CCM na Mpango wa Kumuua Zitto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na Mpango wa Kumuua Zitto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by RMA, Dec 24, 2010.

 1. R

  RMA JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi karibuni kwenye taarifa ya habari TBC1 Manumba alisikika akitamka kwamba Zitto anatishiwa kuuawa! Ni habari ya kuogopesha na kushangaza kwa vile watanzania hatuna utamaduni wa mauaji. Hadi mkuu wa jeshi la polisi atoe kauli kama hiyo, upelelezi wa kina umekwishafanyika na ushahidi wa uhakika na wa kutosha upo! Tena tunaamini mkuu wa namna hiyo hawezi kuropoka ovyo!

  Suala la njama za mauaji si la kufumbiwa macho hata kidogo. Liwekwe hadharani na watuhumiwa wafikishwe mahakamani na sheria ichukue mkondo wake. Manumba asipofanya hivyo, akiri hadharani kwamba aliropoka na kisha ajiuzulu.

  Kwa mawazo yangu, kwa kuwa jeshi la polisi limekuwa la CCM, matamshi ya namna hii yanaweza kuwa maandalizi ya awali ya kuwahadaa wananchi ili baadae CCM wenyewe watekeleze mauaji na kisha wawasingizie wapinzani wao ili kuwamaliza kisiasa. Huu ndio mwendelezo uleule wa umafia wa Mahita kwa chama cha CUF alipoonyesha kisu kupitia taarifa ya habari ya ITV chenye rangi ya bendera ya CUF siku moja kabla ya uchaguzi miaka kadhaa iliyopita na watanzania wakaamini habari ile ya uzushi..

  CCM wanafahamu kwa sasa hali yao ni mbaya na uchaguzi wa 2015 ni patashika. Kauli ya Manumba ni maandalizi ya uzushi mwingine ili baadae watekeleze mauaji ya Zito kisha wawasingizie CHADEMA ili kuwamaliza kisiasa. Wanatafuta namna ya kuua mijadala ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Manumba atoe majina ya watuhumiwa wa mauaji hadharani. Ee Mungu utuepushe na huyu pepo mchafu aliyeivamia nchi yetu!
   
 2. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Anthony Kayanda, Kigoma
  [​IMG]

  Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe


  MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amezua jambo jingine kwenye chama chake cha Chadema baada ya kueleza kuwa kelele zote ndani ya chama hicho, zinatokana na fitina ambazo zimejengwa baada ya kutangaza kuwa mwaka 2015 atagombea nafasi kubwa kwenye uchaguzi mkuu.

  Zitto, ambaye alijipatia umaarufu katika Bunge la Tisa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja, ndio kwanza ametoka kwenye mgogoro na wabunge wenzake baada ya kutofautiana na uamuzi wao wa kutoka kwenye ukumbi wa Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete akianza kuhutubia ili kutuma ujumbe wa msimamo wa chama wa kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais.

  Kabla ya uchaguzi, Zitto alisababisha kizaazaa baada ya kutangaza kugombea uenyekiti wa Chadema katika kipindi ambacho chama hicho kilionekana kutaka mwenyekiti wake wa sasa, Freeman Mbowe aendeleze kazi ya kukijenga chama.


  Zitto pia alitofautiana na viongozi wenzake baada ya kutamka hadharani kuwa haungi mkono uamuzi wa katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa wa kuwaachisha kazi wafanyakazi wawili kwenye ofisi ya makao makuu ya chama hicho kwa tuhuma za kuvujisha siri.

  Tamko lake kwenye mkutano wa hadhara aliouitisha kwenye Uwanja wa Cine Atlas mjini Kigoma juzi unaonekana kukaribisha mgogoro mwingine baina yake na wanachama wenzake baada ya kutuhumu kuwepo na njama dhidi yake kutokana na nia ya kugombea urais mwaka 2015 baada ya Dk Slaa kuzoa kura nyingi katika uchaguzi wa mwaka huu alipogombea nafasi hiyo.


  Zitto, ambaye katika siku za karibuni amekuwa akitofautiana na wanachama wenzake kiasi cha kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye katika uongozi wa kambi ya upinzani bungeni, alisema hayo juzi katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika eneo la Cine-Atlas lililo Ujiji mjini Kigoma.

  Zitto aliuambia mkutano wa hadhara kuwa kelele zote ndani ya Chadema zimetokana na fitina zinazotengenezwa dhidi yake kwa kuwa kuna uwezekano kwake wa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.


  "Baada ya uchaguzi kumalizika, watu sasa wanajipanga kwa ajili ya uchaguzi mwingine. Kuna watu wanaotaka nihame Chadema kwa kuwa wananiona ni kikwazo kwao, lakini nasema siwezi kuhama kwa kuwa nina mtazamo wa mbele wa kugombea urais," alisema Zitto.

  "Kigoma inaweza kumtoa rais ingawa watu wanasema haiwezekani kwa sababu ni mwisho wa reli (ya Kati). Nasema siwezi kufanya makosa ya kuhama kama walivyofanya walionitangulia na wakapoteza dira.


  "Kingine najua mtakuwa mmesikia mengi kupitia vyombo vya habari, lakini nataka niwaeleze kwamba sikulishwa sumu na hakuna anayeweza kunipa sumu."

  Mbunge huyo ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa Chadema, aliongeza kusema: "Mimi sing’oki Chadema kamwe na wale wanaotaka nitoke basi waanze wao. Kwa sababu, chama hiki ni chetu. Watu waliteswa, walifungwa jela, hata kupigwa na polisi na kuumizwa kwa ajili ya Chadema. Nasema siwezi kukimbia hata mara moja."

  Alisema baadhi ya watu wa Kigoma waliokuwa viongozi wa Chadema na kuamua kukimbilia CCM baada ya kutokea mifarakano ndani ya chama hicho, wamejikuta wakipata aibu kwa kupoteza heshima mkoani Kigoma.


  Alisema viongozi hao licha ya kukimbilia CCM, bado mkoa huo haujapiga hatua yoyote kubwa ya kimaendeleo jambo linaloonyesha kwamba maendeleo hayaletwi na chama bali ni juhudi na mikakati ya viongozi kwa kushirikiana na wananchi katika kuibua miradi, kuisimamia na kuitunza kwa faida ya Jamii.

  Zitto alibainisha kuwa migogoro yote inayoonekana Chadema ni mchakato wa kidemokrasia lakini kwa ujumla mambo ni shwari ndani ya chama hicho.


  "Ndugu zangu nataka niwaambie kwamba, kwa kawaida, baada ya uchaguzi mmoja, watu hujipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao. Sasa haya mnayoyasikia ni mchakato wa kidemokrasia tu ndani ya Chadema, lakini kwa ujumla mambo ni shwari," alisema.

  Zitto ametoa kauli hiyo takriban majuma mawili tangu alieleza gazeti hili kuwa ameamua kutozungumzia masuala ya chama chake kwa kuwa ameona kufanya hivyo ni kuchochea migogoro.


  Zitto alikuwa ametakiwa kutoa msimamo wake baada ya kamati kuu ya Chadema kukataa kuidhinisha uamuzi wa wabunge wa chama hicho kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye na kumtaka mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kupima mwenyewe uzito wa kitendo hicho cha wabunge wenzake.

  Katika hatua nyingine, Zitto aliwataka viongozi wa Chadema kujiuliza sababu zilizosababisha NCCR Mageuzi kushinda majimbo manne mkoani Kigoma huku walioshinda ubunge wakiwa wanachama walioihama Chadema.


  "Viongozi (Chadema), tunapaswa kukaa chini na kutafakari kwa kina, tatizo lipo kwetu sisi viongozi au tulisimika wagombea wasiokubalika?

  "Kati ya wabunge wanne wa NCCR, watatu walikuwa viongozi wetu wa chama hadi mwaka 2009 na kama tungekaa nao vizuri, pengine leo hii wangekuwa wabunge wetu na kuongeza idadi yetu Kigoma."

  Aliwaeleza Wananchi hao kwamba Serikali ina tabia ya kusikiliza sauti ya Kigoma wakati mbunge anapokuwa chama cha upinzani na kwamba hali hiyo imechangia mkoa huo kuanza kupata miradi ya barabara kadhaa za lami, hivyo kurahisisha shughuli za uchukuzi na usafirishaji, jambo lililokuwa kikwazo kwa miaka mingi mkoani humo.


  Kuhusu kesi inayomkabili mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Chadema, Ally Mleh Zitto alieleza kwamba wabunge wa Chadema wanaotoka Kigoma watahakikishiwa wanaisimamia kesi hiyo, ili iweze kusikilizwa na maamuzi kutolewa kwa haki na kwamba chama hicho kinatarajia ushindi.


  Zitto alisema kwa mujibu wa fomu za matokeo zilizokusanywa kutoka vituoni, mgombea wa Chadema alishinda katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu.

  Katika uchaguzi huo zilizuka vurugu kubwa baada ya polisi kuwapiga mabomu ya mochozi wananchi waliofurika kwa wingi katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kigoma Mjini kufuatilia matokeo.

  Hata hivyo, Serukamba aliwaeleza wananchi Desemba 17 kwamba kamwe hatarajii kupoteza nafasi hiyo kutokana na kesi dhidi yake kutokuwea na ushahidi wowote wa kumkwamisha.


  Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa kwa mara ya kwanza Januari 15, 2011 katika Mahakama Kuu Kanda ya Magharibi ambapo inatarajiwa kutawala hisia za wengi ndani na nje ya Jimbo hilo.
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Zitto anapata migogoro Chadema kwa Dini yake, chadema hawatokubali kuona muIslam anakuwa Mwenyekiti, ilo asahau kabisa. Huo ndio ukweli.
   
 4. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,077
  Likes Received: 4,662
  Trophy Points: 280

  Where i highlighted RED nimjibu professionally

  1. hakuna fitina umeji fitinisha mwenyewe
  a) kwa kupingana na wabunge wenzako during Walk-out, tukajua ww si mwenzetu
  b) la kugombea urais hizo ni ndoto kila mtu ana ndoto hata za Ali nacha zilikuwa ndoto, usijidanganye ww maarufu, that is not sign of intellectuals instead you will expose u r arrogance.

  2. uliposema Dowans inunuliwe na Serikali na kila mmoja anajua wazi Ufisadi na kupeana na Richmond ulikuwa unaota? au ulilishwa na mafisadi mara baada ya kuwa kamati ya madini?

  Nikushauri, usiongee kwenye magazeti thinking u will convince watu waelewa, we work with data na matendo ya mtu si unacho ongea, maneno waambie wasiokuwa na memory, ww unajua CDM members we have high & unlimited memory, tunaangalia matendo ya mtu na data kuhusu msimamo wake kisiasa, ww unahongeka kirahisi Zitto we confirmed thru you, still tupo pamoja watching you with an eagle eye, kanyaga twende
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Dec 24, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,019
  Trophy Points: 280
  ..tayari Chadema imewahi kuongozwa na Mwenyekiti Muislamu, Mzee Mohamed "Bob" Makani.

  ..Makamu wa Mwenyekiti wa Chadema ni Muislamu.

  ..matatizo ya Zitto ni ukaribu wake na makada wa CCM na kuyumba-yumba kimsimamo.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  jokaKuu,
  Kuna watu wengine hawahitaji pumzi yako au energy kuwajibu. They see but they do not comprehend. They hear but they cannot understand.
   
 7. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Wewe Dar es salaam acha udini wewe.Tatizo la Zitto sio dini yake,tatizo ni kuwa Zitto ni mbinafsi,ana umimi sana anataka kuwa maarufu kuliko CHADEMA.

  Zitto anapenda sifa,anapenda maamuzi yake kuliko ya chama.Suala la waliokuwa wanachama wa CHADEMA kugombea kupitia NCCR na kushinda ni la chama,yeye kama kiongozi wa CHADEMA alikuwa wapi siku zote kurekebisha mambo mpaka CDM kishindwe ndio aropoke ili viongozi wengine CDM waonekane hawafai na yeye aonekane bora.

  Huu ni utoto na unafiki.Katiba hairuhusu mtu kugombea Urais akiwa na umri pungufu ya miaka 40,hivyo asahau kugombea urais mwaka 2015.
   
 8. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sijaona Zitto akiyumba kimsimamo tofauti na wanasiasa wengine wa Chadema, amekuwa consistent katika kile anachikiamini; na mara zote wakati umetuonyesha kuwa alivyovisimamia vimekuwa sahihi.

  Suala hapa ni siasa za maji taka ata its best, tungekuwa tunaangalia facts, Zitto ameprove kuwa na mtizamo wa mbali sana kuliko wanasiasa wengi tunaowaona leo kuwa wapo sahihi, tunahitaji watu wengi zaidi kama Zitto ili kulikwamua taifa hili kutoka kwenye siasa za kifuasi na uadui na kuwa siasa za hoja kwa maslahi ya taifa.
   
 9. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Angalia facts zako, Zitto alilipinga hili tokea mwanzo, bahati mbaya mashujaa wetu waliwaona hao ni "sisimizi tu" bila kutazama mbali, he was right...they were wrong.
   
 10. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Rubbish wengine wanaita crap! sababu CDM haina sera, values hizo ulizosema! there is no room for religious perpetrators or fanaticism in CDM fyi!
   
 11. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Bana ee, tusidanganyane. Wangebaki Chadema pengine wasingeshinda. Baada ya kuhama, waliwezeshwa kifedha na mafisadi kupitia zitto ili kukomoa Chadema. Walikuwa ni nyoka wa zitto ndani ya Chadema kusambaratisha chama. Zitto anatumia kushinda kwao kupitia chama siyo rizki kutishia uongozi wa Chadema wasije fukuza nyoka wake waliobakia Chadema. Hatudanganyiki!
   
 12. AIZAK

  AIZAK Member

  #12
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  The wicked shall be turned into hell, and all the nations that forget God. Psalm 9:17
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Majira la leo limenena ya kuwa.................Zitto:Sikupewa sumu....................................

  Hii yaashiria ya kuwa debe la maisha ya Zitto kuwa hatarani ni la viongozi serikalini na ndani ya CCM tu....lakini si la pahali pengine...................
   
 14. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,176
  Likes Received: 1,900
  Trophy Points: 280
  Umebeba junia la nazi ngata kifuu mwanangu Zito hana mawazo kama wewe wote tumepigika waislamu wakristo na wapagani! Usiwe kipaza sauti cha mafisadi ambao ajenda yao kuwagawa wananchi kwa dini zao ili mnapo zozana Wafisadi kiulaini JITAMBUE
   
 15. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #15
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ngugu wana Jf nakumbuka wiki chache zilizopita Mh zito kabwe alikuwa ktk mvutano mkubwa na wanachama wenzake ndani ya chadema baada ya kupinga kitendo cha wabunge wa CDM kutoka nje wakati mkuu wa chi akihutubia

  lakini pia alipinga kitendo cha Mkuu wa CDM kuwa achisha kazi wafanyakazi wawili ktk ofisi ya makao makuu ya CDM

  sasaa ameamuwa kuweka wazi kwanini hayo yote yanatokea juu yake eti ni kutokana na chuki dhidi yake baada ya kutia nia ya kugombea uraisi 2015

  Huwa naamini kuwa mahali popote pale hata hapa JF kama ukiwa mkweli na muwazi kwa kila jambo hutopendwa na wasiopenda ukweli na uwazi

  hivyo Mh Zito Kabwe anaponzwa na ukweli na uwazi wake anaoutowa kwa kila jambo ndani ya chama na kwa wale wasiopenda ukweli wa mambo wataendelea kumchukia zito hadi kufa kwani ndivyo alivyo.

  Mh Zito Kabwe,endelea na msimamo wako ilimradi tu usikivuruge chama chetu,

  msema ukweli hapendwi mahali popote pale duniani

  mapinduziiiii daimaaaaaa :target::target:
   
 16. Tambara Bovu

  Tambara Bovu JF-Expert Member

  #16
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 19, 2007
  Messages: 586
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  labda ashinde uraisi kupitia mgongo wa shujaa Dr Slaa,lakini hivihivi na ukinyonga wake usioeleweka,hawezi shinda kamwe.watanzania wapenda mabadiliko wameshapoteza imani naye siku nyingi.
  zitto hayuko juu ya CDM na asidhani jeuri na kiburi chake kinatufurahisha wananchi.kwani kabla ya zitto cdm haikuwepo?atapita kama walivyopita wengine na aidhani kwa cdm yeye pekee ndo mwenye mipango ya kuwa raisi 2015.kuna wengine wazuri hawajajitokeza bado asubiri muda tu.hiki sio kipindi cha wabunge watano wa CDM bungeni
   
 17. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #17
  Dec 24, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huna point tetea mafisadi wenzako kama RA, El, Tanil, etc si wapenzi wa CDM
   
 18. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #18
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Lakini tuendelee kutambuwa kuwa tunauona ukinyonga wake kwa kuwa ni mkweli na muwazi kwa mambo mengi,hivyo kwa sisi wana CDM tusiopenda ukweli huo na uwazi wake tutaendelea kutokuwa na imani nae daima, na hii inatokana na asilimia kubwa ya wtz si wakweli hivyo hatupendi ukweli

  tumpe nafasi,anaweza fanya jambo jema ktk CDM yetu
  mapinduziiiiii daimaaaaaa:whoo::whoo:
   
 19. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #19
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  ukiwa mkweli ktk hii dunia hutopendwaaaaaaa daimaaaaa,hata wewe wajuwa hiloooooo
  mapinduziiiiiii daimaaaaaaaa
   
 20. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #20
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mh!Zitto ifikapo 2015 atakuwa ana miaka 39,hivyo hatakuwa hana sifa ya kugomea urais.katika hali ya kawaida watu wenye akili timamu hawawezi kuumiza vichwa na jambo dogo kama hili.Zitto ni mnafiki anajalibu kuficha ukweli,mbona hajaelezea kwa undani suala la yeye kupingana na msimamo wa chama chake ilihali yeye ni mwanachama kama wanachama wengine!!!
   
Loading...