CCM na itikadi ya ujamaa na kujitegemea

maulaga

JF-Expert Member
Feb 22, 2009
472
120
Nimestushwa na kushangazwa sana na kauri ya katibu mkuu mpya wa CCM bwana Wilson Mukama aliyoitoa akiwa Zanzibar akidai CCM ina itikadi ya ujamaa na kujitegemea na kutangaza ati CHADEMA hawana itikadi. Hivi kweli Mukama hajui kwamba itikadi ya ujamaa na kujitegemea iliuwawa hukohuko Zanzibar miaka ya 1990 kwakuliua Azimio la Arusha na kuruhusu ubepari wa kikasino kwa viongozi wa CCM kukusanya na kulimbikiza mtaji kwa njia yoyote ikiwemo ufisadi na kualika wawekezaji uchwara kutoka nje kuja kupora rasilimali zetu? Jamani, kumbe Makamba alikuwa bora kuliko hii takataka. Poleni sana wana CCM maana mmeletewa upupu utakao wawasha mpaka mfe.
SOURCE; Taarifa ya habari ITV saa mbili usiku (18.04.2011)
 
Nami pia nimwona alipokuwa anatema pumba hizo.
Makamba nafuu
 
Sioni hata chembe moja ya 'Ujamaa na kujitegemea' kwenye utendaji wa ccm. Unless wanaunza kesho. Shida ujamaa na uwekezeji mara nyingi havipatan. Confussion!
 
Can you spell.....uh..CHINA?
 
Huku ni kuwatukana wananchi bila aibu! Anaongea kwa tambo eti ccm inafuata itikadi ya ujamaa na kujitegemea na kudai chadema haina itikadi halafu watu waliovaa nguo za kijani wanamshangilia na kumpigia makofi na vigeregere.. Kwanza dhana ya ujamaa na kujitegemea iko kwenye katiba ya JMT sura ya kwanza yenye kichwa cha habari "JAMHURI YA MUUNGANO, VYAMA VYA SIASA, WATU NA SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA. Sasa sielewi kama serikali iliiba itikadi hii kwa ccm au ccm iliiba kutoka serikalini. Au kwa kuwa tanzania ilikuwa na chama kimoja basi itikadi ya chama ilikuwa pia itikadi ya serikali. Pili ccm inajua wazi kwamba chama hicho sasa kinafuata itikadi ya ubepari ndio maana chama kimejaa mabepari wengi wakiwemo wafanya biashara lukuki ambao wengine ni wabunge lakini katibu mkuu mteule wa ccm anaongea bila aibu na kusema ccm inafuata itikadi ya ujamaa na kujitegemea na kuhoji chadema wana itikadi gani!!! Kweli ccm watamkumbuka makamba. Mkama hana jipya lolote.
 
Kobello,
kama umekuwa ukifuatilia vizuri utakumbuka kwamba China na hata USSR wakati huo hawakuwahi kuubali Ujamaa wa Tanzania. Kwa Tz ni more of African Socialiam na ulikuwa (nisisitize- ulikuwa) more inward looking kwa maana kwamba kama Taifa lilizingatia sana solution kutoka ndani kuliko nje na ndio kukawa na 'kujitegemea'. Sasa hivi ujamaa wa kibakuli huku viwanda vimekufa sioni hata mantiki yake.
 
Huwezi ukaongozwa kwa kisu na uma kwa kula halafu ukasema ni ujamaa na kujitegemea. Mpeni pole kwani hajui alisemalo!
 
Nimestushwa na kushangazwa sana na kauri ya katibu mkuu mpya wa CCM bwana Wilson Mukama aliyoitoa akiwa Zanzibar akidai CCM ina itikadi ya ujamaa na kujitegemea na kutangaza ati CHADEMA hawana itikadi. Hivi kweli Mukama hajui kwamba itikadi ya ujamaa na kujitegemea iliuwawa hukohuko Zanzibar miaka ya 1990 kwakuliua Azimio la Arusha na kuruhusu ubepari wa kikasino kwa viongozi wa CCM kukusanya na kulimbikiza mtaji kwa njia yoyote ikiwemo ufisadi na kualika wawekezaji uchwara kutoka nje kuja kupora rasilimali zetu? Jamani, kumbe Makamba alikuwa bora kuliko hii takataka. Poleni sana wana CCM maana mmeletewa upupu utakao wawasha mpaka mfe.
SOURCE; Taarifa ya habari ITV saa mbili usiku (18.04.2011)

Inawezekana ni kweli kuwa itikadi ya CCM ni UJAMAA na KUJITEGEMEA. Ila inabidi tueleweshwe huu ujamaa na kujitegemea una maana gani katika mazingira ya CCM ya sasa. Kwani huu walionao siyo ujamaa kama ukiupima kwa kipimo cha ujamaa aliokuwa akihubiri muasisi wa CCM (Nyerere).

Kwa mtazamo wangu UJAMAA kwa muktadha wa CCM mamboleo una maana ya kurithishana nafasi za uongozi wa chama na serikali kwa JAMAA na marafiki wa karibu wa viongozi wa sasa na wastaafu. KUJITEGEMEA kwa muktadha wa CCM mamboleo kuna maana ya kufanya maamuzi ya kifisadi yanayoliingiza taifa katika madeni na hasara, kwa kujitegemea, bila kuwashirikisha wananchi na wawakilishi wao bungeni.
 
Msameheni kwani hajui atendalo maana anaonekana pia kama vile si mwenzao hata alipoteuliwa hakuwa na magwanda ya kijani
 
Ni kweli CCM inarudisha siasa ya ujamaa na kujitegemea ndio maana inawatimua mafisadi wote.
Nimestushwa na kushangazwa sana na kauri ya katibu mkuu mpya wa CCM bwana Wilson Mukama aliyoitoa akiwa Zanzibar akidai CCM ina itikadi ya ujamaa na kujitegemea na kutangaza ati CHADEMA hawana itikadi. Hivi kweli Mukama hajui kwamba itikadi ya ujamaa na kujitegemea iliuwawa hukohuko Zanzibar miaka ya 1990 kwakuliua Azimio la Arusha na kuruhusu ubepari wa kikasino kwa viongozi wa CCM kukusanya na kulimbikiza mtaji kwa njia yoyote ikiwemo ufisadi na kualika wawekezaji uchwara kutoka nje kuja kupora rasilimali zetu? Jamani, kumbe Makamba alikuwa bora kuliko hii takataka. Poleni sana wana CCM maana mmeletewa upupu utakao wawasha mpaka mfe.
SOURCE; Taarifa ya habari ITV saa mbili usiku (18.04.2011)
 
Nimestushwa na kushangazwa sana na kauri ya katibu mkuu mpya wa CCM bwana Wilson Mukama aliyoitoa akiwa Zanzibar akidai CCM ina itikadi ya ujamaa na kujitegemea na kutangaza ati CHADEMA hawana itikadi. Hivi kweli Mukama hajui kwamba itikadi ya ujamaa na kujitegemea iliuwawa hukohuko Zanzibar miaka ya 1990 kwakuliua Azimio la Arusha na kuruhusu ubepari wa kikasino kwa viongozi wa CCM kukusanya na kulimbikiza mtaji kwa njia yoyote ikiwemo ufisadi na kualika wawekezaji uchwara kutoka nje kuja kupora rasilimali zetu? Jamani, kumbe Makamba alikuwa bora kuliko hii takataka. Poleni sana wana CCM maana mmeletewa upupu utakao wawasha mpaka mfe.
SOURCE; Taarifa ya habari ITV saa mbili usiku (18.04.2011)

Unashtuka nini, hawa ni debe tupu:A S 465:
 
Njaa mbaya!!

mzee amekaa bench muda mrefu sana anakuja na spidi ya ajabu, tutamkumbuka hata Makamba
 
Hawawezi kuhutubia bila ya kuitaja CDM,tunawashukuru kwa kuzidi kutukumbusha kwamba kipo na kinazidi kuwanyima usingizi..
 
kweli duniani kuna mambo! nami nilimsikia akihutubia Zanzibar, kumbe CCM hawana watu makini. Kumbe huyu jamaa aliyemrithi makamba anapumba kuliko yule wa kwanza!!!

SSM NAWAPA POLE HAMNA KITU KWENYE VIONGOZI WENU, NI PUMBA KWA KWENDA MBELE,

MASIKINI CCM!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!, NAONA HAKUNA ATAKEYE INUA HIKI CHAMA, WOTE VICHWA MAJI!!!, NDO MAANA NCHI IMEFIKISHWA HAPA. HIVI KWELI KATIBU MKUU MPYA ALIKUWA NDANI YA NCHI HII KWA MIAKA 20 ILIYOPITA?????????? MI NAONA KIZUNGUZUNGU KWA CCM.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom