Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,330
- 33,961
Wakati Tundu Lissu aliposhambuliwa ilidhaniwa kwamba CCM kama chama na wanachama wake binafsi wataweka chuki zao dhidi ya CHADEMA na dhidi ya wanachadema na kwa kuonesha hisia za kiutu kwa kushambuliwa kwa Lissu. Lakini CCM walipita njia tofauti kabisa tena ya kikatili.
CCM kila mara imekuwa inatoa mtizamo unaokinzana na hali halisi ya matendo yake. Wakati Alphonce Mawazo ameuawa, Polisi kuzuia mazishi yake mpaka kesi kwenda Mahakamani, CCM iliwataka CHADEMA "wawe na utulivu"
CHADEMA wanawezaje kuwa na utulivu wakati kiongozi wao kauwa na kama chama wanazuiwa kufanya mazishi wanayoona yanastahili kwa kiongozi wao? Hivi CHADEMA wanawezaje kuwasikiliza CCM wakati kiongozi wao kauawa na watu wanaoshukiwa kuwa ni wana CCM?
CCM imekuwa inawatendea matendo mengi sana maovu watu wa CHADEMA na hapo hapo huwataka wana CHADEMA wawe wema kwa matendo maovu wanaoyotendewa ama na CCM wenyewe ama na CCM kwa kutumia vyombo vya dola.
Ili CHADEMA wawe wema inabidi CCM wawe wema kwanza!!