CCM na Mpango wa Kumuua Zitto

CCM na Mpango wa Kumuua Zitto

..tayari Chadema imewahi kuongozwa na Mwenyekiti Muislamu, Mzee Mohamed "Bob" Makani.

..Makamu wa Mwenyekiti wa Chadema ni Muislamu.

..matatizo ya Zitto ni ukaribu wake na makada wa CCM na kuyumba-yumba kimsimamo.

Joka Kuu,

Ni kweli Bob Makani ni muislamu na pia aliwahi kuwa mwenyekiti wetu lakini kuna masuala ya kuangalia kama haya hapa chini;

1. Jinsi gani wahafidhina katika chama walipopambana kuzuia ushindi wa Bob kule Mwanza hadi kufikia kufanya vurugu na Freeman Mbowe kutoa bastola na kupiga risasi ndani ya ukumbi wa mkutano. Chaguo lao wakati ule lilikuwa Mzee Ndesamburo lakini nguvu za wanachama zikasimama.

2. Jinsi gani wahafidhina hasa wale wa mkoa wa Kilimanjaro ambako ilikuwa ngome ya chama kisiasa na kiuchumi hao walipokisusa chama hadi pale walipofanikiwa kukichukua tena kupitia kwa kijana wao Mbowe.

Kuhusu Makamo wa mwenyekiti ni kweli lakini ni lini umewahi kumsikia? Huoni kuwa uwepo wake hana tofauti na ilivyokuwa wakati wa Chacha Wangwe na hivi karibuni yule mgombea mwenza wetu. Vipi ukiambiwa huyu naye anawekwa katika kundi la kina Kabwe na kuwekwa kando katika masuala yote ya uongozi wa chama isipokuwa pale tu kwenye vikao vya chama ambako anacommand heshima kubwa.

Nakubaliana nawe kuwa ubaguzi wa dini dhidi ya Zitto sio sababu kuu lakini wapo ambao wanamuona yeye kuwa sio mwenzao mradi tu hatoki katika kundi la wenye kuamini kuwa CDM ni chama chao na yeye kwa mujibu wa dini yake anaonekana sio mtu wa kumuamini.

Kwa taarifa yako haya mambo yanayoendelea ndani ya chama ni muendelezo wa historia yetu tangia mwanzoni lakini sasa ametokea mtu ambaye hayuko tayari kuona maambano haya kati ya wapenda mabadiliko na wahafidhina yanasonga mbele mpaka kieleweke.
 
labda ashinde uraisi kupitia mgongo wa shujaa Dr Slaa,lakini hivihivi na ukinyonga wake usioeleweka,hawezi shinda kamwe.watanzania wapenda mabadiliko wameshapoteza imani naye siku nyingi.
zitto hayuko juu ya CDM na asidhani jeuri na kiburi chake kinatufurahisha wananchi.kwani kabla ya zitto cdm haikuwepo?atapita kama walivyopita wengine na aidhani kwa cdm yeye pekee ndo mwenye mipango ya kuwa raisi 2015.kuna wengine wazuri hawajajitokeza bado asubiri muda tu.hiki sio kipindi cha wabunge watano wa CDM bungeni

Hiki kiswahili bana.....haya sio mambo mema
 
Hivi karibuni kwenye taarifa ya habari TBC1 Manumba alisikika akitamka kwamba Zitto anatishiwa kuuawa! Ni habari ya kuogopesha na kushangaza kwa vile watanzania hatuna utamaduni wa mauaji. Hadi mkuu wa jeshi la polisi atoe kauli kama hiyo, upelelezi wa kina umekwishafanyika na ushahidi wa uhakika na wa kutosha upo! Tena tunaamini mkuu wa namna hiyo hawezi kuropoka ovyo!

Suala la njama za mauaji si la kufumbiwa macho hata kidogo. Liwekwe hadharani na watuhumiwa wafikishwe mahakamani na sheria ichukue mkondo wake. Manumba asipofanya hivyo, akiri hadharani kwamba aliropoka na kisha ajiuzulu.

Kwa mawazo yangu, kwa kuwa jeshi la polisi limekuwa la CCM, matamshi ya namna hii yanaweza kuwa maandalizi ya awali ya kuwahadaa wananchi ili baadae CCM wenyewe watekeleze mauaji na kisha wawasingizie wapinzani wao ili kuwamaliza kisiasa. Huu ndio mwendelezo uleule wa umafia wa Mahita kwa chama cha CUF alipoonyesha kisu kupitia taarifa ya habari ya ITV chenye rangi ya bendera ya CUF siku moja kabla ya uchaguzi miaka kadhaa iliyopita na watanzania wakaamini habari ile ya uzushi..

CCM wanafahamu kwa sasa hali yao ni mbaya na uchaguzi wa 2015 ni patashika. Kauli ya Manumba ni maandalizi ya uzushi mwingine ili baadae watekeleze mauaji ya Zito kisha wawasingizie CHADEMA ili kuwamaliza kisiasa. Wanatafuta namna ya kuua mijadala ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Manumba atoe majina ya watuhumiwa wa mauaji hadharani. Ee Mungu utuepushe na huyu pepo mchafu aliyeivamia nchi yetu!

CCM haina uwezo wa kumwua Zitto.
Zitto anajiua mwenyewe.
 
Zitto anapata migogoro Chadema kwa Dini yake, chadema hawatokubali kuona muIslam anakuwa Mwenyekiti, ilo asahau kabisa. Huo ndio ukweli.

chadema hawatakubali mtu mwenye uswahiba na mafisadi na ccm kuwa mwenyekiti...huo ndio ukweli
 
Gazeti la Majira la leo limenena ya kuwa.................Zitto:Sikupewa sumu....................................

Hii yaashiria ya kuwa debe la maisha ya Zitto kuwa hatarani ni la viongozi serikalini na ndani ya CCM tu....lakini si la pahali pengine...................

hapo kwenye blue sijakuelewa!kwani zitto hayuko ndani ya CCM?Zitto is a secret and open member of CCM..get it
 
Hivi karibuni kwenye taarifa ya habari TBC1 Manumba alisikika akitamka kwamba Zitto anatishiwa kuuawa! Ni habari ya kuogopesha na kushangaza kwa vile watanzania hatuna utamaduni wa mauaji. Hadi mkuu wa jeshi la polisi atoe kauli kama hiyo, upelelezi wa kina umekwishafanyika na ushahidi wa uhakika na wa kutosha upo! Tena tunaamini mkuu wa namna hiyo hawezi kuropoka ovyo!

Suala la njama za mauaji si la kufumbiwa macho hata kidogo. Liwekwe hadharani na watuhumiwa wafikishwe mahakamani na sheria ichukue mkondo wake. Manumba asipofanya hivyo, akiri hadharani kwamba aliropoka na kisha ajiuzulu.

Kwa mawazo yangu, kwa kuwa jeshi la polisi limekuwa la CCM, matamshi ya namna hii yanaweza kuwa maandalizi ya awali ya kuwahadaa wananchi ili baadae CCM wenyewe watekeleze mauaji na kisha wawasingizie wapinzani wao ili kuwamaliza kisiasa. Huu ndio mwendelezo uleule wa umafia wa Mahita kwa chama cha CUF alipoonyesha kisu kupitia taarifa ya habari ya ITV chenye rangi ya bendera ya CUF siku moja kabla ya uchaguzi miaka kadhaa iliyopita na watanzania wakaamini habari ile ya uzushi..

CCM wanafahamu kwa sasa hali yao ni mbaya na uchaguzi wa 2015 ni patashika. Kauli ya Manumba ni maandalizi ya uzushi mwingine ili baadae watekeleze mauaji ya Zito kisha wawasingizie CHADEMA ili kuwamaliza kisiasa. Wanatafuta namna ya kuua mijadala ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Manumba atoe majina ya watuhumiwa wa mauaji hadharani. Ee Mungu utuepushe na huyu pepo mchafu aliyeivamia nchi yetu!

Taarifa hizi zina utata sana.Huu knows, labda CCM na mafisadi wameshamaliza kazi nae, so they want to get rid of him asije akawa mwiba baadae.Inawezekana pia kwamba ni utoto ule wa kutaka kuonyesha uma kwamba hawako karibu naye.kumbe actually the truth is the opposite.Ukweli hata hivyo ni kwamba huyu kijana amejiingiza kwenye very dangerous territory.They might indeed take his life away,either CCM or CHADEMA.
 
Back
Top Bottom