Uchaguzi 2020 CCM mnachekesha, mliwatia woga wa bure wateule waliotaka kutia nia kuwania Ubunge. Vipi kuhusu hawa?

MwajabuOmary

JF-Expert Member
Jul 11, 2013
236
209
Wakati wa mchakato wa kuwapata wagombea na hasa wa Ubunge, viongozi wa ngazi za juu kabisa za chama walijinadi kwamba wana CCM wote waliokua katika nafasi za kuteuliwa na Mkuu majina yao yatakatwa.

Makatazo haya yalikua yakirudiwa mara kwa mara na hata kuwatia uoga baadhi ya wana CCM waliokua na sifa za kugombea kuogopa kwenda kugombea.

Cha kushangaza ni kwamba mambo yamekua kinyume, yupo bwana:-

Godwin Kunambi
Patrobas Katambi
Christopher Ole Sendeka
Kitila Mkumbo
Mrisho Gambo

Kwa matamko yale ya awali, ni nini ambacho mlikua mnakiwakilisha?
 
Kwa uelewa wangu hawakukatazwa mkuu, waliambiwa nafasi zao za kuteuliwa hazitaachwa wazi, ukiomba likizo ili ukagombee ubunge nafasi yako inakua replaced hakuna back up plan kama Miaka ya nyuma.

wengi Wa wateule wa mh Raisi waliogopa kujitosa kwa Sababu ya kuogopa “mtaka mawili moja umponyoka“

Hao wateule waliojitosa kwenye ubunge ni mashujaa na inaonesha kwa jinsi wasivyo waroho wa madaraka waliona liwalo na Liwe ilimladi wasimamie wanachokipenda.
 
MwajabuOmary,

Hilo lilikuwa tamko la serikali kulingana na katiba kuwa ukitaka kugombea inabidi uache madaraka ya kiserikali ya kuteuliwa ambayo hayatokani na kuwa mbunge.

Kwa hiyo wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi wote inabidi waache madaraka hayo. Wanaoruhusikwa kubaki na madaraka ni rais, mawaziri na Spika tu kwa vile madaraka hayo yanatokana na kuchaguliwa tu.
 
Kwa uelewa wangu hawakukatazwa mkuu, waliambiwa nafasi zao za kuteuliwa hazitaachwa wazi, ukiomba likizo ili ukagombee ubunge nafasi yako inakua replaced hakuna back up plan kama Miaka ya nyuma

wengi Wa wateule wa mh Raisi waliogopa kujitosa kwa Sababu ya kuogopa “mtaka mawili moja umponyoka“

hao wateule waliojitosa kwenye ubunge ni mashujaa na inaonesha kwa jinsi wasivyo waroho wa madaraka waliona liwalo na Liwe ilimladi wasimamie wanachokipenda

Huu ndio ukweli
 
Back
Top Bottom