia kwenye kura za maoni ndani ya chama cha Democrat kuomba kugombea Urais kupitia chama hicho kwenye Uchaguzi wa mwaka 2016 na kushindwa na Hilary Clinton. Kwenye mkutano huu Sanders alifanya siasa zote pamoja na kumshutumu Donald Trump jinsi anavyoendesha nchi ya Marekani.

Hoja kwamba wanasiasa na vyama vilivyoshindwa uchaguzi nchinin Marekani vitasubiri mpaka 2020 ndiyo vifanye kazi za siasa Mwigulu kazitoa wapi?
 
Mbona Marekani hawatuigi sisi ambao tunauza Vyama kwa Mabilionea?

Kwa Taarifa yako hiyo ni People's Summit ambayo inafanyika kwa Mwaka Mara Moja ni Si Mkutano wa Kisiasa Moja kwa Moja Unahusisha watu wengi.

Jamaa Uko Shallow sana aisee hujui hata People's Summit unaifananisha na Mikutano ya CHADEMA?
 
Lile ni tukio la Kila Mwaka naomba Mlikubali wewe pamoja na Ummoja wenu wa Vilaza-Tanzania (UVT)
Lipi ni tukio la kila mwaka, kufanya siasa baada ya uchaguzi ni tukio la kila mwaka? Halafu mbona kila siku maandamano yanafanyika Washington DC kumpinga ama kumuunga mkono Trump? UVT ni kifupisho cha Umoja wa Vijana Tanzania kabla ya kubadilishwa na kuitwa Umoja wa Vijana wa CCM-UVCCM.
 
Lile ni tukio la Kila Mwaka naomba Mlikubali wewe pamoja na Ummoja wenu wa Vilaza-Tanzania (UVT)
Je wanazuiwa kuongea na maamuzi ya Trump? Say obama, hilary akitaka fanya hivo ni trump anamzuia? Mlivo mazuzu mnajilinganisha na ulaya na marekani upande mmoja na mnasema uwongo na mengine ya muhim sana mbona hamjilinganishi nao... kama demokrasia, uhuru wa habari etc... watu mmeshindwa wapa hata maji tu ya kunywa watz na hata kuwa na vyoo vya shimo kwa miaka yote mliyo kuwa madarakani tangu uhuru.. . Hovyoooooo... na wewe unalipwa visent na kiwa shabiki....
 
Je wanazuiwa kuongea na maamuzi ya Trump? Say obama, hilary akitaka fanya hivo ni trump anamzuia? Mlivo mazuzu mnajilinganisha na ulaya na marekani upande mmoja na mnasema uwongo na menginenya muhim mbona hamjilinganishi nao... watu mmeshindwa wapa hata maji tu ya kunywa watz na hata kuwa na vyoo vya shimo kwa miaka yote mliyo kuwa madarakani tangu uhuru.. .
Mbona Nyinyi Juzi Kati Mlikua na Summit/Baraza la Chadema Dodoma na Mliropoka Maneno Mengi! Si inafanana na za akina Bern?
 
Lipi ni tukio la kila mwaka, kufanya siasa baada ya uchaguzi ni tukio la kila mwaka? Halafu mbona kila siku maandamano yanafanyika Washington DC kumpinga ama kumuunga mkono Trump? UVT ni kirefu cha Umoja wa Vijana Tanzania kabla ya kubadilishwa na kuitwa Umoja wa Vijana wa CCM-UVCCM.
Ha haaa haaaa.... utamkuta huyu nae msomi ana kadigrii kake kamoja... kupewa vipesa tu na watawala analisaliti taifa. hovyo kweli hawa UVT.....
 
Lipi ni tukio la kila mwaka, kufanya siasa baada ya uchaguzi ni tukio la kila mwaka? Halafu mbona kila siku maandamano yanafanyika Washington DC kumpinga ama kumuunga mkono Trump? UVT ni kirefu cha Umoja wa Vijana Tanzania kabla ya kubadilishwa na kuitwa Umoja wa Vijana wa CCM-UVCCM.
People's Summit ilifanyika hata mwaka Jana.
 
Mbona Nyinyi Juzi Kati Mlikua na Summit/Baraza la Chadema Dodoma na Mliropoka Maneno Mengi! Si inafanana na za akina Bern?
Vikao na mikutano ya kisiasa ni vitu tofauti sana. Halafu si mwanasiasa mmoja mwenye haki ya kumpangia mwanasiasa mwenzake jinsi ya kuendesha siasa. Kama CHADEMA wanaona mikutano ya hadhara ndiyo njia sahihi ya kufanya siasa zao si CCM wenye mamlaka ya kuwaambia wasifanye bali ni sheria. Je kuna sheria inayozuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa baada ya uchaguzi kupita?
 
People's Summit ilifanyika hata mwaka Jana.
Lakini inapofanyika huwa wanaomba "ruhusa" ya kufanya ama Trump anakuwa na mamlaka ya kuwaambia wasifanye au wakifanya wanaweza kukamatwa kwa maneno watakayoyasema kwenye mkutano wao huo?
 
Lakini inapofanyika huwa wanaomba "ruhusa" ya kufanya ama Trump anakuwa na mamlaka ya kuwaambia wasifanye au wakifanya wanaweza kukamatwa kwa maneno watakayoyasema kwenye mkutano wao huo?
Wale wana Utaratibu Maalumu nyinyi Si Mnataka Kutanda Barabarani Kuzuia Shughuli za Kichumi kwa Kufunga Barabara hizo kitu ndo Hakikubali hizo Summit wenzetu wanafanya Sehemu Maalumu hakuna Usumbufu.

Allen Mbona Kichwa chako Kimekua chepesi sana siku hizi! Ulihonga nini hadi Ukawa verified maana si Kwa Akili hizi au Kuna mtu alikutumia Applications!
 
Lipi ni tukio la kila mwaka, kufanya siasa baada ya uchaguzi ni tukio la kila mwaka? Halafu mbona kila siku maandamano yanafanyika Washington DC kumpinga ama kumuunga mkono Trump? UVT ni kifupisho cha Umoja wa Vijana Tanzania kabla ya kubadilishwa na kuitwa Umoja wa Vijana wa CCM-UVCCM.
Achana na majanga ya Lumumba haya mkuu, Menyewe yanajali matumbo tu hayajui kitu. Uhangaika na Lemutuz mmbeba viatu vya Diamond achana nae.
 
Wale wana Utaratibu Maalumu nyinyi Si Mnataka Kutanda Barabarani Kuzuia Shughuli za Kichumi kwa Kufunga Barabara hizo kitu ndo Hakikubali hizo Summit wenzetu wanafanya Sehemu Maalumu hakuna Usumbufu.

Allen Mbona Kichwa chako Kimekua chepesi sana siku hizi! Ulihonga nini hadi Ukawa verified maana si Kwa Akili hizi au Kuna mtu alikutumia Applications!
Huo utaratibu maalum si unafaa kwenye nchi ambazo miji yake imepangwa? Hapa Tanzania Serikali inayoongozwa na CCM imepima na kupanga matumizi ya ardhi chini ya asilimia 10 tu ya ardhi yote iliyopo. Halafu kwa mfano watu kufanya mkutano Jangwani wanaziba barabara ipi? Ila maandamano ya Bongo Movie hayazibi barabara na kuzuia shughuli za kiuchumi?
 
Wale wana Utaratibu Maalumu nyinyi Si Mnataka Kutanda Barabarani Kuzuia Shughuli za Kichumi kwa Kufunga Barabara hizo kitu ndo Hakikubali hizo Summit wenzetu wanafanya Sehemu Maalumu hakuna Usumbufu.

Allen Mbona Kichwa chako Kimekua chepesi sana siku hizi! Ulihonga nini hadi Ukawa verified maana si Kwa Akili hizi au Kuna mtu alikutumia Applications!
Hakuna unachokifahu wewe kilaza usidanganye watu hapa. Unahangaikia tumbo lako kubwa hakuna asiyekujua? Njoo na data kama usiropoke tuu.
 
Back
Top Bottom