CCM msijifariji kwa vile Wananchi wapo kimya

Elice Elly

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
1,268
1,593
CCM ni kweli Wananchi wapo kimya, lakini msidhani ukimwa huu wa Wananchi ni kuonyesha kuwa wanafurahishwa na mambo yanayoendelea. Watu wengi wana hasira moyoni na wapo kimya kwa sababu wanajua wakiongea watakutana na kesi za uhujumu uchumi. Lakini ukitaka kujua hasira walizo nazo wananchi juu yenu angalia mifano midogo tu waliyoonyesha wananchi wiki hii.

Huko Kongwa Wananchi wamemkataa Mbunge wao (Spika Ndugai) Mbele ya huku Rais akiwa amevaa Magwanda ya jeshi, kumbuka Raia wakiona magwanda ya Jeshi huwa wanaogopa sana, lakini safari hii pamoja na magwanda hayo kuvaliwa na Mkuu wa nchi.

Huko Mwanza nako kiilicho mpata Naibu Waitara wote tulishuhudia,Hizi siyo dalili nzuri.Wananchi pamoja na kujua kuna kesi za uhujumu uchumi, kutekwa, mambo yanayofanana na hayo ni wazi sasa wanaonyesha dalili za hofu kuondoka ndani yao.

Matukio haya yananikumbusha mambo yaliyowahi mtokea marehemu Kleruu kule iring,zamani watu wakisikia kuna kiongozi Fulani wa serikali amekuja katika kijiji Fulani watafunga safari kwa miguu kwenda kumsikiliza tena kwa utulivu Mkuu, lakini sasa yanayoendelea wote tunashuhudia.

Na mambo haya ni viongozi wenyewe pamoja na CCM mmejiandalia na kwa kugundua kosa lenu mmeamua kufanya kosa jingine yaani kuwanyamazisha watu kwa kutumia Vyombo Vya dola na kesi za uhujumu uchumi.

Tambueni tu hayo yote hayawezi kuwafanya watu wawe mazezeta, Muda ukifika utakuwa shahidi mzuri.

IMG-20200507-WA0026.jpeg
 
Mkuu Watanzania wengi wapo Ccm hizi kalele za watu mia mtandaoni zisikudanganye
 
Kwangu Mimi hii ndiyo thread Bora ya mwezi huu Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu atakubaliana na ushauri wako
 
Back
Top Bottom