ccm na mikakati isiyo thabiti (INCONSISTENT STRATEGIES) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ccm na mikakati isiyo thabiti (INCONSISTENT STRATEGIES)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Omutwale, Sep 23, 2011.

 1. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hivi majuzi, kuna Mwana-JF alianika hapa JF mikakati iliyomo katika Waraka wa siri ulioandaliwa na ccm kuwamaliza CDM. Baada ya kuusoma nilihitimisha kwa kujisemea kuwa, haya ni mawazo yanayoletwa na hisia binafsi za Mwandishi. Na haya mawazo yanatokana na mapenzi yaliyomzidia Mwandishi kwa chama chake, kiasi kwamba anashindwa kutafakari taarifa kwa kina. Nilihitimisha hivyo kwa sababu kuu moja; ccm imekuwa ikikituhumu CDM kwa UKATOLIKI na UCHAGA na hivyo kuingiza UGAIDI wa Afghanistan na Libya ingekuwa ni kuua hoja ya UKATOLIKI. Na muendelezo huu ungeisaidia CDM badala ya ccm.

  Tuhuma ya UKATOLIKI imefanikiwa kwa kiasi cha kuchelewesha uhuru wa pili Tanzania. Wananchi wameshikwa kisawasawa na hoja ya UDINI kiasi kwamba hawajadili hoja bali huegemea “ni mwenzetu”. Hawajali njaa, bei ghali ya bidhaa wala ugumu wa maisha ilimradi aliyesababisha ni mwenzao. Kwa sasa udini unasafisha na kurasimisha kila aina ya ovu na dhambi. Haya ni mafanikio kwa ccm ambayo kwa mpanga-mkakati ya kisiasa mzuri angependa kuyaendeleza na kuyakomaza. Mbinu ya kuyakomaza ingekuwa kujenga hoja endelevu juu ya UDINI tena udini wa KIKATOLIKI. Hivyo basi nisingetegemea mtu makini ndani ya ccm kuendeleza hoja ya UKATOLIKI kwa kuingiza UGAIDI ambao maarifa yake yamesemekana kupatikana kutoka Afghanistan na Libya. Nasema hivi kwa sababu iwe ni propaganda ama kweli, UGAIDI umehusishwa zaidi na dini nyingine tofauti na UKRISTU achilia mbali tukio la hivi karibuni huko Norway. Nyongeza ya hapo, hakuna muunganiko kati ya UKATOLIKI na Afghanistan na Libya. Imani katika nchi hizi za Afghanistan na Libya haitoi mwanya wa kuwa na uhusiano na Ukatoliki (wanaita Ukafiri) na hasa katika mahusiano ya kimataifa. Hoja ya Ukatoliki wa CDM ingepata mashiko zaidi kama ingezidi kusukumwa kwa kuunganishwa na UMAFIA kuliko kuingiza UGAIDI. Asili ya UMAFIA ni Italy ambako Ukatoliki una mizizi. Na ni huko huko Italy ambako mlenga wa ccm ndani ya CDM alipata sehemu kubwa ya elimu yake. Kidogo hapa kungekuwa na muunganiko ambao ungeweza kuleta uhalisia wa kughushi.

  Baada ya kusoma aliyosema Wilson Mukama jana katika mkutanao wake na Waandishi wa Habari, nimekubali kuwa kumbe mimi ndiye sikuwa sahihi na Mwana-JF aliripoti kitu cha kweli kabisa. Kukiri kwangu kutokuwa sahihi ni kudhihirisha udhaifu wa hali ya juu wa ccm katika kupanga mikakati ya kisiasa na kuiendeleza. Siungi mkono mikakati ya kipuuzi yenye kuegemea katika udini, dhuluma au kuwagawa watu kibaguzi bali najaribu kuonyesha umuhimu wa kuwa thabiti (consistent) unapo panga Mkakati. Kwa kosa hili la kuchanganya UKATOLIKI na UGAIDI wa Afghanistan na Libya CDM wamepata upenyo mzuri amabo wakiutumia vema wanaweza kupunguza upinzani unaotokana na UDINI.

  Kazi ni Kwenu…….
   
 2. shegaboy

  shegaboy JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Omutwale Umesema mambo ya msingi sana na inashangaza sana na inatia aibu kwa mtu kama mkama kusema mambo ambayo moja kwa moja yanaibomoa serikali yake. Nashindwa kuelewa wale waliomuandalia huu ujumbe wanamapenzi mema na yeye au la. kwani moja kwa moja inaibomoa serikali yake. Kwanza inaonyesha kuwa Usalama wa taifa, Polisi wote hawako makini katika na kuonyesha kuwa nchi hii sasa aina ulinzi wowote kama chama kinaweza kuingiza makomandoo 33 bila usalama wataifa kujua wala polisi ila yeye mkama anajua inasikitisha sana. na napenda kusema kuwa sasa wazili wa ulinzi, mkuu wa majeshi na wazili wa mambo ya ndani, IGP wajiuzulu. Wanafanya nini katika nyadhifa zao wakatia utendaji hakuna.
   
 3. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  shegaboy,
  Asante. Hiyo pia ni hoja nyingine kuonyesha kujikanganya kwa ccm katika mikakati ya yake.
  Ni sawa na dereva kulalamika kuwa gari linakimbia sana wakati yeye ndiye anayekanyaga accelerator! ccm inajinadi kuwa yenyewe ndiyo ina serikali/dola. Na inajenga hoja kwa kuwaambia wananchi wa Igunga wasichachague wapinzani kwani wapinzani hawana dola. Na papo hapo inalalamika wapinzani kuingiza makomandoo. Huwezi kuingiza makomandoo nchini kama huna dola hasa jeshi. Huku ni kujikanganya kuliko pitiliza!
   
 4. MANI

  MANI Platinum Member

  #4
  Sep 23, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,412
  Likes Received: 1,871
  Trophy Points: 280
  Wasameheni uwezo wao kufikiri ndio upo hapo.
   
 5. M

  Musia Member

  #5
  Sep 23, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mimi hofu yangu ni uwezo wa kuchambua mambo walio nao viongozi wa CCM. Wanatakiwa kuwa makini sana na propaganda za aina hiyo kwa sababu sielewi inakuwaje wao kama chama wazipate hizi taarifa kabla ya idara zetu za usalama na jeshi. Yaani sipati picha kwamba wao ndio wanaopata taarifa mwanzo na kuzitolea katika uwanja wa siasa. Nilitegemea wasemaji wa mambo hayo wawe ni idara zetu za usalama na sio chama cha siasa. Huu ni udhalilishaji kwa jeshi, usalama wa taifa, uhamiaji na polisi.
   
 6. joseeY

  joseeY Senior Member

  #6
  Sep 23, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Hapo umenena kaka!
  Naona jambo hapa. Ili uwe na wadhifa fulani ndani ya CCM basi lazima uwe umethibitika kuwa na hitilafu kidogo kwenye ubongo. Maneno kama ya Mukama nilikuwa nayasikia kwa Tambwe Hizza na kuondolewa kwake nilikutafsiri km CCM kuimarika kimaarifa lkn leo nimegundua 'I was wrong'. Wamemfukuza afadhali, wamemkaribisha potelea mbali.

  Mukama anadai CDM wameleta Makomandoo waliopata mafunzo Libya, Palestine na sijui wapi kwingine anakojua na inaonesha kuwa taarifa za usalama hapa kwetu zinatoka CCM kwenda polisi na sio polisi kwenda serikalini. Wakati Sophia Simba aliposema CDM inadhaminiwa na mabepari wa Kiingereza alidai anao ushahidi na akaahidi kuutoa akiungwa mkono na waziri wa mambo ya nje. Mpaka leo hakuna hata fununu ya ushahidi wao pamoja na kukumbushwa mara kadhaa. Kama Mukama nae ameahidi kutoa ushahidi wa makomandoo wa CDM basi ni vyema wakaacha utoto wa kusema mambo kama wapo kilabuni. Na pengine hizi ndio siasa chafu za CCM alizozisema fisadi Rostam.

  Ni shida sana kuongozwa na watu wasio na upeo wa kufikiri badala yake midomo ndio inakuwa bize kuongea kila kilichowazwa bila hadhari. Makamba mropokaji kaenda kaja Mukama mbwabwajaji.
   
 7. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  huwezi kupata makomandoo kwa njia za panya hawa tuwaite magaidi.
  ccm kwisha kazi.
  Kama chadema imeweza kuingiza magaidi 33 nchini tanzania marekani hawajui,tanzania haijui ila ccm inajua na imeshindwa kuzuia na kuwaomba wananchi wa igunga waisaidie maswali ni mengi kuliko majibu.
  1.wapiga kura wa igunga wana nguvu kuliko serikali ya ccm?
  2.chadema hawashikiki?
  3.polisi,usalama wa taifa,jwt na uhamiaji hawana kazi?
  4.taarifa za itelejensia za ccm ni nzuri kulio za dola kwa hiyo vyombo vya dola viondolewe serikalini na kukabidhiwa ccm?
  5.je hawa magaidi ni watanzania au ni waarabu?
  6.kama ni waarabu wanaigunga wanaelewanaje nao kwani amedai wamegawanywa vijijini?
  7.kama ni watanzania walipelekwa libya na afghanistan kwa ajili ya igunga tu?

  Mukama nilidhani ni mtu makini ila kwenye hili yeye si gamba tu balikansa ndani ya gamba.
   
 8. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mzee Jenerali Ulimwengu aliwahi kusema kuwa...
  Mtu aliyevimbiwa haitaji "kujivua gamba" sababu hiyo sio sababu ya kuvimbiwa kweke..
  Ila anahitaji "haluli" ili aile ikasafihe tumbo na kuondoa kuvimbiwa huko!
  Kuchanganya huku kwa madawa ndio kilichowakumba CCM chama chenye "viongozi"
  Waliovimbiwa kwa ulafi wa mali za umaa.......
  Nadhani ni heri kwa mustakabali wetu kwa watu hawa waliovimbiwa as soon watapasuka matumbo!
   
Loading...