CCM na Mkakati wa kuwateka vijana wasomi vyuoni..!

Ngoja waziri mkuu aliestaafu kwa kasha ya Richmond atakapoongea na waandishi wa habar anaweza akatoa way forwad na strategic plan za ushindi.
 
Wanajamvi,

CCM kama chama kikongwe cha muda mrefu mpaka sasa kosa linalowatafuna ni kukosekana kwa vijana wasomi na makini kutokana na kwamba CCM haikutoa vipaumbele kwa nafasi mbalimbali ndani ya chama kitendo ambacho kinakosa watu wenye mawazo mapya ya kusaidia chama tofauti na CHADEMA ambacho kimetumia mwanya huo kuwapa vijana wasomi na makini kukisaidia chama chao.

Mosi wamekuja kuzinduka usingizi wa pono umuhimu wa vijana kwa sasa na kukuta tayari wenzao wameshawachukua yenyewe imebakia na vijana wa watoto wa vigogo tu kama Ridhiwani,January Makamba na makundi yao walioanzisha ndani ya chama.

Kosa hili ni serious kwa CCM linawatafuna haswa wanachofanya Kinana na Nape ni kuwavuta vijana karibu na chama kitendo ambacho wanatumia nguvu kubwa sana.

Kwenu wadau.
 
CCM inawasomi wengi sana dogo,nadhani haujafanya utafiti wa kutosha,tatizo linalowasumbua ni misimamo ya chama,hapo ndo unakuta sio professor,sio mtu mwenye masters wote wanakuwa kama watoto wa shule ya msingi,wanasahau kutumia ubongo wao na elimu walionayo wanabaki kuongea waliokaririshwa
 
CCM ni wengi waliotumia madesa. Wanaamliwa kila kitu. Hapimi anachoambiwa na akili zake. Sababu wengi ni waliotumia madesa.
 
Lakini yeye kazungumzia "wasomo makini" hao uliowataja sio wasomi makini!
 
vijana wengi wa ccm ni wasomi waliobobea, tena ni wachumi, wanasheria, wahandisi na wanasayansi.
1.januari makamba ni mtaalam wa sayansi ya teknolojia na mawasiliano
2.willium ngeleja ni mwanasheria na wakili
3.pro. muhongo mtaalam wa geolojia na rasilimali za ardhini (elimu ya miamba na madini)
4.dr mwakyembe - wakili
5. Dr hamis kigwangalla - daktari wa binadam tena anamtibu tundu lissu kichwa chake
6. DR faustine ndugulile - daktari wa binadamu
 
CCM ni wengi waliotumia madesa. Wanaamliwa kila kitu. Hapimi anachoambiwa na akili zake. Sababu wengi ni waliotumia madesa.
wewe ni feki huna kitu upstair, umekariri neno madesa ili watu wajue kuwa ww umefika chuo kikuu, kumbe gilo neno umelisikia kwa ndugu yako wewe ni form four failure kama mbowe
 
Wanajamvi,

CCM kama chama kikongwe cha muda mrefu mpaka sasa kosa linalowatafuna ni kukosekana kwa vijana wasomi na makini kutokana na kwamba CCM haikutoa vipaumbele kwa nafasi mbalimbali ndani ya chama kitendo ambacho kinakosa watu wenye mawazo mapya ya kusaidia chama tofauti na CHADEMA ambacho kimetumia mwanya huo kuwapa vijana wasomi na makini kukisaidia chama chao.

Mosi wamekuja kuzinduka usingizi wa pono umuhimu wa vijana kwa sasa na kukuta tayari wenzao wameshawachukua yenyewe imebakia na vijana wa watoto wa vigogo tu kama Ridhiwani,January Makamba na makundi yao walioanzisha ndani ya chama.

Kosa hili ni serious kwa CCM linawatafuna haswa wanachofanya Kinana na Nape ni kuwavuta vijana karibu na chama kitendo ambacho wanatumia nguvu kubwa sana.

Kwenu wadau.
wataje hao vijana wa ccm ambao hawajasoma/sio wasomi
cc
mleta mada
 
CCM wameanza mkakati wa kujipenyeza tena vyuoni..!Sasa wamekuja na mkakati wa kuwarubuni vijana wasomi wapambanaji kupiota ahadi kama vile kupewa ajira katika sekta nyeti,kusomeshwa shahada za juu,pesa nk..

Mfano UDSM aliyekuwa spika wa bunge lka wanafunzi Mwangomango ameahidiwa kuwa atasomeswa shule ya sheria Tanzania pindi atakapomaliza shahada yake ya kwanza ya sSheria..,pia wapo vijana wengine wameahidiwa kuwa wataajiriwa katika mabenki pindi awtakapomaliza..!

Vijana kuwani makini kumbukeni Mwita Mwikabe Waitara aiahidiwa hivyo hivyo..!

Nawasilisha..!

c bora hata hao wa udsm wanaahidiwa kupewa nafasi,huku dodoma wanaenda kula wali tu na kupewa elfu 5 tu,mfano juzi juzi tu hapa wanafunzi wa udom walienda kula chakula na ritz mjin
 
hii ni kweli.mi nipo udom,ccm hawajitambui
 
CCM inawasomi wengi sana dogo,nadhani haujafanya utafiti wa kutosha,tatizo linalowasumbua ni misimamo ya chama,hapo ndo unakuta sio professor,sio mtu mwenye masters wote wanakuwa kama watoto wa shule ya msingi,wanasahau kutumia ubongo wao na elimu walionayo wanabaki kuongea waliokaririshwa

kuna ubeti mmoja huwa unanikera sana umekaa kiumbeaumbea.
"tumethubutu,tumeweza na tunasonga mbele" huwa najiulza ccm wameweza nn?
 
Back
Top Bottom