Uchaguzi 2020 CCM na CHADEMA tupeni raha kesho tarehe 27/10/2020

Mtukudzi

Senior Member
Nov 14, 2013
103
408
Kesho ni siku muhimu sana kwa vyama miamba wa nchi hii. Ni siku ya kufunga kampeni za uchaguzi mkuu wa 2020.

Mpaka leo hatuwezi kusema nani atashinda au nani atashindwa. Hali hiyo inathibitisha maneno aliyowahi kusema bwana Mbowe kuwa, "siasa ni dynamics."

Bandiko langu hili naliweka muda huu kuomba vyama vyetu hivi viwili vijitafakari kila chama kwa nafasi take kinapoelekea kufunga kampeni zake.

CCM
Siyo siri chama cha Mapinduzi wamefanya kampeni nzuri na hakika wamepata coverage nzuri upande wa media. TBC mpaka ninapoandika wapo kazini kuonyesha mazuri ya CCM. Siku zote za kampeni TBC achilia mbali TV ya CCM(Channel 10) imefanya kazi kubwa kwa ajili ya CCM. Kwa hiyo CCM kesho wekeni ulafi pembeni achia hata TV moja binafsi( ITV, StarTV au CloudsTV) ionyeshe ufungaji wa kampeni za CHADEMA.

CHADEMA
CHADEMA mmefanya kampeni za level nyingine kabisa. Awali ilikuwa kwamba mnaenda kwenye uchaguzi mkiwa mmeshindwa tayari. Zile dynamics za siasa mmetendea haki. Mgombea wenu ameiva ndiyo maana huku mtaani anaitwa "nusu MTU nusu chuma". Bila kuambatana na Mbowe ambaye amekabwa kwelikweli huko jimboni, Bw. Lissu amefufua matumaini ya watu waliozaliwa kuwa Wapinzani.

Kwa kuwa kesho ni siku ya kufunga kampeni tafadhali ingia gharama mkalipie TV ya kuonyesha shughuli yenu. Tunataka mnaingia kwenye chumba cha kupiga kura mkiwa mmetuthitishia kuwa mnaweza kulipia TV ukizingatia kuwa chama chenu kina ruzuku na kipindi chote cha kampeni mmechangisha pesa kwa ajili ya kampeni.

Hitimisho:
Watanzania twende tukapige kura.
 
Huwezi kuwa na akili nzuri na kuwasifu ccm kwa eti kwa kampeni nzuri, wakati wamepoka vyombo vyote vya habari, vyombo vya dola na kuwazimia wapinzani tv, redio na magazeti! Mgombea wa ccm ametumia nafasi yake kutoa maagizo wakati wa kampeni kinyume kabisa na sheria! N.K.

Nawasifu CHADEMA kwa uvumilivu na ushujaa mkubwa pamoja na matatizo na dhuluma zote wamevuta mamilioni ya watz kuliko ccm!
 
Back
Top Bottom