CCM msitake CHADEMA wawe wema mnapowadhulumu!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,034
33,514
Wakati Tundu Lissu aliposhambuliwa ilidhaniwa kwamba CCM kama chama na wanachama wake binafsi wataweka chuki zao dhidi ya CHADEMA na dhidi ya wanachadema na kwa kuonesha hisia za kiutu kwa kushambuliwa kwa Lissu. Lakini CCM walipita njia tofauti kabisa tena ya kikatili.

CCM kila mara imekuwa inatoa mtizamo unaokinzana na hali halisi ya matendo yake. Wakati Alphonce Mawazo ameuawa, Polisi kuzuia mazishi yake mpaka kesi kwenda Mahakamani, CCM iliwataka CHADEMA "wawe na utulivu"

CHADEMA wanawezaje kuwa na utulivu wakati kiongozi wao kauwa na kama chama wanazuiwa kufanya mazishi wanayoona yanastahili kwa kiongozi wao? Hivi CHADEMA wanawezaje kuwasikiliza CCM wakati kiongozi wao kauawa na watu wanaoshukiwa kuwa ni wana CCM?

CCM imekuwa inawatendea matendo mengi sana maovu watu wa CHADEMA na hapo hapo huwataka wana CHADEMA wawe wema kwa matendo maovu wanaoyotendewa ama na CCM wenyewe ama na CCM kwa kutumia vyombo vya dola.

Ili CHADEMA wawe wema inabidi CCM wawe wema kwanza!!
 
Majizi chadema ndiyo mashetani wa nchi hii

Kila siku wanaiombea mabaya nchi yetu
 
kuonesha hisia ya kuumia wakati mwengine kakumbwa na tatizo si suala la kuilaumu CCM kwa sababu kila hulichukulia jambo kwa kadiri mtu linavyomgusa. CCM kuna watu ambao wanahisia tofauti pia , wengine walimuombea Tundu Lissu na wengine walienda kumuona hospitali. usilazimishe kila mtu achukulie jambo kama unavyolichukulia wewe

unaposema CCM inawatendea mambo mengi CHADEMA hueleweki kwa sababu vyama vyote vya siasa vimewekewa taratibu za kujiendesha na CCM ndio inasimamia taratibu hizo kwa kuwa ndio ipo madarakani. uzuri wa taratibu hizo hata CCM zinawahusu na wanawajibika nazo. unataka CHADEMA wanapovunja sheria za nchi serikali inayooongozwa na CCM iangalie tu ?

umeonesha hisia zisizo sahihi kwa sababu vyama vya upinzani tanzania vipo vingi na si CHADEMA tu. kwa nini huifanye chadema so special kuliko vyama vingine? kwani hayo maonezi ya CCM hayapo kwa ACT? Kama hayapo why? hamuoni kwamba CHADEMA ndio mna tatizo?
 
FPT umeongea kama CCM wanavyoongea. Hivi wewe unadhani CCM huwa wanapambana na kila chama ama hupambana na kile chama tu kinachohatarisha uwepo wake madarakani?

Nikukumbushe tu kwamba baada ya uchaguzi wa mwaka 1995 ni NCCR -Mageuzi ndiyo ilikuwa inaandamwa, baada ya uchaguzi wa mwaka 2000 na 2005 ni CUF ilikuwa zamu yao! Kuanzia mwaka 2010 hadi sasa ni CHADEMA ndiyo wanaandamwa.

Hivi kwa akili za kawaida ni kweli unadhani CCM walifurahia Lissu kunusurika kuuawa
 
Eti wanataka tuwe pamoja kama taifa, wakati wanapofanya hujuma za wazi wanajiona wana haki miliki ya nchi hii. Sasa hivi box la kura haliheshimiwi kisa ccm washinde. Wapinzani wakishiriki uchaguzi hasa cdm wanafanyiwa ukatili na hujuma za wazi, na ukatili huo unaratibiwa na vyombo vya dola kwa amri ya mkulu. Wapinzani wameamua kususia ili malalamiko ya hizo hujuma yafanyiwe kazi, lakini kinachoendelea ni kejeli na dhihaka eti ukisusa wenzio wala. Safari hii watakula kibichi. Mzungu achukue hatua haraka wapinzani tumechoka na dhuluma ya genge liitwalo ccm. Mkuu kakabidhiwa nchi aongoze lakini inaonekana yuko kwa maslahi ya ccm na hujuma dhidi ya wapinzani.
 
Wakati Tundu Lissu aliposhambuliwa ilidhaniwa kwamba CCM kama chama na wanachama wake binafsi wataweka chuki zao dhidi ya CHADEMA na dhidi ya wanachadema na kwa kuonesha hisia za kiutu kwa kushambuliwa kwa Lissu. Lakini CCM walipita njia tofauti kabisa tena ya kikatili.

CCM kila mara imekuwa inatoa mtizamo unaokinzana na hali halisi ya matendo yake. Wakati Alphonce Mawazo ameuawa, Polisi kuzuia mazishi yake mpaka kesi kwenda Mahakamani, CCM iliwataka CHADEMA "wawe na utulivu"

CHADEMA wanawezaje kuwa na utulivu wakati kiongozi wao kauwa na kama chama wanazuiwa kufanya mazishi wanayoona yanastahili kwa kiongozi wao? Hivi CHADEMA wanawezaje kuwasikiliza CCM wakati kiongozi wao kauawa na watu wanaoshukiwa kuwa ni wana CCM?

CCM imekuwa inawatendea matendo mengi sana maovu watu wa CHADEMA na hapo hapo huwataka wana CHADEMA wawe wema kwa matendo maovu wanaoyotendewa ama na CCM wenyewe ama na CCM kwa kutumia vyombo vya dola.

Ili CHADEMA wawe wema inabidi CCM wawe wema kwanza!!
Huwaga nawashangaa mnafanyiwa uharamia mnakaa kimya angali mnajua wanapoishi
 
Majizi chadema ndiyo mashetani wa nchi hii

Kila siku wanaiombea mabaya nchi yetu
Nchi ya inayongozwa na hawa vichwa maji si bora ife kabisa..! Uliwahi kuona nani anatuhumiwa kwa wizi aliye chadema, utasema lowassa na sumaye, ila ujue walikuwa majizi wakiwa ccm walipohamia chadema wakaokoka.

Mimi ccm ila kuna upuuzi tunaufanya sisi wenyewe dunia ikiingilia eti anatafutwa mchawi ujinga mtupu.
 
Back
Top Bottom