CCM na CCJ yake, CHADEMA na ACT Yao: Je, Historia Itafuata Mkondo au Itachepuka?

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,136
Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, chama kipya cha kisiasa; CCJ kilianzishwa. CCJ ilikuja kwa kasi kiasi cha kuanza kuitia hofu CCM huku hofu hii ikichangiwa sana na maneno ya hapa na pale kuhusu uhusiano wa CCJ na wanasiasa waandamizi ndani ya CCM, hususani Samwel Sitta na Mwakyembe! Wengine ambao walihusishwa na CCJ ni pamoja na Nape Mnauye! Hata hivyo, ukongwe na busara za wana-CCM ukaifanya CCM kuto-panic ingawaje kulikuwa na watu waliokuwa wakihesabu siku washuhudie exodus from CCM to CCJ! Hili, halikutokea licha ya kumshudia Fred Mpendazoe akijitoa mhanga na kuwa mwana-CCM wa kwanza mwandamizi kujiunga na CCJ na wengine wakawa kana kwamba wanapima uelekeo wa upepo!

Katika hali ambayo haikutarajiwa kabisa, ikiwa imebaki miezi michache kufikia tarehe ya uchaguzi mkuu, hatimae ikaja kubainika CCJ haikuwa na wanachama kwenye sehemu mbalimbali za nchi; wanachama ambao hapo kabla ilidai kuwa nao! Wakati ambapo Msajili wa Vyama vya Siasa alikuja kufanya uhakiki huu ulikuwa ni ule ambao CCJ isingeweza tena kujikusanya upya na kuwahi uchaguzi mkuu! Huo, ukawa ndio mwisho wa CCJ, msiba ukapita na hatimae matanga kuanuliwa... kilichobaki hivi sasa ni historia!

Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015 tunashuhudia mambo yale yale ya 2010 yakitokea. Badala ya CCJ, leo hii hatuna budi kutambua uwepo wa ACT. Hata hivyo, tofauti na 2010, mwelekeo wa 2015 umethibitisha kwenda kinyume chake! Wakati CCJ ilikuwa ni tishio kwa chama tawala, ACT kinaonekana kuwa ni tishio dhidi ya chama kikuu cha upinzani; CHADEMA! Wakati tangu kuasisiwa kwa CCJ kulihusishwa na wanasiasa waandamizi ndani ya CCM, tangu kuasisiwa kwa ACT kulihusishwa na wanasiasa kutoka CHADEMA! Wakati msimu wa 2010 ilimshuhudia Mpendazoe akiwa mbunge wa kwanza kutoka CCM kujiripua, safari hii tunamuona aliyekuwa mbunge wa CHADEMA!

The question is; Je, CHADEMA na wana-CHADEMA wana uwezo wa kutulia na kuwa calm kama ilivyokuwa kwa CCM mwaka 2010? I am afraid the answer is NOT! Sina shaka hata kidogo kwamba, nusura ya CCM mwaka 2010 ilitokana na utulivu wao. Pamoja na wanachama waandamizi kuhusishwaa na CCJ lakini CCM haikuwachukulia kama maadui hadharani au wasaliti... hakuna aliyefukuzwa kwenye nafasi yake wala kukejeliwa ama iwe kwenye mitandao ya kijamii au kwenye majukwaa ya kisiasa! Kwa muda wote, CCM walichukulia yote hayo kama tetesi tu huku bila shaka wakipanga mikakati ya chini chini kuangalia ni namna gani wangenusurika na jinamizi la CCJ! Nashawishika kuamini kwamba, hata hatua ya Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya uhakiki wa wanachama dakika za majeruhi, ilikuwa ni moja ya mikakati hiyo ya chini chini! Inawezekana kabisa Wazee wa Kazi (TISS) walipewa kibarua cha ku-assess nguvu ya CCJ na wakagundua kwamba hawakuwa na wanachama waliodai kuwa nao! Lakini hata kama waligundua miezi kadhaa au hata mwaka kabla ya uchaguzi mkuu, CCM na vyombo vyake wakaamua kusubiria wakati muafaka wa kuichinjia baharini CCJ! Muda muafaka ni ule ambao wasingepata tena muda wa kukusanya nguvu!

Tukirudi kwa ACT, hapa kuna tofauti kubwa sana kati ya CHADEMA na CCM! Wakati CCM hawapendi kuchukulia mambo kwa pupa, CHADEMA ni watu wa kuchukulia mambo kwa pupa huku wenyewe wakijidanganya ni watu wa kufanya maamuzi magumu! Kutokana na ukweli huo, sitarajii utulivu ambao ulikuwapo CCM wakati wa CCJ unaweza kuwapo CHADEMA na zama hizi za ACT! Kama walivyo viongozi wao, wanachama, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA wapo tofauti sana na wale wa CCM ambapo, kwa CHADEMA majaority ni watu wanaotawaliwa na papara na jazba kuanzia ngazi za juu mpaka chini! Wakati akina Samwel Sitta na wenzake waliachwa waendelee kufanya kazi zao bila bugudha, sina shaka hivi sasa tutashuhudia shutuma na tuhuma mbali mbali za kuchukiza dhidi ya wanachama wa CHADEMA watakaojihusisha na mtu kama Zitto kwa namna yoyote ile! Ingawaje wana-CHADEMA wanajipa matumaini kwamba kuondoka kwa Zitto hakuwezi kuwa na athari kubwa kwa chama lakini kila mwenye macho na ufahamu anafahamu fika kwamba kuondoka kwa Zitto ni jinamizi la kuogofya! Wakati mwaka 2010 CCM ilinuruika na jinamizi la CCJ kwa sababu kulikuwa na utulivu ndani ya chama, CHADEMA inaweza kukumbwa na msukosuko wa kutisha kwavile kuanzia ngazi za juu hadi chini ni watu wenye uhaba wa busara huku wakiwa ni wenye kutawaliwa na jazba. Tuhuma na shutuma mbalimbali za kuchukiza ambazo sina shaka zitafuata muda si mrefu dhidi ya baadhi ya wana-CHADEMA zitachochea wana-CHADEMA wengi zaidi kukimbia kwavile watajihisi hawapo salama tena ndani ya chama!

Binafsi, mtu pekee ninayemuona ana uwezo wa kuinusru CHADEMA ni Freeman Mbowe peke yake unless mtu kama Profesa Safari nae ataweza kupewa nafasi hiyo! Dr. Slaa, pamoja na ushawishi wake ndani ya chama pengine kuliko hata Mbowe, lakini kwa bahati mbaya Dr. Slaa anawakilisha kundi lile lile la wana-CHADEMA wanaotawaliwa na jazba!

Kutokana na hilo, ikiwa Freeman Mbowe atashindwa kuwadhibiti watu kama akina Tundu Lissu, Godbless Lema na wafia chama wengine, basi tutarajie mambo mabaya zaidi kwa CHADEMA! Ikiwa Dr. Slaa hatatumia ushawishi wake na ku-team na watu wenye busara kama akina Profesa Safari na Mbowe na badala yake aka-team na watu kama akina Lissu na Lema, basi tutarajie maafa zaidi kwa CHADEMA! Ikiwa wana-CHADEMA JF hawatakuwa na busara kama za akina Mbowe na badala yake kutawaliwa na akili za akina Tundu Lissu na hatimae kuanza kushusha nyuzi mfululizo JF dhidi ya huyu ama yule wanayemuhisi ni msaliti kiasi cha wao kuona hawana thamani tena, basi tutarajie maafa zaidi kwa upande wa CHADEMA!

Narudia, kitu pekee ambacho CCM kiliwanusuru na jinamizi la CCJ ni busara za uongozi wa CCM pamoja na wanachama wao kuanzia ngazi za juu hadi chini! I hate to say this, hii token haipo kwa upande wa CHADEMA ingawaje inawezekana kui-create! Kingine ambacho kiliinusuru CCM ni mkono wa Msajili wa Vyama vya Siasa... token hii pia, CHADEMA hawana! Lakini hata kama Msajili wa Vyama Vya Siasa ataamua kuihakiki ACT leo, sitarajii kwamba ACT wanaeza kuwa wajinga kama walivyokuwa CCJ! Isitoshe, Msajili afanye hivyo kwa maslahi ya nani? Maslahi ya CHADEMA? HELL NO unless kama sharia ndivyo isemavyo! Kutokana na ukweli huo, utaona kwamba, salama pekee ya CHADEMA ni uongozi wake kutumia busara na kuchulia kila kitakachosemwa kama tetesi tu! Kinyume chake, tusubirie the next episode!
 
Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, chama kipya cha kisiasa; CCJ kilianzishwa. CCJ ilikuja kwa kasi kiasi cha kuanza kuitia hofu CCM huku hofu hii ikichangiwa sana na maneno ya hapa na pale kuhusu uhusiano wa CCJ na wanasiasa waandamizi ndani ya CCM, hususani Samwel Sitta na Mwakyembe! Wengine ambao walihusishwa na CCJ ni pamoja na Nape Mnauye! Hata hivyo, ukongwe na busara za wana-CCM ukaifanya CCM kuto-panic ingawaje kulikuwa na watu waliokuwa wakihesabu siku washuhudie exodus from CCM to CCJ! Hili, halikutokea licha ya kumshudia Fred Mpendazoe akijitoa mhanga na kuwa mwana-CCM wa kwanza mwandamizi kujiunga na CCJ na wengine wakawa kana kwamba wanapima uelekeo wa upepo!

Kilichofanya CCM isitetereshwe na CCJ ni kutumia nguvu zake za dola na wala sio viongozi wa CCM kama unavyodanganya hapa. Kuanzia usalama wa taifa, polisi na msajili wa vyama, ofisi ya bunge, wakuu wa mikoa na wilaya walitumika kuhujumu CCJ. Halafu unasema ATC ni tishio kwa Chadema... tishio lake liko wapi na Chadema haina dola? Kwanini isiwe tishio kwa CCM yenye Dola? Huoni mna lenu jambo na jambo lenyewe ni kuhujumu upinzani? Nina taarifa zote na jinsi Zitto alivyoahidiwa uwaziri mkuu pindi Lowassa akishika madaraka. Nina taarifa jinsi Kikwete na Lowassa wanvyochezea watu akili ili ionekane kama wamekosana kumbe anamuunga mkono kwa kila jambo analofanya.
 
Unaonaje nikikupuuza?
 
Uzi huu umejawa na hekima sana, ni ushauri mzuri mno, Lakini ndugu yangu huna taarifa kuwa baada ya ZZK kuitisha PC na CHADEMA kimeitisha ya kwake ? tena same day? Huoni kama kuna kupanic kwa hali ya juu?.. Haitoshi hii kuwa ni tofauti kubwa ya CCM dhidi ya CCJ na CDM dhidi ya ACT? Safu ya CDM ni nyembamba sana na either wanakosa watu wenye hekima au waliopo wachache hawathaminiwi, kwa akili ya haraka tu walipaswa kumpuuza zitto kwa sasa na kuelekeza nguvu zao kwenye ujenzi wa chama....Lakini nani wa kufanya hayo? Lema? Sugu? Msigwa? Afande Sele?..
 
Hili la kwamba CHADEMA wameitisha Press Conference ndio nimeliona hivi sasa hapo jamvini... hata kuufungua uzi wenyewe sijaufungua na kama ndivyo, na kama watataka kuzngumzia suala la Zitto basi itakuwa ni mwendelezo wa matumizi ya papara kama sio namna ya kutaka kuwatisha wengine!
 
Ukweli ulio wazi Zitto ataondoka na wengi Chadema, wafuasi wengi wa Chadema wale makini wanaotumia fikra zao kupima mambo hawawezi kubaki Chadema.
 
CHADEMA sio sawa na CCM
CCM wana dola....wanatoa ajira serikalini
ndo maana kina Nape wakapewa ukuu wa wilaya na mwisho wakarudishwa kundini
kna Mwakyembe na Sitta wamepewa uwaziri

CHADEMA hawako in power...hawana nguvu ya kumshughulikia mtu that much
sanasana wakijifanya 'bize kuishughulikia ACT' itawa cost muda na pesa pia...

Kama Zitto akifanikiwa kupata wabunge kadhaa na ACT..
na CHADEMA wabunge wakipungua...most likely after uchaguzi wanaweza kuwa vyama sawa kwa nguvu
hakuna mkbwa wala mdogo......while CCM watakuwa still the power it is..
 
Supporters wengi wa Zitto ni ma CCM,na wale wengine ni wale wale waliokuwa nae.
Ni bora chama kishindwe uchaguzi kuliko kushinda kikiwa na Wahuni na wasaliti. NasDaz unataka kuishauri CHADEMA ifuate strategy za CCM kwa kufunika Kombe Mwana haramu apite.
CHADEMA iko Imara na haito tetereka kwa utabiri wa CCM ambao kwenye dua zao kila uchwao wanaomba CHADEMA ife
 
Last edited by a moderator:

Kufunika kombe mwanaharamu apite kivipi? Ni kufunika kombe ama ni kuwa watulivu! Si kwamba CCM hawakufahamu kuhusu akina Sitta na CCJ yao bali waliamua kuwa watulivu na kuchukulia ni kama tetesi huku wakipanga ni namna gani wangeweza kukabiliana na CCJ... huku sio kufunika kombe mwanaharamu apite, la hasha bali ni matumizi ya busara katika ku-handle matatizo makubwa! Kwa tabia ya CHADEMA, leo hii atokee mbunge au mwanachama yeyote wa CHADEMA akaonekana kuwa close na Zitto, basi mbunge ama mwanachama huyo ataanza kuangaliwa kwa jicho la usaliti na tuhuma chungu tele... katu huko hatuwezi kuita ni kushughulikia matatizo kwa staili tofauti na ile ya CCM!

Kwamba CHADEMA ipo imara, binafsi sijui isipokuwa nilicho na uhakika nacho ni kwamba hivi sasa kinapita kwenye mtihani mzito! Jazba na papara zikichukua nafasi ya busara, basi nina mashaka ikiwa kauli yako utaweza kuisimamia kwa miezi kadhaa ijayo... kuisimamia kwa uhalisia na sio kwa ushabiki!
 
Kufunika kombe mwanaharamu apite kivipi? Ni kufunika kombe ama ni kuwa watulivu! Si kwamba CCM hawakufahamu kuhusu akina Sitta na CCJ yao bali waliamua kuwa watulivu na kuchukulia ni kama tetesi huku !
NasDaz ,

Hiyo Hapo juu ndio Tafsiri ya Kufunika Kombe Mwanaharamu apite
 
Last edited by a moderator:
NasDaz ,

Hiyo Hapo juu ndio Tafsiri ya Kufunika Kombe Mwanaharamu apite
Utulivu na ustahimilivu ni tunda la busara wakati funika kombe ni tunda la kuficha au ku-entertain uovu... haya hayawezi kuwa mambo yaliyo sawa!
 
Habari kaka NasDaz,

Nadhani kuna utofauti Mkubwa sana kati ya CCJ na ACT, japo vina fanana kwa minajili ya kuwa vimetokana na wanachama waliotoka kwenye Vyama vyao na kuunda hivyo vyama

Nadhani kabla ya kufanya uchambuzi wa hivyo vyama ni muhimu kuijua CCM na Nguvu zake

Serikali ya CCM ndio inayo control Police, TISS, NEC na Msajili wa Vyama vya siasa, CCJ kilikuwa ni Chama cha kweli na kilikuwa ndio anguko kuu la CCM, Watu kama Mwakyembe, Nnape, Sitta, Mpendazoe na wengine walishajipanga vizuri nadhani wakiwa na back up ya kina Warioba na wenzie (Butiku, Salim, ect),
CCM kwa kuiona hiyo hatari kupitia labda TISS yake, walitumia rungu la Msajili wa Vyama vya siasa kui-disqualify CCJ kwamba haijatimiza sharti la kuwa na wanachama nchi nzima, Na huo ndio ulikuwa Mwanzo wa mwisho wa CCJ huku watu kama Mpendazoe wakisha jitumbukiza shimoni

Kwa Upende wa ACT ni tofauti, Vyombo vilivyotumika kuiangusha CCJ ndio vinatumika kuiinua ACT
Chama Cha ACT kina mapungufu makubwa ya kiusajili ambayo yako wazi sana, lakini Msajili wa vyama ameamua labda kwa kushinikizwa kukipa usajili hicho chama, Chama Hakina Katiba ya kueleweka, Hakina viongozi wa kueleweka, Hakina Bendera ya kueleweka na hakina Nembo ya kueleweka lakini kimesajiliwa na Msajili wa vyama vya siasa.

Kwa sasa Kuna kesi ya kiuongozi ndani ya ACT believe me hiyo kesi , wakina Zitto lazima washinde kwa sababu wana backup ya CCM ambayo ndio inaongoza taasisi zote muhimu nchini (Ikiwemo Mahakama) sio kwa minajiri ya kiutendaji bali Kisiasa zaidi

CCJ ilikufa kwa nguvu nilizoziainisha hapo juu,
Ila ACT itadumu mpaka mwisho wa uchaguzi wa Mwaka huu 2015 kwa sababu itabebwa na TISS, NEC, CCM na Msajili wa vyama wote wakiwa na lengo la kuiyumbisha na kuipotezea nguvu Chadema.,
Lakini baada ya uchaguzi kuanzia 2016 mpaka uchaguzi mwingine 2020 kutakuwa hakuna Chama cha ACT, chama kitakuwa kimeshakufa
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom