...CCM ni chama cha Nyerere
Hivi ccm ni ya kijamaa?Au ni ya kibepari?Je ni chama cha wakulima au wafanyabiashara?Kwa sababu hawa watu siwaelewi kabisa,kama waliachana na sera ya ujamaa walichukua sera ipi?Kawa walia sera ya kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi je kimekuwa chama cha nani?Ccm ndo ina wabunge wengi,hivyo ndo inaunda serikali kama ccm haieleweki sera yake inamaana serikali nayo pia haieleweki hata watu wa nje ya nchi hawaijui Tanzania ni nchi ya aina gani,Nape ni katibu uenezi wa ccm,huyu mtu anaeneza nini?Watu wa ccm naombeni majibu
Ibara ya 4(3) ya Katiba ya CCM inasema kuwa "Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba Ujamaa na Kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru." Ibara ya 5(3) inasema "kwa hiyo Malengo na Madhumuni ya CCM yatakuwa" ni pamoja na "Kuhimiza ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea kwa mujibu wa Azimio la Arusha."
Je huo ujamaa wa ccm upo wapi,je ujamaa unaruhusu watu kujirundikia mali kama walivyofanya Ridhiwan,Mkapa,Sumaye?Je ujamaa unaruhusu ufisadi kama wa dowans,richmond,epa,meremeta,kagoda,iptl..... akhhh kwanza nahisi hasira nikikumbuka hayo yote,ndugu hebu jaribu kuwa muungwana na nchi yako!!