CCM mnatekeleza ilani ipi?

CCM mnatekeleza ilani ipi?

Gagnija

Platinum Member
Joined
Apr 28, 2006
Posts
13,777
Reaction score
14,653
2020 ballot paper ilikuwa na picha ya Magufuli na mgombea mwenza Samia. Baada ya March 2021, inaonekana kila alilofanya Magufuli lilikuwa baya.

Ni ilani ipi mnayotekeleza? Au chama kina ilani zaidi ya moja!


​
 
Ilani kwa CCM ni kama toilet paper.

Hebu ona wanasema wajawazito huduma ni bure, mjamzito kakosa 150k kajifia.

Waziri wa mchiriku(kwangu mimi hafai na hana vigezo vya kuwa waziri wa afya labda dunia ianze upya)

Ameunda tume ambayo itatumia zaidi ya 150k huku familia ikiachwa na majonzi na mzigo wa watu kufutiwa leseni na kuachishwa kazi imekua kama jumba bovu kwao.

Sasa mama anakosa 150k ya upasuaji huku Samia ananunua kila goli millioni 10 na bado wenza wa viongozi wanadai mafao.

Ilani hapo ni kama toilet paper tu.
 
..binafsi sijaridhika na serikali yetu kuwapa Dp world 40% ya mapato kwa ahadi ya uwekezaji wa usd 250 mil.

..naamini sisi wenyewe tungeweza kupata hizo usd 250 mil na kuajiri wataalamu watakaosaidia kuboresha mifumo iliyoko bandarini.

..kwa maoni yangu mkataba huu umelazimishwa tu ili genge la watu fulani ktk serikali na Ccm litengeneze pesa.
 
2020 ballot paper ilikuwa na picha ya Magufuli na mgombea mwenza Samia. Baada ya March 2021, inaonekana kila alilofanya Magufuli lilikuwa baya.

Ni ilani ipi mnayotekeleza? Au chama kina ilani zaidi ya moja!

hakuwa na ilani wala Samia hana ilani, ilani ni ya CCM, hivyo serikali ya CCM inatekeleza ilani ya CCM ya 2020-2025.
Sii kweli kuwa kila alilofanya Magufuli lilikuwa baya, bali kuna baadhi tuu ya mambo Magufuli hakuyafanya vizuri, Samia anarekebisha lakini hayahusu ilani.

Miongoni mwa mambo ambayo Magufuli hakuyafanya vema ni issues za demokrasia kwa kuzuia mikutano ya siasa, Samia karuhusu. Issues za kukamatana kwa kukomoana kuozea jela Samia ameondoa!, mambo ya watu kupotea na miili kuopolewa baharini kwenye viroba, hayapo tena, na kikundi cha wasiojulikana kimekuwa disbanded.

Mengine yote utekelezaji wa ilani ya CCM unaendelea na sasa kumteua msimamizi mpya wa utekelezaji wa ilani.

P
 
2020 ballot paper ilikuwa na picha ya Magufuli na mgombea mwenza Samia. Baada ya March 2021, inaonekana kila alilofanya Magufuli lilikuwa baya.

Ni ilani ipi mnayotekeleza? Au chama kina ilani zaidi ya moja!

Ilani yetu ni kuirudisha tanzania utumwani mwa muarabu haraka iwezekanavyo.
 
Back
Top Bottom