CCM mwisho kule Msata, Mjini kote CHADEMA tupu hivi sasa.

CCM mwisho kule Msata, Mjini kote CHADEMA tupu hivi sasa.

Kamanda Francis

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2013
Posts
834
Reaction score
140
NASUBIRI USHAHIDI ILI NIAMINI KUWA CCM NA SERIKALI YAO SIO WAJINGA KUZUIA MAANDAMANO YA AMANI NCHINI

Wakuu, awali yote nikiri kuwa, ni kweli kwa muda nimekuwa kimya kiasi chake, ila sio kweli kama nilivyoelezwa kupitia simu za mkononi, sms, email na Inbox ya facebook na Whasap kwamba, kuna uvumi mitaani kuwa baada ya Uchaguzi wa BAVICHA kumalizika nilikihama Chama changu (CHADEMA) na kuandaa taratibu za kuhamia ACT-Tanzania.

Binafsi nakanusha na kuulaani vikali uvumi huu unaoenezwa na wapuuzi wachache wasiokitakia mema Chama chetu (CHADEMA) kinachojiandaa kushika dola baadae mwaka ujao, baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Baada ya ufafanuzi huo, ikumbukwe kuwa, kwa muda wote nimekuwa nikisema, "CCM mwisho kule Msata, Mjini ni CHADEMA tupu" nakumbuka wengi wenu mlinibeza sana, lakini jana ilidhihirika pale mitaa ya Posta mpya, kwenye viwanja vya Wizara ya Mambo ya ndani, hata Diwani wa Kinondoni (Chadema) Boniface Jacob, aliishuhudia nguvu ya umma inavyofanya maamuzi.

Jeshi la Polisi maarufu kama "POLICCM" walitaka kumgeuzia kibao Mwenyekiti wa Chama chetu Mhe.Freeman Mbowe ili watimize azma yao ya kutaka kumdharirisha kwa kumpeleka Rockup Kituo Cha Polisi Central, bahati nzuri, wapambanaji tukaudaka fasta mpango ule dhaifu na wa kijinga, ikabidi tujipange kukabiliana na hali husika.

Baada ya majamaa kuusoma upepo kupitia Intelejensia wao waliokuwa wamewapandikiza kwetu, ikabidi waanze kuhaha na kutokwa povu, ili hali yule kinara wao wa vyombo vya habari, akishindwa kutulia Ofisini, ikamlazimu achungulie dirishani akiwa ghorofani, ndipo akagundua kuwa, huku chini kulikuwa na nyomi la kufa mtu, ikabidi kwanza aingie msalani fasta, maana alipatwa na uhalo wa tumbo ghafla.

Baada ya kutoka msalani, fasta akamfata Mwanasheria wetu wa Chama Mhe.Tundu Lissu ili ashuke chini aweke mambo sawa, maana tayari huku chini tulikuwa tumeanza kukinukisha ili Mhe.Mbowe aruhusiwe haraka sana tuondoke naye.

Mhe.Lissu kwa huruma ya ubinadamu, akamwonea huruma yule kinara wa Polisi anayehangaika na maandamano haya ya umma, akashuka mpaka tulipokuwa, na kwa heshima ya Chama na kwa niaba ya Mwenyekiti wetu, akatuomba na kutusihi kuwa wapole huku akituhakikishia kuwa Mhe.Mbowe ataachiwa huru kwa dhamana, na atasindikizwa na Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo Mtaa wa Posta mpya mpaka Makao Makuu ya CHADEMA, Mtaa wa Ufipa Kinondoni, tena kwa Gari lenye king'ora, na kweli ikawa hivyo, ndipo sie sote tukaondoka kuelekea Makao Makuu ya Chama Kinondoni.

Tulipofika Makao Makuu ya Chama pale Kinondoni, Mhe.Mbowe alitoa shukrani zake za dhati kwa wafuasi, wanachama, wapenzi na wakereketwa wote wa CHADEMA Nchini kote, walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kumpigania dhidi ya hawa maharamia wanaotumiwa na Chama tawala kwa maslahi binafsi badala ya kuwatumikia wananchi ambao ndio wanaolipa kodi zinazowafanya walipwe stahiki zao, licha ya kwamba kila kukicha wanavaa pea moja ya viatu na sare moja ya kauka haraka nikuvae.

Mhe.Mbowe alituasa kwamba, kuanzia sasa, kwa kuwa tunaelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tarehe 14/12/2014, kila mmoja wetu kwa eneo lake analotokea, ahakikishe kwamba kuna msingi wa CHADEMA wenye wanachama wasiopungua 200, hususani kwa wapambanaji wa Jiji la Dar Es Salaam ambako niko kitovu cha Nchi.

Naye Mhe.Tundu Lissu alisema, atawashangaa sana Jeshi la Polisi na Serikali hii kiziwi ya CCM, kama wataipeleka kesi ile mahakamani kwa lengo la kumshitaki Mhe.Mbowe. Pia Mhe.Lissu alisema na kusisitiza kuwa, tunapoandika Barua za Maandamano ya Amani au Mikutano ya hadhara ya Kichama, tugakikishe kwamba, kichwa cha habari kinasomeka hivi; "YAH:TAARIFA YA KUFANYA MAANDAMANO YA AMANI" AU "YAH:TAARIFA YA KUFANYA MKUTANO WA HADHARA WA CHAMA CHA SIASA"

Mhe.Lissu alisisitiza hivyo kwa sababu, hakuna Sheria yoyote ile ndani ya Nchi hii inayowapa mamlaka Jeshi la Polisi kutoa kibali cha Maandamano au Mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa, isipokuwa jukumu lao pekee ni kuhakikisha kuwa Ulinzi na Usalama unaimaarishwa kwa wahusika, na hilo ni lazima kwao kutekeleza na sio ombi, na Jeshi la Polisi wanafahamu vizuri utaratibu huu wa Kisheria, ila wanaamua kuitumikia CCM ili kulinda tumbo zao tu, na si vinginevyo, huku wakiutumia udhaifu wetu wa kutozifahamu Sheria za Nchi yetu, maana Sheria nyingi zimeandikwa kwa Kiingereza na nadra sana kuziona.

Imeandikwa Na:

Francis Boniface Katibu BAVICHA, Serengeti, Mara, Tanzania. 19/09/2014. ***************** 0785881009/0767881009 francisboniface50@gmail.com

Ahsanteni sana!!!
 
Kweli bwana ukimpenda mtoto hata kama ni kichaa cha kuvua nguo hadharani, kuvunja mali za ndani na hata kuumiza wengine utakuwa radhi. Bora mapenzi yatimizwe!!!!!!
 
Jana polisi mkoani Arusha
walifanya maandamano mji
mzima wa Arusha na
viunga vyake bila kulindwa
na hatimae maandamano
yao yakaisha salama bila
vurugu.
Maandamano ya Polisi
yaliyofanyika jana bila
vurugu yamenikumbusha
maandamano ya CHADEMA
yanayofanyika huku
wakijilinda wenyewe!
Maandamano ya CHADEMA
huwa ya amani na
humalizika bila vurugu au
hata mende kuuwawa
wakifanya maandamano
kwa kujilinda wao
wenyewe.
Polisi kazi yao na wajibu
wao ni kulinda
maandamano na
kuhakikisha kuwa
yanakuwa ya amani huku
wakihakikisha azma ya
waandamanaji ina timia
bila amani kutoweka,
wanapaswa kulinda
maandamano na
kuyasindikiza huku
wakihakikisha usalama wa
raia na mali unakuwepo.
Maandamano ya jana ya
Polisi yalikuwa ya aina
yake! Waliandamana bila
kupata kibali kwa aliye
yatangaza, polisi hawaja
wahi kutangaza
maandamano na
kuandamana, jana
imekuwa mshangao! Aliye
tangaza maandamano ya
kupinga ubadhirifu unao
endelea Dodoma ni
Mbowe, maandamano ya
kupinga kinacho endelea
Dodoma bado hayaja anza
rasmi, kulikoni Polisi
waanze kuingia road?!
Na kama huwa wanajua
kuandamana bila vurugu
kwa nini huwa wanaingilia
maandamano ya CHADEMA
na kujeruhi waandamanaji
wasio na hatia?
Jana nimeona kwenye
taarifa ya Habari ya ITV eti
"Chadema wawapa polisi
wakati mgumu..." nimebaki
nashangaa, aliye jipa
wakati mgumu kwa
kuandamana kabla ya
muda na kuandamana bila
ridhaa ya aliyetoa agizo la
kupinga kinacho endelea
Dodoma ni nani?!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom