CCM na Kikwete, nataka majibu

CCM na Kikwete, nataka majibu

GIBA KB

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2012
Posts
367
Reaction score
111
Katika kampeni za urais za mwaka 2010,mgombea urais kupitia ccm J.Kikwete alipokuwa akihutubia katika mkutano wa kampeni uliifanyika katika uwanja wa uhuru(Mashujaa) Bukoba. Alitoa ahadi ya Kujengwa kwa meli mpya kubwa kuliko MV VICTORIA itakayo rahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria kutoka Bukoba kwenda Mwanza.Nakumbuka alishangiliwa sana na wananchi wa Bukoba.Swali ni je,mchakato wa ujenzi wa Meli hii unaanza lini kwa sababu hata dalili hazionekani?
 
Kwani wakati anhutubia alisema kuwa meli hiyo itajengwa lini?
 
Hakusema lakini ahadi mara zote huwa ni deni
Nimeamua kuuliza mwaka huu sababu huyu Mzee wa sikukuu anaondoka Magogoni mwakani na hatujapata majibu
 
Katika kampeni za urais za mwaka 2010,mgombea urais kupitia ccm J.Kikwete alipokuwa akihutubia katika mkutano wa kampeni uliifanyika katika uwanja wa uhuru(Mashujaa) Bukoba. Alitoa ahadi ya Kujengwa kwa meli mpya kubwa kuliko MV VICTORIA itakayo rahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria kutoka Bukoba kwenda Mwanza.Nakumbuka alishangiliwa sana na wananchi wa Bukoba.Swali ni je,mchakato wa ujenzi wa Meli hii unaanza lini kwa sababu hata dalili hazionekani?

Hivi ulifikiri ni kweli? pole sana.
 
Usiogope meli itakuja mkuuu ccm ikiahidi lazima inatimiza ahadi
 
CCM sio chama cha siasa,ni kikundi tu cha MATAPELI!
 
Ule ni usanii kama kawaida yao,magamba unawajua unawaskia???Matamanio yao ni madaraka tu ili waweze kutuibia zaidi na zaidi huku wakituacha bila hosptal,shule,chakula na hata usafiri wa uhakika kama huo wa meli si ulisikia eti yule wanayejivunia kuwa ni mchapa kazi wao namba 1 alisema huku kigamboni tupige mbizi???Ninafikiri huko pia mbizi zinawahusu.
 
Hiyo ilikuwa sound tu mkuu kwa ajiri ya kupata kura, haina tofauti na Lowasa anavyowagawia hela makanisani na misikitini, pia kugawa pikipiki kwa waendesha pikipiki. Mnarushiwa ndoano, mnaimeza, hahahahaaaaa
 
Teh teh, hiyo ilikuwa ni ahadi ya wanamtandao na sio ccm! Poleni sana wanamatoke!
 
Usiogope meli itakuja mkuuu ccm ikiahidi lazima inatimiza ahadi

A cha kupiga kelele mbona hapa Maswa alituahidi kutupatia maji ya bomba yanayotoka Mwanza kwenda Shinyanga yangeletwa hapa kabla ya 2010 lakini Whollaaaaa
 
Katika kampeni za urais za mwaka 2010,mgombea urais kupitia ccm J.Kikwete alipokuwa akihutubia katika mkutano wa kampeni uliifanyika katika uwanja wa uhuru(Mashujaa) Bukoba. Alitoa ahadi ya Kujengwa kwa meli mpya kubwa kuliko MV VICTORIA itakayo rahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria kutoka Bukoba kwenda Mwanza.Nakumbuka alishangiliwa sana na wananchi wa Bukoba.Swali ni je,mchakato wa ujenzi wa Meli hii unaanza lini kwa sababu hata dalili hazionekani?

Hii ni moja tu kati ya yale yaliyomo katika ahadi za Mheshimiwa Rais wetu Dr Kikwete kama zinavyobaininshwa katika vianzio mbalimbali vya habari, bofya na usome:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...hadi-za-kikwete-kwa-wananchi-2010-2015-a.html

http://www.mwananchi.co.tz/Makala/T...uke-zigo-la-ahadi/-/1597592/1997896/-/q5vur3z
/-/index.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ke-hazitekelezeki-mpaka-kufikia-2015-a-2.html

http://www.-----------.co.tz/ahadi_za_kikwete_‘bomu’ 

https://twitter.com/JamiiForums/status/28867011294
 
Back
Top Bottom