CCM na CCJ yake, CHADEMA na ACT Yao: Je, Historia Itafuata Mkondo au Itachepuka?

mkuu NazDaz,umeongea jambo la msingi kabisa,lakini kwa watu wasiotumia kichwa kufikiri,lazima wataleta kebehi nyingi sana.
Kama ulivyoeleza hapo juu,CDM wakiacha mambo haendelee kama ilivyo kwa hawa watu wasioongozwa na busara na hekima kuendelea kuropoka,itawagharimu sana kuliko vile walivyokua wanafikiri,lakini swali la msingi ni je mpaka sasa hata wakiamua kufuata ushauri wako,watakuwa hawajachelewa kweli?
 
CHADEMA sio sawa na CCM
CCM wana dola....wanatoa ajira serikalini
ndo maana kina Nape wakapewa ukuu wa wilaya na mwisho wakarudishwa kundini
kna Mwakyembe na Sitta wamepewa uwaziri

CHADEMA hawako in power...hawana nguvu ya kumshughulikia mtu that much
sanasana wakijifanya 'bize kuishughulikia ACT' itawa cost muda na pesa pia...

Kama Zitto akifanikiwa kupata wabunge kadhaa na ACT..
na CHADEMA wabunge wakipungua...most likely after uchaguzi wanaweza kuwa vyama sawa kwa nguvu
hakuna mkbwa wala mdogo......while CCM watakuwa still the power it is..

Unadhani kama ni hawa hawa Chadema wangekuwa wako madarakani wangempa ukuu wa wilaya Nape au wangemfukuza kwenye chama?
 
Kilichofanya CCM isitetereshwe na CCJ ni kutumia nguvu zake za dola na wala sio viongozi wa CCM kama unavyodanganya hapa. Kuanzia usalama wa taifa, polisi na msajili wa vyama, ofisi ya bunge, wakuu wa mikoa na wilaya walitumika kuhujumu CCJ. Halafu unasema ATC ni tishio kwa Chadema... tishio lake liko wapi na Chadema haina dola? Kwanini isiwe tishio kwa CCM yenye Dola? Huoni mna lenu jambo na jambo lenyewe ni kuhujumu upinzani? Nina taarifa zote na jinsi Zitto alivyoahidiwa uwaziri mkuu pindi Lowassa akishika madaraka. Nina taarifa jinsi Kikwete na Lowassa wanvyochezea watu akili ili ionekane kama wamekosana kumbe anamuunga mkono kwa kila jambo analofanya.

Zitto kuwa PM?.....nitashangaa sana!.....kweli hii nchi ni ya Hovyo!...ni bora hata kibaji Lusinde asie kuwa na Shule awe PM kuliko Zitto,

sina kuchi na Zitto, zitto kichwani yupo vizuri sana sana, ila Zitto amekosa Busara na Hekima.
 
kitakachoiangamiza chadema(though i pray for that) ni kuwa na idadi kuuubwa ya wajinga kama wewe. hakuna haja ya kujibizana na mwehu wa aina yako. kimsingi ni kuwaacha ninyi wafu mzikane.
 
Mkuu Kituko, samahani kwa kuchelewa kujibu... unajua tena na pilikapilika za asubuhi!

Kimsingi ulichosema, ndicho ninachomaanisha lakini sikutaka kuingia ndani! Sikutaka kutumia active sentence kwa kitu nisicho na ushahidi nacho na ndio maana nikaishia kusema:
Nashawishika kuamini kwamba, hata hatua ya Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya uhakiki wa wanachama dakika za majeruhi, ilikuwa ni moja ya mikakati hiyo ya chini chini! Inawezekana kabisa Wazee wa Kazi (TISS) walipewa kibarua cha ku-assess nguvu ya CCJ na wakagundua kwamba hawakuwa na wanachama waliodai kuwa nao! Lakini hata kama waligundua miezi kadhaa au hata mwaka kabla ya uchaguzi mkuu, CCM na vyombo vyake wakaamua kusubiria wakati muafaka wa kuichinjia baharini CCJ! Muda muafaka ni ule ambao wasingepata tena muda wa kukusanya nguvu!
Na hatimae nikasema wazi kwamba, kwa kuwa CCJ ilikuwa ni threat kwa CCM basi vyombo vya serikali vingeweza kufanya chochote lakini so long ACT inaonekana kuwa ni threat kwa CHADEMA, basi hakuna chombo cha serikali kitakacho-act against ACT!

Lakini pamoja na yote hayo, bado naamini kwamba utulivu wa CCM nao ulisaidia, sio kuipasua pasua CCJ bali kutokipasuapasua chama! Kwa jinsi CHADEMA walivyo, tuhuma zile za wazi dhidi ya akina Mwakyembe ingekuwa ndo upande wa CHADEMA, lazima wangetimuana timuana badala ya kutuliza akili na ku-solve matatizo kisayansi! Tukubali tusikubali, kwenye siasa hususani hizi za Afrika kunakuwa na watu ambao wanakuwa na influence kubwa kwenye chama! Nguvu ambazo alikuwa nazo Mrema 1995 kama isingekua Baba wa Taifa kupita huku na kule kumpigia debe Mkapa, basi huenda mambo kwa CCM mwaka ule yangekuwa mabaya kuliko ilivyokuwa imetokea! Kutokana na ukweli huo, measure za ku-deal na mtu kama Dr. Slaa kamwe haziwezi kuwa sana na measure za ku-deal na Diwani wa Mabogini! Unapotaka ku-deal na Dr. Slaa unatakiwa kuwa mwangalifu zaidi kuliko unavyotaka ku-deal na mtu mwingine kwa sababu, tukiacha siasa pembeni, mtu kama Dr. Slaa anao ubavu wa kuibomoa CHADEMA na ikachukua muda ku-recover! Na mbaya zaidi, muhimili wa CHADEMA upo mikononi mwa watu zaidi kuliko wanachama na watu wanaoshikilia mhimili huo ni wachache zaidi ukilinganisha na wanaoshikilia muhimili wa CCM!

Hata hivyo, hii haimaanishi kwamba watu wenye ushawishi wakikosea ndo basi wasiadhibiwe bali hatua yoyote dhidi yao haitakiwi kuchukuliwa kwa jazba wala papara! Wakati mwingine kwenye siasa kinachotawala ni majungu zaidi kuliko uhalisia! Na always, timua timua sio kigezo cha uongozi kuwa bora au kutofumbia macho uovu bali timua timua ni one type of the management failure!
 
Last edited by a moderator:
Zitto kuwa PM?.....nitashangaa sana!.....kweli hii nchi ni ya Hovyo!...ni bora hata kibaji Lusinde asie kuwa na Shule awe PM kuliko Zitto,

sina kuchi na Zitto, zitto kichwani yupo vizuri sana sana, ila Zitto amekosa Busara na Hekima.
Hizo ni porojo tu kwahiyo zisikuumize kichwa coz' hata katiba yenyewe hairuhusu jambo hilo unless kama wanataka kutuambia Zitto anaenda CCM!
 
Utulivu na ustahimilivu ni tunda la busara wakati funika kombe ni tunda la kuficha au ku-entertain uovu... haya hayawezi kuwa mambo yaliyo sawa!

Kuanzisha Chama kwa Siri ukiwa ndani ya Chama ni Usaliti na wala sio Busara.
Ni Sawa na Kufunga ndoa Nyingine ukiwa Ndani ya Ndoa still
 
Kuanzisha Chama kwa Siri ukiwa ndani ya Chama ni Usaliti na wala sio Busara.
Ni Sawa na Kufunga ndoa Nyingine ukiwa Ndani ya Ndoa still
Sasa mbona unachanganya mambo? Sijasema Sitta na wenzie walifanya jambo la busara kwa kuwa na mafungamano na chama kingine wakati wakiwa ndani ya chama kingine! Waliofanya busara ni CCM na uongozi wake kwa kufahamu ni namna gani wanaweza ku-handle situation kama hizo! Hapa tunazungumzia namna ya ku-manage matatizo na sio ku-deal na matatizo! In ordinary customer care, people talk on "how to deal with difficult customers" but in professional customer care we don't talk on "how to deal with difficult customers" but we talk on "how to handle difficult customers!"
 
Hicho anachokisema mtoa mada kama "busara" za CCM a.k.a yake ni unafiki. Kama Chadema wangeiga hii "busara" ya CCM, that would be it (kwishney kwa Chadema).

Hii ni turning point ya Chadema going forward. Chadema must position themselves differently towards October 2015 and beyond. CCM is a failed institution na hakuna chochote cha kuiga kule.
 
kitakachoiangamiza chadema(though i pray for that) ni kuwa na idadi kuuubwa ya wajinga kama wewe. hakuna haja ya kujibizana na mwehu wa aina yako. kimsingi ni kuwaacha ninyi wafu mzikane.

Ebo umeshajibizana tena na mwehu halafu unasema ''hakuna haja kujibizana na mwehu'' Mwehu ni nani sasa kati yetu! Lesson number one: Ukiona mgonywa wa ukurutu anaguna baada ya kupakwa dawa ujue imemwingia kunakostahili!
 
mkuu NazDaz,umeongea jambo la msingi kabisa,lakini kwa watu wasiotumia kichwa kufikiri,lazima wataleta kebehi nyingi sana.
Kama ulivyoeleza hapo juu,CDM wakiacha mambo haendelee kama ilivyo kwa hawa watu wasioongozwa na busara na hekima kuendelea kuropoka,itawagharimu sana kuliko vile walivyokua wanafikiri,lakini swali la msingi ni je mpaka sasa hata wakiamua kufuata ushauri wako,watakuwa hawajachelewa kweli?

''Ikiwagharimu'' si ndio furaha yako mazee! Au wewe ulizaliwa kuikomboa Chadema! Hamjui hata kuficha hisia zenu! Mabwana zenu waliowatuma nafuu wangetuma ngedere wana maarifa kuliko ninyi
 
Sasa mbona unachanganya mambo? Sijasema Sitta na wenzie walifanya jambo la busara kwa kuwa na mafungamano na chama kingine wakati wakiwa ndani ya chama kingine! Waliofanya busara ni CCM na uongozi wake kwa kufahamu ni namna gani wanaweza ku-handle situation kama hizo! Hapa tunazungumzia namna ya ku-manage matatizo na sio ku-deal na matatizo! In ordinary customer care, people talk on "how to deal with difficult customers" but in professional customer care we don't talk on "how to deal with difficult customers" but we talk on "how to handle difficult customers!"
Mabwana zenu waliowatuma wana hasara kubwa! Hamwezi kuficha chuki zenu kwa Chadema hata mnapojifanya kutoa ushauri nasaha wenu!
 
Una akili sana wewe, nimeupenda uchambuzi wako wa kina.

Habari kaka NasDaz,

Nadhani kuna utofauti Mkubwa sana kati ya CCJ na ACT, japo vina fanana kwa minajili ya kuwa vimetokana na wanachama waliotoka kwenye Vyama vyao na kuunda hivyo vyama

Nadhani kabla ya kufanya uchambuzi wa hivyo vyama ni muhimu kuijua CCM na Nguvu zake

Serikali ya CCM ndio inayo control Police, TISS, NEC na Msajili wa Vyama vya siasa, CCJ kilikuwa ni Chama cha kweli na kilikuwa ndio anguko kuu la CCM, Watu kama Mwakyembe, Nnape, Sitta, Mpendazoe na wengine walishajipanga vizuri nadhani wakiwa na back up ya kina Warioba na wenzie (Butiku, Salim, ect),
CCM kwa kuiona hiyo hatari kupitia labda TISS yake, walitumia rungu la Msajili wa Vyama vya siasa kui-disqualify CCJ kwamba haijatimiza sharti la kuwa na wanachama nchi nzima, Na huo ndio ulikuwa Mwanzo wa mwisho wa CCJ huku watu kama Mpendazoe wakisha jitumbukiza shimoni

Kwa Upende wa ACT ni tofauti, Vyombo vilivyotumika kuiangusha CCJ ndio vinatumika kuiinua ACT
Chama Cha ACT kina mapungufu makubwa ya kiusajili ambayo yako wazi sana, lakini Msajili wa vyama ameamua labda kwa kushinikizwa kukipa usajili hicho chama, Chama Hakina Katiba ya kueleweka, Hakina viongozi wa kueleweka, Hakina Bendera ya kueleweka na hakina Nembo ya kueleweka lakini kimesajiliwa na Msajili wa vyama vya siasa.

Kwa sasa Kuna kesi ya kiuongozi ndani ya ACT believe me hiyo kesi , wakina Zitto lazima washinde kwa sababu wana backup ya CCM ambayo ndio inaongoza taasisi zote muhimu nchini (Ikiwemo Mahakama) sio kwa minajiri ya kiutendaji bali Kisiasa zaidi

CCJ ilikufa kwa nguvu nilizoziainisha hapo juu,
Ila ACT itadumu mpaka mwisho wa uchaguzi wa Mwaka huu 2015 kwa sababu itabebwa na TISS, NEC, CCM na Msajili wa vyama wote wakiwa na lengo la kuiyumbisha na kuipotezea nguvu Chadema.,
Lakini baada ya uchaguzi kuanzia 2016 mpaka uchaguzi mwingine 2020 kutakuwa hakuna Chama cha ACT, chama kitakuwa kimeshakufa
 
Kwako wewe kilichoandikwa hapo ni kama hadithi ya Abunuwas, lakini huo ndio ukweli wa mambo. Inahitaji akili kubwa kuelewa kwa kina kilichoandikwa.

Kisa kakutungia hadithi upendayo kusikia? Teh teh,kwikwikwi.
 
Back
Top Bottom