CCM na CHADEMA nusu wazipige Arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na CHADEMA nusu wazipige Arumeru

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Mwanajamii, Mar 8, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]CCM, Chadema youth nearly fight [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 07 March 2012 22:24 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]By The Citizen Correspondent
  Arumeru.
  The presence of three opposition MPs at a funeral at Migungani, Mbuguni Ward in Arumeru District, Arusha Region nearly triggered a brawl between CCM and Chadema supporters.Supporters of the two parties came close to a fight on Tuesday after three Chama Cha Demokrasia na Maendeleo MPs accompanied the party’s parliamentary candidate for the Arumeru East by-election, Mr Joshua Nassari to the funeral.

  The Chadema legislators have pitched a camp in the constituency whose seat was left vacant by the late Jeremiah Sumari of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM). The Chadema lawmakers were Vincent Nyerere (Musoma Urban) who is the campaign manager, and Special Seats MPs, Rose Kamili (Manyara Region) and Rebecca Mgodo (Arusha Region).

  The delegation of Chadema MPs arrived at the scene shortly before the body of the deceased, Viola Gimosa, was brought from Mount Meru Hospital escorted mostly by Tanzanite small-scale miners from Mirerani.

  The misunderstanding started when CCM supporters started to inquire who had invited the Chadema legislators to the funeral.At this juncture, a group of Chadema youths stood up and declared that traditions demand that people do not have to be invited in a funeral.

  my take:siasa isitugawe,tuzikane tusaidiane kama watanzania[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,800
  Likes Received: 17,885
  Trophy Points: 280
  it wud be better if u came up with full translation, to be great thinkers doesnt mean we're good in English,and am among of them, i will make some comments if i find it in ma mother tongue
   
 3. SAMMY DANNY

  SAMMY DANNY Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  you information is interesting and politics sasa imefika pabaya hata katika misiba! we need political torrelance between the parties.
   
 4. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hv hao supporters wa magamba wanazo kichwani kweli?msiba uwa una mualiko hasa kwa tamaduni zetu za kiafrika? Kutenda bila kufikiri ni tabu sana
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wednesday, 07 March 2012 19:27

  Moses Mashalla na Mussa Juma, Arumeru
  WAKATI hekaheka za kuwania ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki zikizidi kushika kasi, wabunge wa viti maalumu kwa tiketi ya Chadema; Rebecca Mgondo na Rose Kamili, wamemshutumu kigogo mmoja wa CCM (jina linahifadhiwa) kutokana na kile wanachodai ameanza mchezo mchafu wa kununua shahada za kupigia kura katika jimbo hilo.

  Wabunge hao walitoa tuhuma hizo juzi wakati walipotembelea ofisi za Chadema Kata ya Mbuguni na kudai kuwa kigogo huyo tayari ameshaanza kutembea maeneo mbalimbali kuwashawishi wapiga kura wa jimbo hilo wamuuzie shahada zao.

  Kamili alidai kuwa kigogo huyo wa CCM tayari ameshaonekana maeneo ya Tengeru na Usa River akinunua shahada za kupigia kura kitendo ambacho hakivumiliki.

  Kamili alisema tayari ameshampigia simu kigogo huyo na kumwonya juu ya mchezo huo akisema hawatakubali kuona vitendo hivyo vinafanyika wilayani Arumeru.

  "Nilimpigia simu nikamwambia mwanangu (akamtaja jina), mbona unafanya vitendo hivi? Akanijibu kwamba mama kwa nini hili jimbo msimwachie kijana akaendeleza yale yaliyoachwa na mzee? Hii ni ajabu!" alisema

  Alituhumu kigogo huyo kwamba amekuwa akinunua shahada hizo kwa Sh50,000 kwa zile zilizo mikononi mwa wafuasi wa Chadema na Sh5,000 kwa shahada zilizo mikononi mwa wafuasi wa CCM.

  Alimshangaa kigogo huyo ambaye ni kijana ndani ya CCM kwa kununua shahada hizo huku akisisitiza kwamba, endapo angekuwa na nia ya kuwasaidia wakazi wa jimbo hilo angetoa fedha hizo kununua vifaa vya hospitali na zahanati mbalimbali zilizopo wilayani humo.

  "Jamani hamshangai kama huyu (anamtaja tena jina lake) angekuwa na nia ya dhati kuwasaidia si hizo fedha angenunulia vifaa vya hospitali? Lakini ananunua shahada halafu uchaguzi ukimalizika mnarudishiwa,!" alisema mbunge huyo.

  Aliwasihi€wakazi wa jimbo hilo kutokubali kuuza shahada zao kwa kuwa watakuwa wamepoteza haki yao ya msingi ya kupiga kura sanjari na kuuza utu wao.

  Takukuru
  Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Arusha, Mbengwa Kasumambuto alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo alisema hazijamfikia ofisini na kuomba muda ili aweze kuzifuatilia kabla ya kuzitolea ufafanuzi.

  Kasumambuto aliwashauri waliotoa tuhuma hizo kufikisha madai yao mbele ya ofisi hizo ili zifanyiwe kazi kuliko kulalamika ovyo.

  Katibu wa CCM Wilaya ya Arumeru, Ole Saivoy alikataa kuzungumzia madai hayo kwa simu.

  Chadema msibani
  Katika hatua nyingine, wabunge watatu wa Chadema, ambao walikuwa wameambatana na mgombea wa ubunge wa chama hicho katika Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, juzi walichafua hali ya hewa baada ya kushiriki katika msiba wa kada wa CCM Viora Gimosa katika eneo la Migungani, Kata ya Mbuguni.
  Wabunge hao ambao wameweka kambi katika jimbo hilo ni pamoja na Meneja wa Kampeni, Vincent Nyerere (Musoma mjini), Kamili na Mgodo.
  Ujumbe wa wabunge hao, uliwasili msibani hapo mchana, muda mfupi baada ya mwili wa marehemu Gimosa kuwasili kutoka Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru ukisindikizwa na idadi kubwa ya magari ya wachimbaji wadogo wa madini ya tanzanite, Mererani.
  Baadhi ya ndugu wa wafiwa na makada wa CCM walianza kuhoji aliyewaalika wabunge hao na mgombea wao kwenye msiba na kujibiwa na kundi la vijana wa Chadema ambali lilisema msibani haalikwi mtu.

  Mmoja wa vijana hao, John Ezekiel alisema mgombea huyo wa Chadema, hata kabla ya kuteuliwa kuwania kiti hicho, amekuwa akihudhuria misiba bila kualikwa kwani kwa kawaida penye msiba hakuna mialiko.

  Hata hivyo, hali hiyo ilionekana kutowafurahisha baadhi ya wanaCCM ambao walilazimika kumwita mgombea wa ubunge wa CCM, Siyoi Sumari afike kwenye msiba huo lakini jitihada za kumpata kupitia kwa wasaidizi wake zilikwama hadi mazishi yalipokamilika.

  "Mimi nilihisi kuwa Chadema watakuja hapa kwani wanajua watu wengi watafika. Nilipiga simu kwa wasaidizi wa Siyoi ili wamlete kabla ya kuondoka chumba cha kuhifadhi maiti na wakaahidi atakuja lakini, nadhani wameshindwa" alisema mmoja wa ndugu wa wafiwa, Hussein Mkodo.

  Mkodo ambaye alipata wakati mgumu kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CCM kutokana na kutuhumiwa kuhusika kumwita mgombea wa Chadema, alilazimika kujieleza mara kadhaa kwa makada wa CCM kuwa yeye si Chadema na kwamba ni CCM damu.

  "Mimi ni mwanachama hai wa CCM , Arusha wote wananijua na ndiyo sababu sielewani hata na Lema (Mbunge wa Arusha Mjini) kwa kuwa mimi nilikuwa namuunga mkono Dk Batilda Burian wakati wa uchaguzi uliopita," alisema Mkodo.

  Wakizungumza katika eneo hilo la msiba, Diwani wa Mbuguni (CCM), Thomas Mollel maarufu kama Askofu na Diwani wa Mererani Mererani (CCM), Justin Nyari, waliwasihi wanaCCM waliofika hapo kutokuwa na hofu juu ya ujio wa Nassari kwani wana uhakika msibani hakuna kura za kumpa ushindi.

  Mollel ambaye ni mfuasi mkubwa wa Siyoi alisema haikuwa rahisi kwa Sumari kufika katika msiba huo kwani alikuwa amechukua fomu asubuhi.
  "Jamani Sumari amechukua fomu leo tu na mnajua kuna taratibu za kutafuta wadhamini na kujaza fomu na kurejesha, hawezi kufika hapa, mimi nimemwakilisha," alisema Mollel.

  Wabunge hao wa Chadema, walikaa msibani na kushiriki mazishi hayo ambayo yalifanyika katika makaburi ya kijiji hicho.
   
 6. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  CCM hawajui ule msemo unaosema LIENI NA WANAOLIA na FURAHINI NA WANAOFURAHI..
   
 7. R

  Real Masai Senior Member

  #7
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hujaelewa nini hapo..Acha ushabiki huo ndo ukweli..Siasa zisitugawe, kwani kwenye mazishi mtu unaalikwa au unaudhuria kwa utamaduni wa kitanzania..
   
 8. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Hili la shahada inabidi liangaliwe upya. uwekwe utaratibu utakaomuwezesha mpigakura halali kupiga kura hata kama shahada yake amemkabidhi Mwigulu.
   
 9. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,800
  Likes Received: 17,885
  Trophy Points: 280
  kaka co ushabiki, hii post ni nzuri na kidogo nimeelewa kupitia comments, and not post itself, am not good in english brother, can u tel me why the post has very few comments til now, it's the matter of language.here in JF we're not all versity graduates, others we are just 4m4 police officers, tumenyimwa elimu ila tumepewa kazi nzito ya kuzuia CDM na vuguvugu lake, hii kazi inatuwia vigumu sana,kwani hata sisi tuna mapenzi makubwa na CDM
   
 10. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mazishi hayana mwaliko
   
 11. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  wanamagamba wanafikra mgando sana
   
Loading...