CCM na Dr Makongoro Mahanga ni utapeli tena kwa Wananchi- Malipo Airport Dar ?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na Dr Makongoro Mahanga ni utapeli tena kwa Wananchi- Malipo Airport Dar ??

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Not_Yet_Uhuru, Oct 26, 2010.

 1. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  :A S cry:
  Haya ni masikitiko sana kwa jinsi Wananchi wa taifa hili wanavyofanywa mazuzu na mbumbumbu kila uchao na viongozi hawa wa CCM na wananchi wenyewe hawajijui wala kujitambua kuwa wanaangamia!

  Makongoro Mahanga
  na CCM yake wamekuwa wakiwahadaa wananchi walio kando ya Uwanja wa Ndege wa Dar - maeneo ya Kiwalani, Kigilagila na wengine walio katika kuvunjiwa nyumba zao kuwa WATALIPWA KABLA YA KUFANYIKA UCHAGUZI MKUU...ikiwa ni geresha na mbinu ili waipe CCM na Mahanga kura...KUMBE WOTE WAMEDANGANYIKA, HADI LEO HII BADO WANASUBIRIA MALIPO, ZIMEBAKI SIKU 3...HAKUNA MALIPO YOYOTE! WANANCHI WAMELIWA TENA NA UTAPELI HUU WA CCM! Poleni sana wananchi wanyonge wa Mungu, mmeliwa tena...hii hatari sana! Subirini watawajia na kiswahili kingine kilichopambwa! Hela za Kampeni zenyewe CCM wamezuia malipo ya wafanyakazi serikalini sembuse wanyonge nyie hamna mbele wala nyuma!

  Angalizo:
  Mkiona alama yoyote ya CCM au hata Mgombea wake mnatakiwa mkimbie kama mmekutana na ukoma!


   
Loading...