CCM Msituchonganishe!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Msituchonganishe!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mnyamahodzo, Apr 9, 2011.

 1. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ni tabia ya mchawi kuwa anapoona sasa anakaribia kuumbuka huwachonganisha watu kwa kauli na vitendo vyake.
  Uchawi ni wa kwenu ninyi wenyewe kama mlinunua ama kurithishwa sisi halituhusu; pokeeni madhira ya uchawi wenu na mfitinike ninyi kwa ninyi. Lakini sisi msituchonganishe.

  CCM hamna maono ya kujenga hata choo cah kutumiwa miaka 20, majengo na vitega uchumi mlivyonavyo ni vile walivyojenga watanzania kwa nguvu zao ama kwa kutumia dola mkavipata. Mlitumia "janjawid" kuharibu taasisi za umma na kusingizia CUF. Mkalilipua jengo la ilipoanzishwa TANU kwa bomu la TNT mkasingizia CUF (wapemba walioko kariakoo na magomeni).

  Mmetawanya meseji za uchochezi wa ukabila na udini, mkazipigia upatu kwenye kampeni 2010 na kusema ni chama fulani wengine wakataja wazi ni CHADEMA. Mliwaanda vijana wenu kwa mafunzo rasmi ili kuleta fujo kabala na siku ya uchaguzi ili damu ya ndugu zetu, rafikii,jamaa na wazazi wetu imwagike na wengine wapoteze viungo mseme ni caham fulani ninyi mkiendelea kustarehe.

  Uzembe wa serikali ya CCM umesababisha hali ya maishe kuwa ngumu/aghali zaidi, ujinga kwa wanafunzi wanaohitimu kuongezeka, ufujaji na uporaji wa mali ya umma kuongezeka, mauaji kwasababu ya uzembe wa serikali (kuanzia Pemba, Bulyanhulu, Mara, Arusha, Mbarali, Mbagala na Gongo la Mboto, kwa uchache, na sasa Loliondo saga na "tiba ya kikombe") kuongezeka. Tunapohoji ama kuyalalamikia hayo na mengine mengi mwatugawa kwa misingi ya itikadi/imani zetu za kidini. Yakwamba "wao wa 'dini ile' ndiyo wanayasabibsha haya" au "wale wa dini ile wanaonawivu kwa sababu serikali inaongozwa na mtu wa dini yetu wanataka kumkwamisha" CCM Msituchonganishe!!

  Mlipotuchonganisha kwa vyama hamkupata matokeo mliyotegemea, kiukabila vivyo hivyo.
  Mchezo mnaotumia kutuchonganisha kwa kutumia imani za kidini na uhuru wa mawazo yetu na hatima yetu ni hatari zaidi.
  La imani za kidini sitaligusia sana lakini napenda hili la "uhuru wa mawazo yetu na hatima yetu", kwa ufupi niseme mchakato mzima wa kupata katiba mpya.

  Katiba tunayoitaka ndiyo itakayoamua ustawi wa Tanzania ya leo na miaka 100 ijayo. Hatupendi kuona damu ya mwana yeyote wa nchi hii ikimwagika ama kiungo kumtoka kwasababu ya kutoa mawazo yake juu ya utengenezaji Katiba bora ama utekelezaji wa Katiba mpya itakayopatikana. Mmeanza mchezo mchafu, mnauita umma kushiriki kutoa mawazo yao na wengine wayasikilize lakini mnawaweka katika eneo la kuchukua watu 300-500. Wengine mwawatenga kwa kutumia ukuta, na kutorusha matangazo katika vyombo vya habari Radio na TV za Taifa ya moja kwa moja. CCM mwatumia pesa kuwaleta (watoto na wakubwa) wavurugaji katika kulijadili suala hili nyeti. Tugombane sisi, ninyi muendelee kuchekelea. Mmesababisha Fakihi Mwakisu kutolewa meno na "janjawid" wenu. Hamko tayari kumtibu wala kumlipa fidia yoyote mwana mwema huyu aliyekwenda kutoa mawazo yake sahihi kwake, sawa sawa na wito. Hivi mmejiuliza, kundi la wale wanaopinga muswada huu nao wangeamua kujibiza mapigo kumwokoa Mwakisu nini kingetokea?

  Yatosha sasa!! Watu kuumizwa na kufariki kwa sababu ya kutetea au kuyapinga mawazo yenu yenye ujinga. Hatukuzaliwa Tanzania ili tufe kwasababu ya ujinga wenu.

  CCM Msituchonganishe!!
  Tutafika wakati kwa kila kijana atayeumizwa ama kuuliwa na sisi turudishe mapigo si kwa raia kijana bali kwa watoto zenu. Na kwa kila mzee, basi mapigo yake kwenu na kwa waume ama wake zenu. Yaani, mzee akiuliwa kwasababu CCM walituchonganisha, basi wataraji kiongozi katika mtandao huo naye kuuliwa, akivunjwa mguu na sisi tutavizia na kuvunja mguu. Ndiyo!! Ni uamuzi mgumu. Lakini tufanye nini kama ninyi mnatuchonganisha hata ndugu zetu wanaumia ama kufa kwa maslahi yenu ilhali ninyi na watoto mwaneemeka tu. Hamjui kuonja maumivu ya misiba yetu, tutawaonjesha kwa lazima.

  CCM Msituchonganishe.

  Naomba msaada toka kwa mwanaJF yeyote kutuwekea zile picha za wale vijana waliokodiwa na CCM kwenda kuleta fujo siku ya mjadala wa rasimu ya Katiba mpya (09/04/20110) pale Karimjee Hall. Mimi sifahamu
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Bei halali ya amani na utulivu ni kutenda haki sawa kwa wote sio hila za mabaunsa na watoto wanaopata div 0 kwenye shule za kata!
   
 3. Lighondi

  Lighondi JF-Expert Member

  #3
  Apr 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 585
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Maumivu ya kichwa huanza poooole pole. Hata Ivory cosy haikuchanganya siku moja!!
   
 4. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #4
  Apr 9, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ni kweli!!

  Hilo lina-apply maeneo mengi kwasasa.Kiuhalisisa mabaunsa wengi wanatumiwa sana na CCM (viongozi wa CCM) kulinda maslahi yao. nao wamekuwa na kiburi fulani kwasababu wanaukaribu mna mheshimiwa au fulani.

  Jingine ni kuwa kuwa, ukiangalia picha kutoka gazeti la tanzania Daima na Nipashe ya Jumamosi tarehe 9/4/2011 unaweza ukazungumzia vema kiwango cha elimu hadi uelewa wa watoto wale waliokodishwa kwenda kuleta fujo pale Karimjee Hall. inasikitisha. wakati kuna watu wako makini kusikiliza wao ni kuchekacheka na vituko lukuki.

  Mwana JF naomba utuingizie zile picha(za watoto waliokodishwa na CCM kwenda Karimjee Hall) hapa ilitwende sambamba na mada.
   
Loading...