Makala kama kweli ni mkweli yeye alitakiwa kuwapa waandishi wa habari hizi risiti wazione na awape copy waweke hadharani maana si siri ila alitaka ukweli . Tutajuaje kama risiti hizo ni za magari yaliyo bandarini ? Why idadi inapungiua tena na wakati wakubwa wake walisema ni 200 ? Je baada ya kumwita Slaa muongo ndiyo hawaendi mahakamani kama walivyo tamka ? Bado kuna siri kubwa ukweli mwingi umefichwa.Ngojeeni Slaa akiibuka .
SHUPAZA na Wana JF,
Kilichobakia ni kuhakikisha Dr. W. Slaa anakuwa Rais wa nchi yetu mwaka ujao. Kazi ifanyike. Hakuna mbadala.
Safari,Tatizo ni Registrar of Political Parties...lazima vyama vi-file in returns za mapato yao aidha toka kwenye michango,fadhila nk..hili sijalisikia Tanzania lakini kwingineko ipo..hata UK ilitoka zogo siku za nyuma juu ya finances za labour...15bn/- sio mzaha..wamwpata wapi?Ruzuku haifiki huko na sidhani wanachama wanalipa michango yao maana sijaona mkakati wa makamba.makalla & co(walaji not advocates) kufuatilia memebrs fees hata kwa speech
HAwezi kuwa rais labda 2015, urais ni zaidi ya mtu mmoja!! Hiyo CHADEMA itaunda serikali kwa potential figures zipi? Tuwe realistic sometimes... na tuache kumuonea Slaa, wacha aendelee kuwa mbunge kwani kule mchango wake ni muhimu sana
Potential figures? una maana ganai?? Hivi CCM zipi ni potential figures?? Je hizo potential figures zimetufikisha wapi?? Sasa kama akina Ghasia, Matayo, Nchimbi, Bendera, Mdhihiri, Mama Ntimizi, Mama Sitta, Megji n.k wameweza kuwa mawaziri iweje leo useme Chadema hawana watu. Hivi vichwa kama vyote vile Chadema unaona havifai. Tatizo mnaangalia Balaza la mawaziri 60. We do not need 60 ministers in a poor country like ours.A maximum of 20 Ministers can do the job.
Wala usifikiri eti selikali mpya ikiingia makatibu na wakurungenzi nao watabadilika.
Mkulima,Lunyungu,
Mpeni Dr. Slaa data za ukweli. Akikosea mara mbili au tatu kama alivyofanya kweli hili la magari, tayari mnakuwa mmewapa CCM ngao ya kummaliza. Kumbuka ya Mrema, alikuwa analipua mabomu ya kweli lakini baada ya muda CCM wakaanza kumpelekea data fake ili aumbuke na kuonekana mwongo.
Ni mategemeo yangu hatutaenda huko na Dr. Slaa. Hii habari sio siri Dr. Slaa ameongea kitu ambacho sio ukweli.
Mkulima,
Ukweli wa ukwepaji huu haujawekwa hadharani na ccm bado. Tutaendelea kuwakaba koo hadi ushuru wote utakapolipwa. Mbinu zote tumezikamata, hakika safari hii hawatapata mteremko kama ilivyokuwa wakati wa Meremeta, Deep Green. Sisi tunachotaka ni Ushuru na kodi zilipwe ili shule zijengwe, Zahanati zijengwe, Barabara zijengwe na wananchi wapate maji. Tumesema nchi hii imetafunwa ya kutosha na sasa inatosha. Ni vizuri wana JF muwe wachunguzi badala ya ushabiki hata kama ni mwana ccm damu damu. Ukosefu wa shule unawabana sawa sawa wajomba zako, wapwa zako walioko vijijini hata kama wewe unanufaika kwa kiwango chochote kile kile.
Mama na dada zako wanatembea kilomita na kilomita kusaka maji na maajabu yanatokea kwenye msako huo na hakuna anayeyazungumzia. Ni swala la dhamira tu. Ushabiki tu hauwezi kulikomboa Taifa hili. Tunataka Ushuru wote na kodi zote zilipwe. Full stop. Siku zimelipwa zote tutanyamaza lakini vinginevyo niliisha kuwapa ruksa waende mahakamani. Hapo ndio data zote zitamwagwa mpaka ushuru wa Mahindra uliokwepwa mwaka 2005, baiskeli nazo pikipiki.
Mashabiki wanaweza kufikiri ni mchezo, lakini wako bado watanzania wenye dhamira!!! na Nchi hii itaendelea kutetewa kikamilifu ccm hawawezi kukaa tena kwa amani
yako wapi hayo maelezo?
Kuelezea ukwepaji wa kodi na dhuruma inayofanywa na viongozi wa CCM si wewe mfuasi usijua hata a/c ya chama ya tawi/kijiji chako.Ni nini umuhimu wa bandiko hili?
Ni nini umuhimu wa bandiko hili?
Ni nini umuhimu wa bandiko hili?